Kiti Kitakatifu:Kwa nchi za Visiwa Vidogo(SIDS)kunahitajika mfumo imara kufikia SDG
Vatican News
Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika taarifa yake tarehe 9 Julai 2026 huko New York, Marekani katika Majadiliano ya Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu (HLPF) la 2026 kuhusu Mikakati ya Mafanikio ya Maendeleo Endelevu (SDG) katika Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo (SIDS), alikaribisha na kwamba “zinatambuliwa kama "kesi maalum ya maendeleo endelevu kwa kuzingatia udhaifu wao wa kipekee."
Ajenda ya Antigua na Barbuda ya SIDS (ABAS)
Ajenda ya Antigua na Barbuda ya SIDS (ABAS) inatoa mfumo muhimu wa kushughulikia changamoto za kiuchumi, kijamii na kimazingira zinazohusiana ambazo nchi hizi zinakabiliwa nazo. Hata hivyo, kuharakisha maendeleo kuhusu Maendeleo endelevu (SDG) katika nchi zinazoendelea za Visiwa Vidogo(SIDS) kunahitaji zaidi ya mfumo imara; juhudi za maendeleo lazima pia zibaki zikizingatia utu wa mwanadamu uliotolewa na Mungu na kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu.
Suala la SIDS la kupata njia za utekelezaji zinazohitajika ili kufikia SDG
“Ni muhimu kusisitiza kwamba viashiria vya kawaida vya kiuchumi havioneshi kikamilifu hali halisi inayokabiliwa na SIDS,” alisisitiza mwakilishi wa Kudumu wa vatican. Viashiria hivi havioneshi vya kutosha udhaifu wa kipekee na ambao mara nyingi kuna uficho wa SIDS. Hili ni muhimu sana linapokuja suala la SIDS kupata njia za utekelezaji zinazohitajika ili kufikia SDGs.
Waraka wa Magnifica Humanitas na wito kwa Jumuiya ya Kimataifa
Katika Waraka wake wa hivi karibuni wa Baba Mtakatifu Leo XIV wa Magnifica Humanitas, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican alisema, “alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusonga mbele zaidi ya vipimo vya maendeleo vilivyounganishwa na pato la taifa (GDP), ambalo "karibu hupuuza vipengele muhimu kwa ustawi wa jumla wa watu na mazingira." Badala yake, “ni muhimu kutekeleza "tathmini kamili na ya wakati unaofaa ya jinsi maamuzi ya kisheria na ya udhibiti yanavyoathiri heshima ya kazi, ustawi wa pamoja, kupunguza ukosefu wa usawa na ulinzi wa mazingira."
Maono yanayofaa kwa SIDS
Maono haya yanafaa hasa kwa Ajenda ya Antigua na Barbuda ya SIDS (ABAS) ambayo kuathiriwa kwake na majanga yanayohusiana na hali ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, na mshtuko wa nje wa kiuchumi hufichua mara kwa mara udhaifu wa muundo ambao vipimo vya Pato la Taifa hushindwa kukidhi.”Kwa njia hiyo, “Vatican inazingatia kazi ya Kundi la Wataalamu wa Ngazi ya Juu kuhusu Zaidi ya Pato la Taifa na inatarajia mchakato wa serikali mbalimbali kuhusu vipimo vya maendeleo katika maendeleo endelevu vinavyokamilisha au kwenda zaidi ya Pato la Taifa.” Kwa kuhitimisha alisema “Kiti Kitakatifu kinatambua kwamba njia ya ustawi thabiti na wa kudumu kwa SIDS, ndani ya Ajenda ya 2030 na zaidi, iko katika nia ya jumuiya ya kimataifa ya kupitisha maendeleo ya binadamu yaliyojumuishwa kweli badala ya takwimu za kiuchumi tu.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.