“Obolo di San Pietro:”Upendo kwa Papa unafika kila siku katika kona za dunia
Vatican News
“Obolo di San Pietro:” hukusanyaji wa michango kwa Papa, ambayo inalenga kusaidia utume wake kwa Kanisa la ulimwengu na mipango mingi kwa wale wanaohitaji zaidi. Ripoti ya 2025 inaonesha mapato ya Mfuko wa “Obolo di San Pietro” ya Euro milioni 57.6, huku matumizi yakifikia Euro milioni 59.8. Tofauti hiyo inatokana na kushuka kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni. Mwaka 2025, michango ya jumla ya Euro milioni 54.5 ilitolewa, ambayo Euro milioni 41.2 ili kusaidia shughuli zinazofanywa na Kiti Kitakatifu katika huduma ya Utume wake Papa na Euro milioni 13.3 ili kusaidia mipango inayotoa msaada wa moja kwa moja kwa wale wanaohitaji zaidi.
Sehemu kubwa zaidi ya mapato hutoka katika majimbo katoliki duniani kite(63.6%), ikifuatiwa na wafadhili binafsi, mifuko ya vyama na taasisi za kidini. Hazina ya Sadaka hii inajumuisha michango inayopokelewa kupitia makusanyo yaliyokusanywa kutoka parokia ulimwenguni kote kwenye sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo. Hii hupitishwa Kiti Kitakatifu na majimbo kupitia Uwakilishi wa Kipapa katika Mabalozi wake, isipokuwa majimbo ya Italia, ambayo hutuma moja kwa moja. Michango mingine hufika kupitia uhamisho wa benki, hundi, au kupitia tovuti, kadi za mkopo, na PayPal. Hatimaye, kuna urithi unaoachwa kupitia wosia.(Ripoti kamili:https://www.obolodisanpietro.va/content/dam/obolodisanpietro/ad-2025/Rapporto-Annuale-2025-IT.pdf)
Picha nzima ya Ukarimu
Marekani (26.1% ya michango yote), Italia, na Brazil ndizo nchi zinazotoa mapato mengi zaidi, ikifuatiwa na Jamhuri ya Korea, Ujerumani, Ufaransa, na Hispania. “Obolo di San Pietro”au Sadaka ya Mtakatifu Petro iamsaidia Papa kutoa msaada wa vifaa kwa nchi zinazoendelea na idadi ya watu walioathiriwa na vita, lakini pia inaunga mkono, kwa njia mbalimbali, uwepo wa uinjilishaji wa parokia, majimbo, na taasisi za kitawa zinazohitaji hasa. Kimsingi, kuna maeneo matatu ya shughuli: upanuzi wa uwepo wa uinjilishaji; mipango ya kijamii; na usaidizi wa uwepo wa uinjilishaji, kwa jumla ya euro milioni 13.3.
Msaada kwa Ukraine
Mipango 252 ilifadhiliwa katika nchi 74, hasa barani Afrika, Asia, na Ulaya. Ufadhili wa masomo ulitolewa katika vyuo vikuu vya kipapa kwa mapadre, waseminari, na watawa kutoka Afrika, Amerika Kusini, na Asia. Msaada wa kibinadamu pia ulitolewa ili kusaidia idadi ya watu wa Ukraine.
Usaidizi wa uinjilishaji barani Afrika na Asia
Upanuzi wa uwepo wa uinjilishaji unajumuisha ujenzi wa makanisa mapya na majengo mengine, kwa lengo la kukuza na kuimarisha uwepo wa uinjilishaji katika Makanisa mapya ya eneo hilo. Nchini Sri Lanka, nyumba ya watawa ilijengwa Mannar; huko Misri, Kanisa la Parokia huko Hagaza; na huko Burkina Faso, kituo cha wachungaji huko Kaya.
Mipango ya kijamii, kuanzia Gaza hadi Haiti
Mipango ya kijamii inajumuisha programu za mafunzo na usaidizi, pamoja na usaidizi wa vifaa kusaidia jamii za wenyeji. Katika muktadha huu, misaada imetengwa kwa ajili ya Gaza, ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wasichana wa Dalit huko Ambikapur, India, na shule ya Sekondari huko Bentiu, Sudan Kusini. Mipango inayosaidia makanisa mahalia katika nchi za kimisionari na zile zinazohitaji uhitaji maalum ni pamoja, kwa mfano, ujenzi wa nyumba ya wageni kwa ajili ya mapadre huko Pathein, Myanmar; huko Haiti, ukarabati wa baraza la wazee la Kanisa la Mtakatifu Jerome huko Gonaïves; na Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino huko Kabwe, Zambia.
“Obolo di San Pietro” yaani Sadaka ya Mtakatifu Petro pia inasaidia shughuli za huduma zinazofanywa na Mabaraza ya Kipapa, taasisi, na mashirika ya Kiti Kitakatifu, zilizogawanywa katika maeneo matatu: usaidizi kwa ajili ya utume wa kitume wa Papa; huduma na utawala; na usimamizi wa mali. Matumizi ya jumla ya taasisi za Vatican katika kuunga mkono utume wa Papa (bila kujumuisha makato ya mapato yaliyopatikana na vyombo vyenyewe) yalifikia Euro milioni 404.5 milioni mwaka 2025, ambapo takriban Euro milioni 41.2 (10%) zinafunikwa na Sadaka Mtakatifu Petro Kati ya kiasi hiki, Euro milioni 148.7 hutumika kusaidia Makanisa mahalia katika mazingira magumu na maalum ya uinjilishaji.
Jambo muhimu la Kuzingatia tena ni kwamba:
“Ikumbukwe “Obolo di San Pietro” ni sadaka ambayo inaweza kuwa kidogo, lakini yennye ishara na thamani ya kina. Hii inaelezea upendo na imani kwa Baba Mtakatifu , kama mfuasi wa Petro. Link ya kutoa sadaka hiyo pekee hakuna nyingine tofauti na hiyo ambapo sadaka ya moja kwa moja zinazotumwa kupitia uhamisho wa benki na posta, hundi au kupitia tovuti:(https://www.obolodisanpietro.va/it/dona.html) na kadi za mkopo na PayPal; lakini vile vile hata urithi unaoachwa kupitia wosia ambapo mfadhili anaonesha hamu maalum ya kutenga mali, kiasi cha pesa au haki za urithi kwa Sadaka ya Petro au moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.