Tafuta

Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu Pio XI waliweka wakfu wa maaskofu wapya bila idhini ya Vatican. Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu Pio XI waliweka wakfu wa maaskofu wapya bila idhini ya Vatican.  (ANSA) Tahariri

Maumivu ya kugawanyika

Kitendo cha mgawanyiko na kutengwa kupitia latae sententiae:mgawanyiko mpya miongoni mwa Walefebvrian na maamuzi yaliyochukuliwa na Kiti Kitakatifu

Andrea Tornielli

Katika siku yenye uchungu ambapo amri hiyo ilitangazwa huku ikibainisha kutengwa moja kwa moja(kiotomatiki) kwa maaskofu wawili Lefebvrian de Galarreta na Fellay na maaskofu wanne wapya waliowekwa wakfu wakati wa kuwekwa mikono, baadhi walionesha kwa usahihi utata wa wazi wa Jumuiya ya Mapadre  ya Mtakatifu Pio X. Kwa maneno, katika matamko rasmi, wanadai kutambua uhalali na mamlaka ya Mrithi wa Petro, Papa Leo XIV, kumpenda na kumwombea. Kiuweli na ukweli daima huzungumza kwa sauti kubwa kuliko maneno, matamanio yake sahihi, miito yake  ya mara kwa mara, na ombi lake la kutoendelea na wakfu wa mgawanyiko bila idhini ya kipapa, au tuseme, na wakfu wa mgawanyiko uliopigwa marufuku waziwazi na Papa, ulipuuzwa kabisa. Katika siku za hivi karibuni, maneno ya Mtakatifu Pio Non verbo neque lingua (si kwa maneno au kwa ulimi,) sed opere et veritate (lakini kwa matendo na ukweli, mh.)… ili kuonesha upendo wetu kwa Papa ni muhimu kumtii. Kwa hiyo, unapompenda Papa, huna mijadala kuhusu kile anachoamuru au anachodai, au ni umbali gani wa utiifu unapaswa kufikiwa, na katika mambo gani mtu anapaswa kutii."


Kitendawili cha wanamapokeo wanaozingatia ibada hiyo kuwa haiwezi kuguswa lakini wanabuni kanuni ya kuchukua nafasi ya ukosefu wa kipengele muhimu katika kila daraja la uaskofu wa Kikatoliki: mamlaka ya Papa yametajwa.  Hata hivyo, suala halisi liko kwingineko. Na halina uhusiano wowote na  Misa katika ibada ya kabla Mtaguso (kwa matani iliitwa "Misa ya Kilatini"), kwa kuwa waamini walioshikamana na aina hiyo ya kiliturujia bado wanaruhusiwa kuisherehekea kwa ushirika kamili na Petro.

Kiini halisi ni kile ambacho ni Tamaduni na zaidi ya yote, ni nani anayepaswa kuilinda, kwa kufanya kukuza uelewa wetu wa Tamaduni  chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Ikiwa Tamaduni imeunganishwa katika mfumo wa kiitikadi, ikiwa mtu anajipatia haki ya kuhukumu Mtaguso uliongozwa na Mapapa wawili watakatifu na kuhudhuriwa na maaskofu elfu tatu kutoka ulimwenguni kote, ambalo lilitangaza hati zilizoidhinishwa kwa kauli moja; Ikiwa mtu anategemea kuwa Mrithi wa Petro na Kanisa Katoliki lote kukubali na kukumbatia mawazo ya kitaalimungu ya kundi fulani, kuna kitu kinachopingana sana. 


 

Na hasa zaidi ya yote, kuna kitu kilicho mbali sana na imani ya Kikatoliki, ambacho siri yake, kama mwandishi mkuu Vittorio Messori, aliyefariki Ijumaa Kuu iliyopita, na ambaye alikuwa amefanya kazi kwa bidii ili Jumuiya ya Mtakatifu Pio X irudi kwenye ushirika kamili, alielezea – ’et et”, non “l’aut aut,” yaani  “ni na inabaki kuwa "yote mawili” na," sio "yote/au."

Na kwa hivyo kuna nafasi katika Kanisa kwa waamini walioshikamana na liturujia ya kale; kuna nafasi katika Kanisa kwa ajili ya majadiliano, kwa ajili ya kusoma na kusoma tena hati na kuzitafsiri. Lakini si kumhukumu Papa na kutotii kwa kufanya vitendo vinavyovunja umoja wa "Mwili wa Fumbo" la Kristo, ambao ni Kanisa. Wala, hata hivyo, kuunda uongozi sambamba dhidi ya katazo la wazi kutoka kwa yule ambaye Yesu alimwambia: "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu."

Taariri kuhusu:Walefebvre

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

02 Julai 2026, 14:13