Mgawanyiko wa Lefebvre wajirudia baada ya miaka 38
Andrea Tornielli
Ni historia chungu, iliyofanywa ya kujaribu kwa ukarimu, na kuacha milango wazi, na fursa zilizotolewa. Ni historia chungu iliyotokana na michaniko mikubwa ambayo imepelekea Jumuiya ya Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X, iliyoanzishwa na Askofu Mkuu Marcel Lefebvre, kutengana na Papa na umoja wa Kanisa Katoliki la Roma, kutokana na kuwaweka wakfu wa kiaskofu bila idhini ya Papa. Ni Mchaniko huo ulitokea tarehe 1 Julai 2026 ambao una matokeo mazito ya moja kwa moja na si kwa maaskofu na mapadre walefebvrian tu, bali hata kwa waamini wote watakaoudhuria ibada, kwa sababu Mapadre wa Jumuyia ya Kipadre hutoa sakramenti bila uhalali, iwe sakramenti ya Kitubio na ndoa zitakuwa batili, kama inavyosomeka maelezo wazi ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.
Maamuzi ya Lefebvre
Wakati wa Mtaguso wa II wa Vatican, Askofu wa Kifaransa Marcel Lefebvre, licha ya kuwa katika sehemu ndogo ya baadhi ya mageuzi, alitia saini iwe katika Katiba kuhusu Liturujia, na iwe hata Tamko kuhusu uhuru wa kidini. Baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1970 Jumuiya ya Udugu wa Mtakatifu Pio X huko Écône, nchini Uswiss, Lefebvre alikataa kuadhimisha liturujia kulingana na Misale mpya ya Mtaguso wa II wa Vatican na kunako 1974 alieleza mageuzi ya Mtaguso kuwa kama“ mapya ya uharibifu wa Kanisa,” akithibitisha kwa andiko lake akikataa mapya ya Roma kama “usasa.” Jimbo lake liliondoa utambuzi wa Jumuiya ya Udugu, lakini Mtakatifu Paulo VI alitafuta namna kufanya mazungumzo, huku akiomba kufungwa kwa seminari. Baada ya kukataa mara kadhaa ushauri, Lefebvre alifungiwa huduma takatifu, lakini aliendelea hata hivyo kuadhimisha misa kwa umma. Kunako mwaka 1976 kwa kupokelewa huko Castelgandolfo, na kufanya mazungumzo na Papa hayakusaidia lolote. Papa Paulo VI alikabidhi Mfalsafa Jean Guitton uchungu wake alioufafanua kama “msalaba wa kweli wa kwanza,” wa upapa wake, licha ya kupenda kubadilisha na si kutenga ushirika wa kawaida.
Makubaliano ya Mafundisho yaliyosainiwa na Lefebvre
Kwa uchaguzi wa Papa Yohane Paulo II, Lefebvre alijionesha kwa kiasi kikubwa cha ufunguzi, kwa kutamka kunako 1980 kuwa hana shaka juu ya uhalali wa Papa Mpya. Kunako Aprili 1988, Kardinali Joseph Ratzinger aliongoza mchakato wa siku tatu na Askofu, kwa kufikia protokali ya Mafundisho ya pamoja, kusaini mnamo tarehe 5 Mei kuwa: Udugu wa Mtakatifu Pio X unaahidi uaminifu kwa Kanisa na kwa Papa, na ulikuwa unakubali Mafundisho ya Mtaguso na ulikuwa ukitambua uhalali wa Misa kwa mujibu wa ibada ya Papa Paulo VI na Yohane Paulo II. Na wakati huo jumuiya ikiwa inatarajia kuwaweka wakfu kwa Askofu wa Jumuiya ya Mapadre. Na ilikuwa kama vile suala hili limetatuliwa.
Tendo la kwanza la kujitenga
Kunako tarehe 6 Mei 1988 Lefebvre alitoa tamko tena kwa kutangaza nia ya kuwaweka wakfu maaskofu wapya bila idhini ya Papa, kwa kuogopa kuwa, Roma isingechagua wagombea kutoka ndani ya Jumuiya ya Udugu wa Mapadre. Licha ya mikutano ya kina na telegramu za Ratzinger aliyekuwa akiomba “kwa upendo wa Kristo na wa Kanisa lake,” wa kuacha kuwaweka wakfu, tarehe 30 Juni 1988 Lefebvre, na Askofu wa Brazil Antonio de Castro Mayer, aliwaweka wakfu maaskofu wapya: Fellay, de Galarreta, Williamson na Tissier de Mallerais. Tarehe 1 Julai, ikatolewa Amri(Decreto) ya kutengwa ya latae sententiae (kwa kilatini ikimaanisha “hukumo iliyotolewa) na sentiae kwa kilatini ikimaanisha hukumu inayopaswa, yaani njia ambazo ni za sheria ya Kanisa Katoliki) kwa tendo la kujitenga. Miaka iliyofuata Kiti kitakatifu kilijionesha kuwa tayari kutoa suluhisho la kisheria, wakati Walefebvrian waliendelea kulalamika juu ya kukosa “uwazi wa mafundisho” kwa kutaka kwamba Kanisa likatae kuwa sehemu ya Mtaguso II wa Vatican.
Hija ya 2000 na ruhusa ya Papa Benedikto
Kunako mwaka 2000 Walefebvrian walitimiza hija ya Jubilei jijini Roma na Askofu Fellay alipokelewa katika Mkutano na Papa Yohane Paulo II. Mawasiliano yalizidi kwa kina na Papa Benedikto XVI, ambaye kunako mwaka 2007 alitoa uhuru wa matumizi ya misale ya kabla ya Mtaguso kwa Barua yake ya Motu proprio Summorum Pontificum na tarehe 24 Januari 2009, alibatilisha kutengwa kwa Maaskofu wanne waliokuwa wamewekwa wakfu na Lefebvre. Uamuzi lakini ulikuwa umegubikwa na kusambaa kwa mahojiano ambayo mmoja wa maaskofu aliyekuwa amejirudi, Richard Williamson, alikuwa ameonesha nafasi ya kukataa kuhusu kuangamiza wayahudi, akiibua utata dhidi ya Papa, ambaye alikuwa akiwaomba Walefebvrian jitihada kuelekea ushirika kamili na Kanisa.
Utangulizi wa 2011 na msamaha wa Francisko
Kunako Septemba 2021, mwishoni mwa mazungumzo ya mafundisho, Kiti Kitakatifu na kwa Jumuiya ya Mapadre waliandika hati ndogo ambayo ilikuwa ikitaka mafundisho ya kipapa, bila kuzuia majadiliano ya kitaalimungu kuhusu Mtaguso. Fellay alibainisha kuwa Hati hiyo haikubaliki. Suluhishi zilizofuata za baadaye hazikusaidia hadi Walefebvrian walitamka kuwa hawatafuti kipaumbele cha kujulikana kisheria. Pamoja na Papa Francisko, katika Jubilei ya Huruma ya 2016, Mapadre wa Jumuiya ya Mtakatifu Pio X walikuwa wamepewa idhini maalum kwa ajili ya kuungamisha, iliyoongezwa, kama ishara ya ufunguzi wa kichungaji kuelekea waamini.
Mgawanyiko, kitubio na ndoa zisizo halali
Tarehe 2 Februari 2026 Jumuiya ya Mtakatifu Pio X ilitangaza kuwaweka wakfu Maaskofu wapya tarehe 1 Julai. Tarehe 12 Februari 2026 hata hivyo Mkuu wa Jumuiya ya Mapadre, Padre Davide Pagliarani alipokelewa mjini Roma na Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Mwenyekiti alipendekeza kwa Walefebvrian juu ya “njia ya mazungumzo hasa ya kitaalimungu, kwa njia ya usahihi” ili kuonesha ulazima mdogo kwa ajili ya ushirika kamili na Kanisa Katoliki na suhuhisho za kisheria: “Uwezekano wa kufanya hayo mazungumzo, yalihitaji kwamba Udugu uache maamuzi ya kuwaweka wakfu wa kiaskofu uliotangazwa.” Licha ya miito na mialiko ya mazungumzo, Walefebvrian waliendelea, wakitaka utengano mpya.
Katika kuhojiana na Waandishi wa Habari huko Castel Gandolfo Tarehe 16 Juni 2026, Papa Leo XIV alitoa maoni kuwa mgawanyiko kati ya wakristo daima ni uchungu, lakini kwa kuwa wao wanakataa mambo msingi ya Kanisa yanayohusiana na Mtaguso wa II wa Vatican “ na ikiwa wanafanya chaguo lile , ninasikitika, lakini sisi tunapaswa kwenda mbele.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.