Vatican:umaskini uliokithiri ni changamoto duniani na dharau ya binadamu
Vatican News
Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Matiafa huko New York Marekani alitoa hotuba yake katika mjadala wa Jukwaa la Kisiasa la Ngaza za Juu(HLPF)kwa 2026 kuhusu “Kuharakisha kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika nchi za Kiafrika, nchi zenye maendeleo duni (LDC), nchi zinazoendelea zisizo na bandari(LLDCs) na nchi zenye kipato cha kati (MIC)tarehe 8 Julai 2026. Katika hotuba yake alisema kuwa: “Tunapokaribia tarehe ya mwisho ya Ajenda ya 2030, ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa ichukue hatua kushughulikia changamoto zinazozuia maendeleo. Katika suala hilo, umaskini, hasa umaskini uliokithiri, ndiyo changamoto kubwa zaidi duniani. Uvumilivu wake katika nyanja zake nyingi unaendelea kuwanyima mamilioni na hasa wanawake na watoto, upatikanaji wa chakula cha kutosha, maji safi, huduma ya afya, elimu na kazi nzuri. Umaskini ni dharau kubwa kwa utu wa mwanadamu uliotolewa na Mungu.
Kushughulika vikwazo vya kimuundo vinavyozuia maendeleo endelevu
Maneno ya Papa Leo XIV ya "tusiache ulinzi wetu linapokuja suala la umaskini,"Mwakilishi wa Kudumu alibainisha kuwa “ni wito wa kuweka kipaumbele katika kutokomeza umaskini, ambaPo ni sharti muhimu kwa maendeleo endelevu.” Katika suala hilo, aliongeza, “usaidizi mpya na ulioimarishwa kwa nchi za Afrika, zenye maendeleo duni( LDC),zisizo na bandari(LLDC) na zenye kipato cha kati(MIC) ni muhimu. Usaidizi kama huo lazima uendelee zaidi ya hatua za muda mfupi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo vinavyozuia maendeleo endelevu.”
Kukuza mfumo wa biashara wenye usawa
Vatican inabainisha kwamba “Hii ni pamoja na kuimarisha upatikanaji wa ufadhili wa masharti nafuu, kukuza mifumo ya biashara yenye usawa, kuwezesha uhamishaji wa teknolojia, na kuendeleza unafuu wa deni wenye maana.” Ili kuharakisha maendeleo, ni muhimu pia kuzingatia udhaifu wa kipekee unaokabiliwa na nchi hizi. Vikwazo vya umbali kijiografia, mabadiliko ya tabianchi na miundombinu midogo vinazidisha ukosefu wa usawa kwa wengi.”
Jukumu muhimu la familia kama umoja wa msingi wa jamii
Hatimaye “Vatican pia inataka kusisitiza jukumu muhimu la familia kama umoja wa msingi wa jamii, "faida kuu ya kijamii," na chanzo muhimu cha ustahimilivu. Sera zinazoimarisha familia huchangia moja kwa moja katika kuondoa umaskini, utulivu wa kijamii na maendeleo fungamani ya Binadamu.” Kwa njia hiyo, “Kuwekeza na kukuza sera hizo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ni muhimu kwa kuhakikisha ustawi wa watu wote, kuondoa umaskini na kufikia maendeleo endelevu ya binadamu.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.