Tafuta

UNICEF inabainisha kuwa elimu iwe kwa wote kike na kiume chini Afghanistan. UNICEF inabainisha kuwa elimu iwe kwa wote kike na kiume chini Afghanistan. 

Mkurugenzi wa UNICEF:watoto wa kike wasiachwe nyuma nchini Afghanistan

UNICEF inakaribishwa kwa shangwe juu ya ufunguzi wa shule za sekondari nchini Afghanistan,ikisisitiza kuwa wasichana hawapaswi kuachwa nyumba bila kwenda shule.Kuna haja ya kuwafudisha wanawake ili waweze kuanza mafunzo yao.Hata kabla ya mgogoro wa hivi karibuni wa kibinadamu,watoto milioni 4,2 hawakuwa shuleni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Bi Henrietta Fore amesema, shirika la UNICEF linakaribisha kwa shangwe juu ya  habari ambayo shule za sekondari nchini Afghanistan zimeanza kufunguliwa, Ijumaa tarehe 17 Septemba 202, mara baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya janga la UVIKO-19  lakini pamoja ana hayo waheshimu wengine kama wasichana wasiachwe bila kupata fursa hiyo ya wakati huu. “Wasichna hawawezi na wala hawapaswi kuachwa nyumba. Ni muhimu kwamba wasichana wote pamoja na wakubwa wewe na uwezo wa kuanza tena mafunzo bila kuwachelewesha”. Kwa maana hiyo UNICEF imesisitiza kuwa “kuna haja ya kuwafudisha wanawake ili waweze kuanza mafunzo yao. Hata kabla ya mgogoro wa hivi karibuni wa kibinadamu, watoto milioni 4,2 hawakuwa wamejiandikisha shuleni. Karibia asilimia 60 ya wao ni watoto wa kike. Kila siku ambayo wasichana wanapoteza mafunzo ni fursa inayopotea kwao, familia zao na jumuiya zao”, amesisitiza Bi Fore.

Hata hivyo kuumekuwapo na maendeleo yenye maana katika mafunzo katika nchi hiyo kwa miongo miwili ya mwisho. Idadi ya shule ziliongezeka mara mbili. Idadi ya watoto shuleni iliongezea kutoka milioni moja hadi milioni 9,5 ya watoto. Ubora huu ni muhimu sana kwa watoto wa nchi hiyo ambao lazima walindwe, waheshimiwe na kutunzwa. Kwa mujibu wa UNICEF,  tena wanatoa ushauri kwa wadau wa maendeleo ili kusaidia mafunzo kwa watoto wote nchini Afghanistan. Pamoja na hayo yote, UNICEF itaendelea kusaidia kwa kuungwa mkono na wadau wengine ili wasichana wote na vijana wa kiume wawe na uwezekano kweli wa kujifunza na kuendeleza vipaji vyao ambavyo lazima kuwa na matarajio na ujenzi wa nchi ya Afghanistan ya amani na uzalishaji ya wakati ujao.

VIDEO/PICHA:   https://weshare.unicef.org/Package/2AMZIFH9OCSK

Ili kusaidia watoto wa Afghanistan:https://unicef.it/afghanistan

18 September 2021, 17:04