Tafuta

2023.06.06 Makaburi ya wahanga wa vita huko Boordyanka nchini Ukrane (Vita vilizuka tangu 24 Februari 2022 vimeua mamia na maelfu ya watu huko Ukraine). 2023.06.06 Makaburi ya wahanga wa vita huko Boordyanka nchini Ukrane (Vita vilizuka tangu 24 Februari 2022 vimeua mamia na maelfu ya watu huko Ukraine). 

Miaka miwili ya vita Ukraine na jinsi gani Ulaya ilikaribisha wakimbizi

Kuna mipango mingi ya mshikamano ambayo imetekelezwa tangu mapigano yalipozuka.Mashirika ya kidini,mashirika yasiyo ya kiserikali na raia mmoja mmoja wameleta msaada wao katika Ulaya Magharibi na pia kwa nchi zinazopakana na Ukraine.Miezi 24 baada ya kuanza kwa vita,watu milioni sita bado wako nje ya makazi yao.Mvutano wa Transnistria huko Moldova.

Alessandro Guarasci na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni miaka miwili ya vita nchini Ukraine  ambayo imefanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi siku baada ya siku. Hali ya kibinadamu imeungwa mkono  bila kusitia na  shirika zima la kimataifa la Caritas Internationalis na shukrani kwa zaidi ya wafanyakazi na watu wa kujitolea zaidi ya 2,600 ambao hawakukosa kujitoa. Caritas Ukraine na Caritas Spes Ukraine zimetoa msaada wa kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni 3.8 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Hali, ile ya mzozo, ambayo ilishuhudia mamia ya Mashirika yasiyo ya kiselikali (NGOs)kuchukua hatua na kuchochea mshikamano wa kimataifa. Sasa itakuwa muhimu kuelewa ikiwa ombi linalotarajiwa la Transnistria la kushikiliwa na Urussi litasababisha ongezeko zaidi la mvutano katika eneo hilo.

Wakimbizi milioni sita

Hivi sasa, kulingana na takwimu za  Caritas, 40% ya idadi ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu na zaidi ya milioni 6 Ukraine ni wakimbizi. Katika mashariki na kusini, ikiwa ni pamoja na maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa muda wa Shirikisho la Urussi, mamilioni ya watu ambao hawana maji ya kutosha, chakula, huduma za afya, malazi, ulinzi na huduma na vifaa vingine muhimu.

Huko Roma, Mtakatifu  Sofia ndio kitovu cha ukarimu

Jijini  Roma injini halisi ya usaidizi iko katika kitovu cha Basilika ya Mtakatifu Sophia. Kutoka hapa, lori za misaada huondoka mara kwa mara kuelekea maeneo yaliyoathiriwa na vita nchini Ukraine. Padre  Marco Sehmen, rais wa chama cha kidini cha Mtakatifu Sofia cha Wakatoliki wa Ukraine , na mkuu wa Basilika alisema kwamba “siku hizi ni za kutafakari, za maombi kwa ajili ya kile kilichotokea miaka miwili iliyopita. Kanisa litakuwa wazi kuliko kawaida, kwa sababu ni wakati wa kukusanyika hata karibu zaidi. Hata hivyo, tunahisi msaada mkubwa, hasa kutoka kwa Baba Mtakatifu kupitia kwa Kardinali Krajewski ambaye siku chache zilizopita malori ya  chakula ambacho kilikuwa kimehifadhiwa hapa, Hagia Sophia yamekwenda. Lakini pia kuna Baraza la Maaskofu wa Italia, Mfuko wa  Wahamiaji, Benki ya Madawa na watu wengi binafsi.”

Huko Roma, Mtakatifu Sofia ndio kitovu cha ukarimu

Huko Roma injini halisi ya usaidizi ni Hagia Sophia. Kutoka hapa, lori za misaada huondoka mara kwa mara kuelekea maeneo yaliyoathiriwa na vita nchini Ukraine. Padre Marco Sehmen, rais wa chama cha kidini cha Mtakatifu Sofia cha Wakatoliki wa Ukraine, na mkuu wa Basilika alisema kwamba “siku hizi ni za kutafakari, za maombi kwa ajili ya kile kilichotokea miaka miwili iliyopita. Kanisa litakuwa wazi kuliko kawaida, kwa sababu ni wakati wa kukusanyika hata karibu zaidi. Hata hivyo, tunahisi msaada mkubwa, hasa kutoka kwa Baba Mtakatifu kupitia kwa Kardinali Krajewski ambaye siku chache zilizopita alianzisha malori ya chakula ambayo yalikuwa yamehifadhiwa hapa, Hagia Sophia. Lakini basi kuna Baraza la Maaskofu wa Italia, Wakfu wa Wahamiaji, Benki ya Madawa na watu wengi binafsi.”

Katika Moldova, wakimbizi 116 elfu 

Hata Moldovia ndogo, ingawa ni Nchi maskini zaidi barani Ulaya, imesaidia kwa njia muhimu, hasa wakati katika miaka hii miwili mikoa ya kusini mwa Ukraine imekumbwa na mapigano. Marco Buono, Mkuu wa ujumbe wa Intersos huko Moldovia, alisema kwamba leo hii kuna wakimbizi elfu 116 nchini humo. Kwa uwiano wa wakazi pengine ni Nchi  ambayo ina mwenyeji zaidi. “Kwa mwaka sasa, tumekuwa na sheria maalum hapa inayoitwa ulinzi, ambapo mkimbizi anayeomba kupata ulinzi huu anatambuliwa na anaweza kupata huduma kivitendo kama raia wa Moldovia” - alisema Buono - Hii pia inatumika zaidi ya yote kwa afya na elimu, huduma mbili muhimu zaidi. Ni lazima izingatiwe kwamba nusu ya watu wanaokuja kutoka Ukraine hapa ni watoto. Kwa hivyo mahitaji hayajatoweka, yapo kila wakati na sisi, kama shirika la kibinadamu, tunajaribu kuyashughulikia pamoja na mashirika mengine yanayofanya kazi nasi.”

Mvutano, kati ya mambo mengine, kuna hatari ya kuongezeka baada ya habari kwamba Congress of Transnistria, eneo linalojitangaza lenye uhuru kutoka Moldova, litapiga kura ya kuungana na Urussi mnamo tarehe 28 Februari 2024. “Mabadiliko yoyote katika hali ilivyo sasa yatakuwa ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa,” alisema Peter Stano, msemaji wa Huduma ya Nje ya Umoja wa Ulaya(UE).

Huko Romania, Wakapuchini husafiri na kurudi na Ukraine

Takriban wakimbizi elfu 900 wa Kiukreni wako katika nchi jirani ya Romania. Padre Eugene Giurgica ayesimamia kituo cha mapokezi cha Wakapuchini huko Sighetu, kaskazini mwa Romania alisema mpaka na Ukraine hupita mita mia chache kutoka katikati na watu wengi wamefika huko kila siku katika miaka hii miwili. Sasa ni familia moja tu iliyobaki huko, lakini mahitaji hayajabadilika. “Hali ambayo tumekuwa tukifanya katika miezi ya hivi karibuni ni kusaidia jamii za wakimbizi ambazo ziko karibu na mpaka, na kwa hivyo, kulingana na michango tunayopokea, tunajaribu kusaidia watu hawa katika maisha yao ya kila siku nchini Ukraine, lakini kulazimishwa kuondoka nyumbani, bila kazi” alisema Padre Giurgica. Kuna aina nyingi za usaidizi, pia unafanywa na raia wa kawaida. Bila shaka, tunaanza kuona uchovu kidogo miongoni mwa wakazi wa Romania, miaka miwili baada ya kuzuka kwa vita.

24 February 2024, 10:55