Tafuta

HALI YA MJI MKUU WA HAITI NI MBAYA SANA. HALI YA MJI MKUU WA HAITI NI MBAYA SANA.  (ANSA)

Haiti:Ni hali ya kutisha na hospitali za Kikatoliki pia zilishambuliwa!

Marcella Catozza,mtawa wa Kifransiskani,ambaye amekuwa akijihusisha na shughuli za kichungaji na upendo nchini Haiti kwa miaka mingi,akizungunza Fides amesema:“Hali inatisha.Magenge yalivamia viwanja vyote vya ndege vya nchi hiyo na kumkamata Waziri Mkuu Ariel Henry ambaye alikuwa akitoka Nairobi aliko tia saini makubaliano ya kutumwa kikosi cha jeshi cha Kenya nchini Haiti.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hali inatisha Nchini Haiti na Magenge yalivamia viwanja vyote vya ndege vya nchi hiyo na kumkamata Waziri Mkuu Ariel Henry ambaye alikuwa akirejea kutoka Nairobi ambako alitia saini makubaliano ya kutumwa kwa kikosi cha kijeshi cha Kenya nchini Haiti. Magenge hayo yalishambulia majengo kadhaa ya umma, yakiwemo magereza na majengo ya kibinafsi yakiwemo hospitali ya Kikatoliki ya Mtakatifu Francis wa Sales huko Port-na-Prince. Na Ariel Henry bado hajaweza kurejea nchini kwa sababu hakuna masharti ya usalama. Hayo yalisema na Marcella Catozza, mtawa wa Kifransiskani, ambaye amekuwa akijihusisha na shughuli za kichungaji na upendo nchini Haiti kwa miaka mingi, akizungunza na shirika la habari za kimisionari la Fides.

Magenge yaliyokuwa yakiuana wao kwa wao yameungana kushambulia

Kwa mujibu wa shirika la kimisionari la habari: “Ukweli ambao lazima utiliwe mkazo ni kwamba magenge haya ambayo hadi Alhamisi iliyopita yalikuwa yakiuana, siku ya Ijumaa 1 Machi 2024 waliungana kushambulia taasisi,” alisema Sista Marcella. Na Jimmy Chérizier, mkuu wa kundi la G9, anayejulikana kama “Barbeque” ndiye  ambaye alizindua wito wa umoja wa magenge” akikumbusha mtawa huyo. Lakini sidhani kama “Barbecue” ndio ubongo wa sababu ya haya yote. Kuna mawazo ya kisiasa, labda yale ambayo yalikubali mauaji ya Rais Jovenel Moïse mnamo 2021,” alisema Sr  Marcella. “Kumbuka kwamba magenge haya yana silaha na magari ya hali ya juu, si mapanga tu; hata wana ndege zisizo na rubani za kutambua mienendo ya polisi na wanajeshi wanaoonekana kutokuwa na uwezo wa kuwazuia.”

Nani anaweza kuwa na nia ya kudhoofisha Haiti?

“Tunaweza kutoa dhana tu kwa sasa. Kwa muda sasa, uwepo wa angalau wauzaji wa aina 5 wa madawa ya kulevya kutoka Mexico umerekodiwa nchini. Hawa wanaweza kutaka kuifanya Haiti kuwa nchi isiyo na mtu ili kuweza kudhibiti vyema ulanguzi wao wa madawa ya kulevya hadi Amerika Kaskazini na Ulaya. Kwa kuwa katikati mwa Carribien, Haiti ni mahali pazuri kama kipitishio cha madawa yanayotoka nchini Colombia na Mexico na kuelekea kwenye masoko tajiri ya Magharibi. Hatimaye, lakini ni uvumi tu ambao nimesikia karibu, kuna mazungumzo ya uwezekano wa kuhusika kwa Rais wa zamani Aristide, ambaye alirejea Haiti mnamo mwaka 2010. Lakini ninarudia kusema, ni uvumi tu,” alihitimisha mtawa huyo.

06 March 2024, 12:31