Tafuta

Siku ya Wanawake duniani 2024 . Siku ya Wanawake duniani 2024 .  (ANSA)

Siku ya Wanawake Duniani:Wekeza kwa wanawake.Harakisha maendeleo!

Katika Siku ya wanawake Duniani 2024,UN Women inabainsha:Ulimwenguni bado unakabiliwa na migogoro ya umaskini,ukosefu wa usawa na sehemu kubwa inawakumba wanawake.“Mazingira ya unyanyasaji wa kazi na unyanyasaji wa kijinsia wa watoto katika majukwaa ya burudani pia wamevuka mipaka."amesema hayo Mtaalamu wa UN kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto.

Na Angella Rwezaula  Vatican.

Tuko katika Juma la maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambapo kwa  mwaka 2024, maadhimisho  haya yanaongozwa na kauli mbiu: “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo.” Ndugu msomaji wa Vatican News lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi. Wanawake kote ulimwenguni ni waathirika wakubwa wa changamoto hizi na hivyo kuongeza changamoto zinazozikabili jamii zao, hususani watoto na vijana. Changamoto hizi zinaweza tu kutatuliwa kwa kubuni suluhu zinazowawezesha wanawake.

Huyu ni mwanamke na Rais wa Bank ya Ulaya ya Kati (ECB) Bi Christine Legarde.
Huyu ni mwanamke na Rais wa Bank ya Ulaya ya Kati (ECB) Bi Christine Legarde.

Kwa kuwekeza kwa wanawake, tunaweza kuibua mabadiliko na kuharakisha mpito kuelekea dunia yenye afya, usalama na usawa zaidi kwa wote. Na zaidi kwa kuwekeza wanawake hata wenyewe wanawaza kuwa na kilimo endelevu, lishe bora, na stadi za biashara ndogo ndogo ili wawe na maarifa na ujuzi unaohitajika kuwaoatia familia zao lishe bora mwaka mzima na kuuza masalio ili kusaidia kulipia mahitaji mengine ya nyumba hata kuwasomesha watoto wao.  Watoto wengi katika familia maskini utakuta wanaingia hata katika  Biashara na unyanyasaji wa kingono na  ambayo inapaswa ujulishwe kuwa ipoa na vyombo vya habari vieleze uharisa. Ni katika muktadha huo ambapo tarehe 5 Machi 2024 jijini Geneva Uswisi katika mkutano wa 55 wa Baraza La Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto, Bi Fatima Singhateh alitaka zitambulike kwa hatua za mtu mmoja mmoja au za pamoja za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika tasnia ya burudani na vyombo vya habari ili kukomeshwa unyanyasiji huo mara moja.

Wanawake wanaanza kununua maua
Wanawake wanaanza kununua maua

Katika ripoti yake  Bi Singhateh alisema ushahidi unaotolewa na waathirika mashujaa na manusura mara zote umesisitiza hitaji la dharura la kuboreshwa kwa ulinzi wa watoto na vijana katika sekta hiyo, na kuibua maswali muhimu kuhusu kutotosheleza kwa hatua zilizopo za kuzuia na ulinzi, mifumo ya uwajibikaji na upatikanaji wa haki. “Idadi kubwa ya kesi za unyanyasaji haziripotiwi, haswa kutokana na mienendo ya nguvu iliyopo, kanuni hatari za kijinsia, hofu ya kulipiza kisasi na kupoteza nafasi za kazi. Mambo haya mara nyingi hujenga mazingira ambayo watu binafsi katika nafasi za mamlaka huwanyanyasa watoto walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na wale wanaotarajiwa kuwa waigizaji.”

Wanaotarajia kuwa waigizaji na waigizaji

Mtaalamu huyo pia alieleza kugundua kuwa tabia ya unyanyasaji ya kingono, ikiwa ni pamoja na wale wanaoanza kuwafundisha watoto wangali wadogo, ilikubaliwa kama kawaida katika tasnia ya burudani, kwani wahalifu mara nyingi hawakabiliwi na madhara yoyote kwa kutumia mamlaka kinyume cha sheria dhidi ya vijana na wanaotarajia kuwa waigizaji.

Wanawake wakewezeshwa wanaweza kwenye uzalishaji na biashara ndogo ndogo
Wanawake wakewezeshwa wanaweza kwenye uzalishaji na biashara ndogo ndogo

“Mazingira ya unyanyasaji wa kazi na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika majukwaa mbalimbali ya burudani hayaelekei tu kuvuka mipaka, lakini pia yanalenga na kuwatumia watoto. Waathiriwa na manusura wamekutana na ukimya, kosefu wa uchunguzi, vitisho au kutokuwepo kwa kuchukuliwa hatua.” Mtaalamu huyo akiwasilisha ripoti yake alitoa wito wa kuwepo kwa njia za kupunguza hatari na kuhakikisha kuwa uhusika wa watoto katika tasnia ya burudani, na mienendo ya watu binafsi au biashara ndani ya sekta hiyo, unaendana na sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Siku ya wanawake duniani kuwekeza kwao
07 March 2024, 14:23