Tafuta

Inakadiriwa kuwa watu milioni 575 wanaweza kuwa bado wanaishi katika umaskini uliokithiri kufikia mwaka 2030.Hivi sasa,asilimia 10.3 ya wanawake wanaishi katika umaskini uliokithiri.Wanahitaji kuungwa mkono ili waweze kujikwamua. Inakadiriwa kuwa watu milioni 575 wanaweza kuwa bado wanaishi katika umaskini uliokithiri kufikia mwaka 2030.Hivi sasa,asilimia 10.3 ya wanawake wanaishi katika umaskini uliokithiri.Wanahitaji kuungwa mkono ili waweze kujikwamua. 

Wawakilishi wa Elimu kutoka Tanzania wapeleka sauti za wasichana&wanawake zisikike katika CSW68!

Washiriki kutoka Tanzania,katika Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani(CSW68)kuanzia 11-22 Machi 2024 ni vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala,waliozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu kufikisha sauti ya wasichana na wanawake vijana zisikika kwenye majukwaa makubwa kama CSW68.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Ripoti iliyotolewa mwanzoni mwa Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ilielezea migogoro inayokatiza na ya ufadhili na mipango ya kitaasisi inayotakiwa kuelekea utekelezaji kamili, wenye ufanisi na wa kasi wa Beijing wa Tamko na Jukwaa la Utekelezaji na utekelezaji wa kijinsia wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu(azimio la Mkutano Mkuu 70/1). Na katika Ripoti hiyo ilihitimisha kwa mapendekezo ya kuzingatiwa na Tume ya Hadhi ya Wanawake. Katika kipengele cha III kinachohusu: “Umaskini wa wanawake na wasichana,” kinabainisha kwamba maendeleo kuelekea kumaliza umaskini yanapaswa kuwa mara 26 kwa kasi zaidi ili kufikia Lengo namba 1 ifikapo mwaka 2030. Inakadiriwa kuwa watu milioni 575 wanaweza kuwa bado wanaishi katika umaskini uliokithiri kufikia mwaka 2030. Hivi sasa, asilimia 10.3 ya wanawake wanaishi katika umaskini uliokithiri. Kama mwelekeo wa sasa utaendelea, inakadiriwa asilimia 8 ya wanawake duniani kote (milioni 342) bado watakuwa wanaishi chini ya dola 2.15 kwa siku mwaka 2030, na wengi wao ni  katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Wanawake na wasichana wanaoishi katika umaskini wanakumbana na kunyimwa mara kwa mara na kuzidisha, ikiwa ni pamoja na kunyimwa kiwango bora cha maisha, usalama wa chakula, lishe na makazi ya kutosha. Kunyimwa huko kunaongezwa na mwelekeo mwingine wa kutofautiana, ikiwa ni pamoja na rangi, kabila, ulemavu, eneo, hali ya ndoa na uhamiaji, hali ya VVU, mwelekeo wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia. Wanawake na wasichana wanaokumbana na aina nyingi, zinazoingiliana za ubaguzi huwa na hali mbaya zaidi katika nyanja zote za ustawi. Kwa njia hiyo katika muktadha wa mkutano huo wa Tume ya 68 ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa katikati  tareha 15 Machi 2024, Idhaa Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ilizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Na akizungumza na baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala, walikuwa ni: Zahra Salehe Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa ICCAO ambaye alieleza ujumbe mkubwa waliokuja nao kwamba: “Tumeletwa hapa kwa ajenda moja ya elimu na ujumbe mkubwa tuliokuja nao ni wa kuhakikisha sauti za wasichana na wanawake vijana zinasikika kwenye majukwaa makubwa kama haya CSW68 na sisi ajenda kubwa ambayo tunaiona kwa sasa ni ‘reentry’ ambayo ni ruhusa ya msichana kurudi shule baada kupitia changamoto kubwa. Tusimuache mtu nyuma kwa sababu ya sababu mbalimbali ambazo zote zimeletwa na kutokuwa na usawa wa kijinsia. Wanaendelea na wanaendelea kutimiza ndoto zao.”

Paulina Ngurumwa kutoka taasisi ya KINNAPA hata hivyo alikubaliana na alichosema kinara wa elimu mwenzake na kwamba wao wanapambana na vikwazo dhidi ya elimu ya wanawake ingawa bado kuna ugumu. Kwa mujibu wake alisema: “Hatuna mabweni, hatuna mahali pa kuwaweka kwa hiyo tunajikuta kuna mzigo mwingi. Kwa hiyo wito wetu wadau kwa ngazi ya ulimwengu, kwa ngazi ya mataifa, kwa ngazi ya taifa letu la Tanzania tushikamane tuone ni namna gani tunaweza kutafuta hata namna gani tuwapatie hawa watoto mabweni ambayo wanaweza wakasomea na wakakaa pale wakawa katika mazingira salama ili waeze kutimiza ndoto zao.”

Hata hivyo kutokana na changamoto kama hizo Nasra Kibukila kutoka shirika la TEN/MeT alihamasisha juu ya  Bajeti ya nchi inayozingatia jinsia na kusema kuwa “Kwa sasa hivi Tanzania tumeshaanza mchakato wa kutengeneza bajeti ya mwaka 2024-2025 na kwas asa hivi iko kwenye ngazi ya wabunge. Tutakapotoka hapa, tutakayojifunza hapa tukirudi nyumbani tunaenda kuwa na mkutano pamoja na wabunge kuweza kuwaelezea yapi tumejifunza kwa jinsi gani kuwa na majeti yenye mrengo wa kijinsia na wao waweze kutusaidia kuhakikisha kuwa pale tutapakuwa na bajeti ya 2024-25inakuwa iko kwenye mrengo wa kijinsia kuweza kuhakikisha kuwa makundi yote maalumu yanakuwa yana bajeti yao kuwawezesha.”

Tunatamani  sheria ya elimu Tanzania itambue wasichana kuendelea na masomo baada ya ujauzito. Kwa upande wa Nasra Kibukila akiwakilisha Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) katika Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, jijini New York, Marekani alizungumza pia na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kueleza ni yapi wanatekeleza nchini Tanzania ili kuhakikisha elimu bora hususani kwa wasichana. Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MeT) ni moja ya mashirika ambayo kupitia ushirikianno na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na kwa ufadhili wa Malala Fund na wadau wengine yanayohamasisha Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu kuhusu Elimu Bora na lengo namba 5 linalohimiza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kwani yanaweza kufanikisha kufikiwa kwa malengo mengine ya maendeleo endelevu kama vile afya bora na ustawi na kutotomeza umaskini.

Mahojiano na Nasra Kibukila wa TEN/MET

Je hili Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET linafanya shughuli zipi?

TEN/MET ni mtandao wa kitaifa 184 za elimu zinazofanya kazi katika sekta ya elimu Tanzania Bara. TEN/MET inatazamia mfumo wa elimu wa kitaifa ambapo kila mtoto wa Kitanzania apate fursa ya kushiriki katika elimu bora. Dira hii inaboreshwa kupitia dhamira yake ya kuratibu na kuimarisha asasi za kiraia za elimu nchini Tanzania kupitia mitandao, kujenga uwezo, utafiti na utetezi. Shughuli za TEN/MET huongozwa na mpango mkakati unaoongozwa na kutengenezwa na malengo matano ya kimkakati ambayo ni: Kuratibu elimu Asasi za Kiraia (AZAKI) huathiri maamuzi katika mfumo wa elimu nchini Tanzania.

2. Kuimarisha mifumo na miundo ya TEN/MET ili kutekeleza majukumu yake.

3. Kuzalisha mbinu bora zinazozingatia ushahidi ndani ya nchi, kikanda na kimataifa ili kuleta matokeo ya sera na mazoea ya elimu.

4. Kutetea ujumuishaji wa jinsia katika mfumo wa elimu ili kupata elimu yenye usawa, shirikishi na bora kwa wanafunzi nchini Tanzania.

5. Kutetea mfumo wa elimu unaokumbatia sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kukidhi matakwa ya mapinduzi ya nne ya viwanda.

Maono

Mfumo wa elimu wa kitaifa ambapo wanafunzi wote wanapata fursa ya kupata elimu jumuishi, yenye usawa na bora.

Utume

Kushawishi na kufahamisha sera na mazoea yanayokuza upatikanaji wa elimu jumuishi, yenye usawa na bora nchini Tanzania.

Ndugu Msomaji / Msikilizajaji hata  hivyo shirika hili kila mara linaziti kutoa wito kwa  jamii nzima kukabili na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto nchini. Kila Mtanzania, mzazi/mlezi, mwalimu na jamii nzima kwa ujumla wetu tunawajibu wa kukemea vitendo na viashiria vya  ukatili dhidi ya  watoto katika eneo na mazingira mahalia. Bila kujali nafasi zetu, jamii nzima tunao  wajibu wa kuchukua hatua sitahiki inapotokea vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto vinafanywa mbele yetu au tupatapotaarifa sahihi zinazohusu ukatili dhidi ya mtoto.

Tunaukumbusha umma wa watanzania kuwa, vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ni jambo changamano, kwani hufanyika katika muktadha na nyanja nyingi katika kila nchi duniani kwa dhana ya kuwarekebisha kimaadili. Njia na dhana hii ni potofu kwani mtoto hawezi kurekebishwa na  kujengwa katika maadili mema kwa njia ya ukatili badala yake ukatili huu umwathiri zaidi kisaikolojia na kuharibu jitihada za kufikia malengo yake.

Kwa hivyo, vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto si jambo la kuvumilika  na linahitaji juhudi madhubuti na za makusudi katika kuvikabili na kuvitokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto hapa nchini na duniani kote kwa ujumla.  Ili kufanikisha adhima hii, tunatoa wito kwa serikali yetu sikivu, jamii ya watanzania na wadau wote  kushirikiana katika kushughulikia matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambayo yanaendelea kushamiri kwa kasi kubwa hapa nchini na duniani kote kama tunavyoshuhudia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Aidha, tunatoa wito kwa serikali yetu sikivu, kwa kushirikiana na wadau, ifanye mapitio upya  ya sheria na miongozo ya haki na ulinzi wa mtoto ili kuondoa mianya yote inayoweza kutumiwa vibaya na watu waliopewa dhamani ya kuwalea, kuwafundisha na kuwaongoza watoto.

Mahojiano ya vinara wa Elimu Tanzania katika CSW68, huko New York Marekani
20 March 2024, 11:39