Tafuta

Shambulio katika mlipuko wa angani uliolenga kituo cha kutoa msaada cha matibabu cha MSF huko Old Fangak Shambulio katika mlipuko wa angani uliolenga kituo cha kutoa msaada cha matibabu cha MSF huko Old Fangak 

Umoja wa Afrika walaani shambulizi dhidi ya hospitali ya MSF nchini Sudan Kusini

Uvamizi wa kituo cha Old Fangak,kaskazini mwa nchi hiyo changa ya Kiafrika,ulisababisha vifo vya watu 7 na wengine 20 kujeruhiwa,akiwemo mgonjwa wa kituo hicho na wafanyikazi 2 wa afya.Ghasia hizo ni sehemu ya mapigano yaliyozuka mapema mwezi Machi kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa kile kinachoitwa Jeshi la Wazungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Umoja wa Afrika (UA)umelaani shambulio lililofanywa Jumamosi tarehe 3 Mei 2025 dhidi ya Old Fangak, kaskazini mwa Sudan Kusini, lililolenga hospitali ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), baadhi ya maeneo ya jiji hilo na soko la ndani, na kusababisha vifo vya watu 7 na wengine 20 kujeruhiwa, akiwemo mgonjwa wa kituo hicho na wahudumu 2 wa afya. Kwa mijibu wa dokezo rais wa Tume ya jumuiya ya Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, alibainisha" hii ilikuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu." Helikopta mbili zililipua hospitali hiyo, na kusababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na uharibifu kamili wa duka la dawa, alisema Mamman Mustapha, mkuu wa ujumbe wa MSF nchini Sudan Kusini, akielezea kuwa vifaa vya matibabu vyote" vilihifadhiwa huko, hasara ambayo inahatarisha uwezo wa kutoa huduma kwa wale wanaohitaji.

Hospitali pekee ya Fangak

"Hospitali ya Old Fangak ndiyo pekee katika Kaunti ya Fangak na inahudumia idadi ya zaidi ya watu 110,000, ambao tayari walikuwa na uwezo mdogo wa kupata huduma za afya," aliongeza mwakilishi wa MSF, akisikitishwa na tukio hilo na kutoa wito kwa "wahusika wote kwenye mzozo kulinda raia na miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na wafanyikazi wa afya, wagonjwa na vituo vya afya," ambayo pia yalilengwa katika mapigano ya hivi karibuni: katikati mwa Aprili, Hospitali nyingine ya MSF ililengwa. Shambulio la hivi punde ni sehemu ya ghasia zilizozuka mwanzoni mwa mwezi Machi kaskazini mwa nchi hiyo changa ya Afrika, iliyojitawala tangu mwaka 2011, kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa kile kinachoitwa Jeshi la Wazungu.

Helikopta zisizo na rubani zilitumika

Hali hiyo imezorota kutokana na mapigano kati ya vikosi vya Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, waliokamatwa mwishoni mwa Machi, ambayo yamezusha hofu ya kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2018, na vifo vya karibu 400,000. Kwa hakika, washirika wa Salva Kiir wanashutumu wafuasi wa Riek Machar kwa kuchochea machafuko katika ligi na wanamgambo wa White Army. Old Fangak, ambapo shambulio dhidi ya hospitali ya MSF lilifanyika, ni moja ya miji mikuu katika Kaunti ya Fangak, katika Jimbo la Jonglei, eneo la nchi hiyo lenye Wanuer wengi na ambalo kihistoria linahusishwa na chama cha upinzani cha Sudan People's Liberation Movement-in-Opposition (SPLM-IO) kinachoongozwa na Machar. Kulingana na Kamishna wa Kaunti Biel Boutros, helikopta na ndege zisizo na rubani zilizotumika katika uvamizi wa wikendi ni mali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPD), na hatua zao zimewaondoa zaidi ya watu 30,000 kutoka eneo hilo. Katika majuma ya hivi karibuni, kundi la White Army lilishambulia ngome ya SSPD huko Nasir, Jimbo la Upper Nile, na kusababisha wimbi la kukamatwa kwa serikali ya Juba, inayotawaliwa na kabila la Dinka, na kampeni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo hao.

06 Mei 2025, 12:17