Tafuta

Wapalestina wakisubiri kupata chakula katika jiko la upendo. Hali ni ngumu sana watoto wanalia kwa njaa na utapiamlo wa kukithiri. Wapalestina wakisubiri kupata chakula katika jiko la upendo. Hali ni ngumu sana watoto wanalia kwa njaa na utapiamlo wa kukithiri.  (q)

UNICEF-WFP:ripoti mpya inaeleza kuwa Watoto huko Gaza wako katika hatari ya njaa!

UNICEF na WFP zinatahadharisha kuhusu maafa yanayokuja,ambapo watoto 71,000 na zaidi ya akina mama 17,000 wanatishiwa na utapiamlo mkali na njaa. "Familia huko Gaza wana njaa huku chakula wanachohitaji kikikwama mpakani kukipata kwa sababu ya mzozo mpya na umarufuku wa jumla wa misaada ya kibinadamu uliyowekwa mapema mwezi Machi,"alisema hayo Cindy McCain,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Watu katika Ukanda wa Gaza wako katika hatari ya njaa kutokana na mapigano mapya, vivuko vya mpaka bado vimefungwa na uhaba wa chakula hatari. Njaa na utapiamlo vimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu kusitishwa kwa upatikanaji wote wa misaada mnamo Machi 2, na kurudisha nyuma mafanikio ya wazi ya kibinadamu yaliyopatikana wakati wa usitishaji mapigano mapema mwaka huu. Watu 470,000 huko Gaza wanakabiliwa na janga la njaa (IPC Awamu ya 5) na wakazi wote wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, kulingana na ripoti ya Ainisho ya Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC) iliyotolewa  tarehe 12 Mei 2025.

Watoto 71,000 kutishiwa na utapiamlo

Ripoti hiyo pia ilitabiri kwamba watoto 71,000 wa kutishiwa  na utapia mlo na zaidi ya akina mama 17,000 watahitaji matibabu ya haraka kwa utapiamlo uliokithiri. Mashirika yalikadiria kuwa watoto 60,000 wangehitaji matibabu kufikia mapema 2025. "Familia huko Gaza wana njaa huku chakula wanachohitaji huku kikikwama mpakani. Hatuwezi kukipata kwa sababu ya mzozo mpya na umarufuku wa jumla wa misaada ya kibinadamu uliyowekwa mapema mwezi Machi,"alisema hayo  Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP). "Ni muhimu kwamba Jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za haraka ili kupata misaada inayotiririka tena Gaza. Ikiwa tutasubiri hadi njaa ithibitishwe, kwa watu wengi itakuwa tayari kuchelewa."

Ripoti ya IPC Gaza inatabiri kuwa operesheni mpya za kijeshi, ambacho ni kizuizi kinachoendelea na ukosefu mkubwa wa vifaa muhimu vinaweza kusukuma uhaba wa chakula, utapiamlo mkali na viwango vya vifo zaidi ya kizingiti cha njaa katika miezi ijayo. Idadi kubwa ya watoto huko Gaza wako katika uhaba mkubwa wa chakula, kama ilivyothibitishwa na mashirika 17 ya Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine yasiyo ya kiserikalia(NGOs) katika ripoti ya IPC.  Pamoja na upatikanaji mdogo wa huduma za afya na uhaba mkubwa wa maji salama na vyoo, utapiamlo unatarajiwa kuongezeka kwa kasi katika majimbo ya Gaza Kaskazini, Gaza na Rafah.

Wito kwa pande zote kuacha mzozo

"Hatari ya njaa haiji mara moja. Inajidhihirisha katika maeneo ambayo upatikanaji wa chakula umekatika, ambapo mifumo ya afya imepungua na ambapo watoto wanaachwa bila mahitaji ya kimsingi ya kuishi.  Njaa na utapiamlo mkali ni hali halisi ya kila siku kwa watoto katika Ukanda wa Gaza,” Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell alisema: “Tumeonya mara kwa mara dhidi ya matarajio hayo na kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa pande zote kuepuka janga.

Vivuko vya mpakani na Gaza vimefungwa kwa zaidi ya miezi miwili - muda mrefu zaidi ambao idadi ya watu wamewahi kukumbana nayo - na kusababisha bei ya chakula katika masoko kupanda na kuacha chakula kidogo kinachopatikana nje ya familia nyingi. Wakati huo huo, zaidi ya tani 116,000 za msaada wa chakula - zinazotosha kulisha watu milioni moja kwa hadi miezi minne - tayari zimewekwa kwenye barabara za misaada, tayari kuletwa. Mamia ya aina za matibabu ya kuokoa maisha kupitia  lishe pia yamewekwa tayari kwa kuingia. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yapo tayari kufanya kazi na washikadau wote na washirika wa usalama wa chakula ili kupata vifaa hivi vya chakula na lishe na kuvisambaza mara tu mipaka itakapofunguliwa kwa ajili ya utoaji wa misaada yenye kanuni.

Juhudi za WFP na UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na UNICEF zimesalia ardhini huko Gaza tayari kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa mujibu wa kanuni zinazohitajika za kibinadamu. Mnamo tarehe 25 Aprili, WFP iliishiwa na chakula cha mwisho cha kusaidia jiko la chakula cha moto kwa familia. Juma moja kabla, majiko yote 25 yanayoungwa mkono na WFP ilifungwa kutokana na kukosa unga wa ngano na mafuta ya kupikia. Katika juma hilo hilo, vifurushi vya chakula vya Shirika la Mpango na Chakula(WFP) kwa familia - na  majuma mawili ya  mgao wa chakula  viliishwa. UNICEF inaendelea kutoa huduma muhimu za maji na lishe, lakini akiba kwa ajili ya kuzuia utapiamlo imeisha na vifaa vya kutibu utapiamlo uliokithiri havitoshi. UNICEF na WFP zinataka pande zote kuweka kipaumbele mahitaji ya raia na kuruhusu kuingia mara moja kwa msaada huko Gaza, kuheshimu majukumu yao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

13 Mei 2025, 14:40