2025.09.12 Mkutano wa Kimataifa kuhusu Udugu wa Kibinadamu. 2025.09.12 Mkutano wa Kimataifa kuhusu Udugu wa Kibinadamu. 

Tamasha la 'Neema kwa Ulimwengu,'wasanii wa kimataifa watakuwa uwanja wa Mt.Petro

Katika Tamasha la Neema kwa Ulimwengu litawaona Pharrell Williams na Andrea Bocelli wasanii maarufu na wengine katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican,usiku saa 3.00 masaa ya Ulaya,Jumamosi Septemba 13.Hii ni sehemu ya maadhimisho ya Mwaka wa Jubilei 2025 na alama ya kufungwa kwa Mkutano wa Kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu,katika kueneza ujumbe wa umoja kati ya tamaduni na watu uliofanyika tarehe 12 na 13 Septemba 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi saa 3.00 usiku masaa ya Ulaya, tarehe 13 Septemba 2025, watazamaji  ulimwenguni kote wanaalikwa kufurahia tamasha la ajabu, la “Grace for the world”- “Neema kwa Ulimwengu” linaloongozwa na wana maono miongoni mwao  Pharrell Williams na Mwalimu Andrea Bocelli na wengine wengi,  watu maarufu duniani kote wa kisanii. Chini ya anga lenye nyota inayoangazia Jiji la Vatican na zaidi Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, katikati ya Uwanja wa Mtakatifu  Petero, tukio hili la aina yake litachanganya sanaa na muziki katika uzoefu mkubwa wa ushirika na ubunifu.

Bocelli aiimba Mbele ya Papa Leo wakati wa uzinduzi wa Borgo Laudato Si
Bocelli aiimba Mbele ya Papa Leo wakati wa uzinduzi wa Borgo Laudato Si   (ANSA)

Jukwaa hilo litakuwa na maonesho yasiyosahaulika ya Pharrell Williams pamoja na Kwaya ya Sauti ya Moto ya Injili, Andrea Bocelli, John Legend, Karol G, Jennifer Hudson, BamBam, Clipse, Teddy Swims, Jelly Roll, Angélique Kidjo, na Kwaya ya Jimbo la Roma ikiongozwa na Mwalimu wake Mkuu Padre Marco Frisina, wakijumuika na kwaya ya kimataifa ya Blackstone.

Tamasha hili litaakisiwa na onyesho la kuvutia na la ndege zisizo na rubani na Nova Sky Stories, lililochochewa na kazi bora za Kikanisa cha Sistine: mchanganyiko ambao haujawahi kushuhudiwa wa teknolojia na sanaa takatifu.  Maadhimisho haya yanaadhimisha Mwaka wa Jubilei 2025 na kuashiria kufungwa kwa Mkutano wa Kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu wa tarehe 12 hadi 13 kuhusu "World Meeting on Human Fraternity "- yaani Udugu wa Kibinadamu, "kueneza ujumbe wa umoja kati ya tamaduni na watu.

Papa alikutana na washiriki wa Mkutano Kimataifa wa udugu wa kibinadamu
Papa alikutana na washiriki wa Mkutano Kimataifa wa udugu wa kibinadamu   (@Vatican Media)

Tarehe 12 Septemba 2025 washiriki wa Mkutano huo walikutana na Baba Mtakatifu Leo XIV  na katika hotuba yake kwa kujikita katika moja ya simulizi ya kibiblia kuhusu Kaini na Abeli, alirudia kuuliza swali: “Ndugu, dada, uko wapi? Swali ambalo linajitokeza katika biashara ya vitakati ya wahamiaji waliodharauliwa, maskini wanaolaumiwa kwa umaskini wao,na waathiriwa wa upweke. Njia iliyoonyeshwa na Baba Mtakatifu “ni ile ya mwelekeo mwingine wa maisha, ukuaji, maendeleo."


Papa aliwataka washiriki wa mkutano  huo kutambua mipango "ndani na kimataifa" ambayo inakuza nafasi mpya za "upendo wa kijamii, mashirikiano kati ya maarifa na mshikamano kati ya vizazi. Alisema kuwa waache iwe mipango ya msingi ambayo pia inajumuisha maskini, sio kama wapokeaji wa misaada, lakini kama mada ya utambuzi na mazungumzo.”

13 Septemba 2025, 13:06