Madagascar:hali ni tete kutokana na maandamano dhidi ya serikali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni majuma mawili sasa hali nchini Madagascar inaendelea kuwa ngumu kutokana na maandamano ya vijana. Padre Cosimo Alvati,Msalesiani mwenye uzoefu mkubwa wa kimisionari nchini Madagascar, aliiambia shirika habari za Kimisionari Fides kwamba, "Madagascar iko katika hali ya mashaka, ikingoja matamko ya Rais Andry Rajoelina,". Na alisisitiza jinsi ambavyo alishtushwa kwa majuma mawili ya maandamano yaliyoanza Septemba 25. Baada ya ukandamizaji mkali wa maandamano, kitengo cha kijeshi, Capsat, kiliomba vikosi vya usalama mnamo Oktoba 11 "kukataa kuwafyatulia risasi" waandamanaji. “Mtazamo wa wanajeshi, ambao wanaonekana kuunga mkono idadi ya watu, bado haujawa wazi kabisa,” mmisionari huyo alisema.
Serikali mpya ilitangazwa lakini bado kuwa rasmi
"Kwa upande wake, maaskari hao bado wanaonekana kuwa waaminifu kwa Rais. Ili kutuliza mambo, serikali mpya ilitangazwa, lakini hadi sasa ni majina ya mawaziri watatu pekee ndiyo yametolewa." Rais ambaye bado hajulikani aliko, alitoa hotuba kwa taifa itakayooneshwa Jumatatu Oktoba 13, saa 1:00 jioni masaa ya nchi yao. "Huu ni mtindo ambao tumeona hapo awali, mwaka 2009, wakati Raojelina mwenyewe alichukua mamlaka kufuatia maandamano ya wananchi dhidi ya Rais wa wakati huo Marc Ravalomanana. Ravalomanana mwenyewe alichukua mamlaka mwaka 2002 kwa kuungwa mkono na baadhi ya wanajeshi baada ya makabiliano makali na Rais anayeondoka Didier Ratsiraka,” alikumbuka Padre Cosimo.
Inasemekana watu 20 wamekufa kutokana na maandamano
Maandamano ya siku za hivi karibuni yamekandamizwa kwa umwagaji damu; kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, kulikuwa na angalau vifo 20 kati ya waandamanaji, lakini hakuna takwimu rasmi zilizotolewa na mamlaka ya Nchi hiyo. "Magenge ya wahalifu yanachukua fursa ya machafuko, yanawinda watu waliochoshwa na umaskini," mmisionari alisisitiza. "Wakati uchumi wa kuishi unatawala mashambani, mijini, sehemu kubwa ya watu wanaishi katika umaskini, ikiwa sio njaa halisi. Ikiwa Wamalagasi hawatapewa matarajio halisi ya kukua, maasi ya aina hii yataendelea kuzuka,” alihitimisha Padre Cosimo.
Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui