Tafuta

Hali ya watoto katika makambi ya Wakimbizi huko Kusini mwa Kordofan, Sudan. Hali ya watoto katika makambi ya Wakimbizi huko Kusini mwa Kordofan, Sudan. 

Usafirishaji wa silaha unaongezeka huku kukiwa na mzozo wa kibinadamu wa Sudan

Usafirishaji wa silaha na masuala ya kibinadamu yamezidi kukithiri mipaka nchini Sudan,huku mitandao ya magendo ikinufaika kutokana na msukosuko ulioko nchini humo,huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na njaa,magonjwa na kuondolewa kwenye makazi yao.

Na Sr. Christine Masivo, CPS, - Vatican.

Mpango wa kimataifa dhidi ya uhalifu uliopangwa umetoa ripoti mpya inayoonyesha kuwa kuna ongezeko la biashara ya silaha zinazochochea vita kati ya Jeshi la Sudan (SAF). Ripoti iliyotolewa tarehe 20 Oktoba 2025, inaeleza kuhusu usafirishaji haramu na madalali wahalifu,wanaofufua njia za zamani kupitia Darfur, Chad Mashariki na kusini mwa Libya.

Mgogoro wa kibinadamu unazidi kuongezeka

Kulingana na Umoja wa Mataifa hali ya Sudan inaendelea kuzorota kwa kasi. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) imethibitisha kuwa watu takriban milioni 25, au nusu ya wakazi wa Sudan, wanakabiliwa na njaa kalia. Mnamo mwezi Septemba iliyopita, Umoja wa Mataifa ulirekodi hali mbaya zaidi kwa miaka mitatu iliyopita tangu mzozo huo uanze Aprili 2023. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Darfur na Kordofan, ambapo miundombinu imeharibiwa na kuachwa ikiwa imechakaa bila huduma muhimu, kama vile huduma za afya, chakula na maji. Mji wa El Fasher Kaskazini mwa Darfur umezingirwa na vikosi vya RSF, ambavyo vinadaiwa kulenga kambi zenye watu wengi waliokimbia makazi yao kwa mashambulizi ya kiholela." Raia wanafanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, kulazimishwa kuajiriwa na kuwekwa rumande kiholela," ilisema ripoti ya Umoja wa Mataifa. "Jengo la Umoja wa Mataifa huko El Fasher lilishambuliwa kunako Septemba 20, na kupoteza magari, na vifaa vingine."

Taifa lililogawanyika

Vita vimepamba moto zaidi Kusini mwa Kordofan karibu na El Obeid, kituo kikuu cha usafiri kinachounganisha Khartoum na Darfur, na kufanya nafasi za watu kutoa misaada kuwa ngumu zaidi kwa miaka mingi. Miji ya Dilling na Kadugli imezingirwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na utekaji nyara, kuwekwa jela, na vitisho kwa wafanyakazi wanaotoa huduma. Mafuriko yameharibu njia kuu za usafirishaji wa bidhaa, hasa Nyala-Mashariki huko Darfur, na barabara kadhaa za mitaa, na kusababisha kuzuka kwa kipindupindu, dengwe na malaria. Magonjwa haya yameathiri sana jamii zinazotatizika kuishi, ikiwa ni pamoja na huko Khartoum ambako wakazi wamekosa huduma za msingi kama vile umeme na maji kwa siku kadhaa. Kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa, "licha ya changamoto nyingi, wenzetu wanaotetea haki za kibinadamu, wanaendelea kutoa msaada muhimu kwa watu waliohamishwa katika maeneo ambayo sisi na washirika wetu tunaweza kufikia kwa usalama."

Sudani hali ni ngumu kwa hadhi ya binadamu
22 Oktoba 2025, 14:44