Tafuta

Uchaguzi Mkuu Tanzania Uchaguzi Mkuu Tanzania  (EMMANUEL HERMAN kalimanzila10@gmail.com)

Watanzania waalikwa kumchagua rais na wabunge:utulivu mashakani

Uchaguzi Mku wa Rais Nchini Tanzania,tarehe 29 Oktoba unaendelea tangu alfajiri,japokuwa umekumbana na maandamano kama yalivyokuwa imesikika hawali katika baadhi ya miji kama Dar Es Salaam.Rais Samia alipiga kura huko Dodoma.Kwa upande wa Zanzibar,hali ilikuwa shwari asubhi ambapo kupitia CCM,Dk.Hussein Ali Mwinyi,alikwenda kupiga kura.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya kuchagua viongozi, ni muhimu kutambua kwamba Mpiga kura ana haki mbalimbali zinazotambuliwa na sheria za Tanzania zikiwamo kupiga kura kwa siri, kumpinga mgombea asiye na sifa na kupiga kura bila ubaguzi.  Mbali na haki pia ana wajibu wa kuheshimu maamuzi ya wengine hata kama hayafanani na yake, kutoa taarifa ya udanganyifu na kudumisha amani na utulivu kwenye eneo la kupigia kura. Ni katika muktadha huo ambapo tarehe 29 Oktoba 2025, inawaona wanachi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kufanya zoezi hili la kuchagua viongozi wao wanaostahili.

"Nimeona waandishi wengi wa habari wakiripoto matukio mbalimbali yanayoendelea"

Rais Samia Suluhu Hassan, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kutekeleza haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka, baada ya yeye mwenyewe kupiga kura mjini Dodoma. Katika maelezo yake alisema “Nilikuwa nafuatilia zoezi hili tangu asubuhi na nimeona waandishi wengi wa habari wakiripoti matukio mbalimbali yanayoendelea. Baada ya kupata picha kamili ya mwenendo wa zoezi, nikaona ni wakati muafaka wa mimi kuja na kukamilisha wajibu wangu huu. Niwaombe Watanzania waendelee kujitokeza na kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua viongozi wanaowataka, ili tumalize zoezi hili kwa amani na tuendelee na shughuli zetu za kila siku.” Na ninawashukuru waandishi wa habari na muendelee kuhamasisha, asante sana.” https://youtu.be/fJZw3yrtEGg

Lakini wakati Rais Samia akisema hayo, hali ya taharuki ilionekana kwenye mitandao katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, ambako waandamanaji walifanya vurugu, kuchoma moto baadhi ya vituo vya mabasi na kuwashambulia hata Askari Polisi kwa mawe. Na hiyo ilionesha hata Polisi kurusha mabomu hewani kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji kwenye maeneo ya barabara ya Mandela-Ubungo, huku kituo cha mabasi ya mwendo kasi cha Magomeni kikionekana kuvamiwa na mabasi yaliokuwepo kuchomwa moto.

Maandamano hayakukosa
Maandamano hayakukosa   (AFP or licensors)

Uchaguzi bila upinzani mkali

Kwa hiyo uchaguzi wa Urasi Tanzania kwa mwaka 2025 unafanyika bila ushiriki wa vyama vikuu vya upinzani Tanzania bara kama vile cha  Chama cha  Chadema ambacho tangu awali kilijitoa kwa kuacha chama tawala cha (CCM) kikiwa karibu bila mpinzani. Chama kikubwa cha upinzani nchini, Chadema, kimesusia uchaguzi huu hasa baada ya kiongozi wake, Tundu Lissu, kufungwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini kufuatia wito wake wa mageuzi ya mfumo wa uchaguzi. Luhaga Mpina, mgombea urais wa chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani, Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), aliondolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa njia hiyo Wagombea 16 wa upinzani kutoka vyama vidogo wameorodheshwa kwenye kura.

Shirika la Amnesty International, Uchaguzi wa hofu

Kadhalika kwamba uchaguzi huu unafanyika kwa hofu kubwa kutokana na matukio kadhaa yaliyojitokeza ya kukosa usalama, ambapo Mashirika ya haki yataja "wimbi la hofu” kuelekea uchaguzi kama vile Shirika la Amnesty International lililaani kile lilichokiita “wimbi la hofu” kabla ya uchaguzi, likieleza kuwepo kwa “kutoweka kwa watu kwa kulazimishwa, mateso na mauaji ya kiholela ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati.”

Na Mpinzani wa Chama cha Chadema, Tundu Lissu, anakabiliwa na kesi ya uhaini ambapo hadi sasa anajitetea mwenyewe kama Mwakili mahakamani. Chama chake, Chadema, kilikataa kushiriki katika uchaguzi. Mgombea mwingine aliyekuwa na nguvu, Luhaga Mpina wa ACT-Wazalendo, aliondolewa kwa sababu za kiufundi.

Shirika la Human Rights Watch na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Na kwa upande wa Shirika la Human Rights Watch lilisema “mamlaka zimekandamiza upinzani wa kisiasa na wakosoaji wa chama tawala, kuziba midomo ya vyombo vya habari, na kushindwa kuhakikisha uhuru wa tume ya uchaguzi.” Kuna hofu kwamba hata baadhi ya wanachama wa chama tawala wanakuwa walengwa. Humphrey Polepole, msemaji wa zamani wa CCM na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, alitoweka nyumbani kwake mwezi Oktoba  baada ya kujiuzulu na kukosoa serikali.  Na wakati huo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema kimebaini visa 83 vya utekaji watu tangu Rais Suluhu aingie madarakani, huku vingine 20 vikiripotiwa juma  za karibuni.

Sehemu nyingine za Tanzania  huko Arusha

Kwa mujibu wa vyombo vya ndani ya nchi vinabainisha kwamba Mitaa ya jiji la Arusha, Kaskazini mwa Tanzania, ilianza na siku ikiwa kimya huku kukiwa na idadi ndogo ya vyombo vya usafiri barabarani, maduka mengi yakiwa yamefungwa na vituo vya kupigia kura vikiwa na wapiga kura wachache au havina kabisa.  Katika baadhi ya maeneo aliyotembelea, maafisa wa polisi walionekana wakizunguka kuhakikisha usalama, wakati raia wachache wakiendelea na shughuli zao za kila siku. Vituo vingi vya kupigia kura vilionekana vikiwa tupu, hali inayochukuliwa kama ishara ya wananchi kutojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo.

Zanzibar

Kwa upande wa zoezi la uchaguzi huko Zanzibar lilianza vizuri, ambako japokuwa taarifa ni kwamba, waandishi wengi wa habari wa kigeni walizuiliwa kusafiri hadi bara kushuhudia uchaguzi huo. Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alikwenda kupiga  kura katika Kituo cha Kariakoo, Jimbo la Kwahani, akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi, majira ya saa 2.25 subuhi, tarehe 29 Oktoba 2025. Vyama kumi na moja vya siasa vimesimamisha wagombea wa urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. https://youtu.be/4QgPxbVcGPM

Baada ya kupiga kura, Dk, Mwinyi alipongeza “hali ya amani na utulivu iliyoshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura nchini kote, akisema mazingira hayo yanatoa fursa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutekeleza wajibu wao wa kikatiba na kidemokrasia. Alisema kuwa “Chama Cha Mapinduzi kina matumaini makubwa ya ushindi kutokana na mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya 2020 hadi 2025 pamoja na miradi mikubwa ya maendeleo iliyotekelezwa katika sekta mbalimbali.”

29 Oktoba 2025, 14:52