Tafuta

Wawakilishi wa  vijana katika COP30:Ernne John Dolor,Amber Vanneck Fidelis Stehle,Prisca Kuworde na Antonio Korkuvi. Wawakilishi wa vijana katika COP30:Ernne John Dolor,Amber Vanneck Fidelis Stehle,Prisca Kuworde na Antonio Korkuvi. 

Kilio cha Haki ya Tabianchi Afrika:Mjumbe wa vijana wa Kikatoliki katika COP30

Antonio Korkuvi kutoka Ghana anaomba ulimwengu kuheshimu wito wa kimaadili wa Laudato si’ na kuunga mkono jamii ambazo zinaishi na athari ya mgogoro ambao hawakuuanzisha.Alisema hayo wakati wa mazungumzo jayo na Vatican wakati wa COP30 kabla ya kukunja jamvi..

Na Francesca Merlo - Belém, Brazil.

Huko Belém, sauti ya mpatanishi kijana wa Ghana ilikuwa na  uzito wa bara zima. Antonio Yayrator Korkuvi, aliyewakilisha Shirikisho la Kimataifa la Harakati za Vijana wa Kanisa Katoliki, alizungumzia sio tu kwa ajili ya Ghana, lakini kwa ajili ya Afrika ambaye ni kiongozi mmoja kijana aliyechaguliwa kuwakilisha eneo ambalo tayari linaishi matokeo ya mzozo ambao hawakuuanzisha. "Tunachangia asilimia nne tu ya hewa chafu duniani," aliambia Vatican News kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Tabianchi COP30 "lakini tunabeba mzigo mkubwa wa mabadiliko ya Tabianchi”

Antonio anaishi kando ya pwani ya Ghana, ambapo kila mwaka bahari huinuka zaidi na zaidi bara. Alielezea matokeo yanayoonekana sana. "Watu wanapoteza makazi yao, ardhi yao - kila kitu kinachowaunganisha na historia yao. Bahari inapoondoa hiyo, inachukua sehemu ya wao ni nani." Hii, alisema, si tu hasara ya kimwili. Ni kisaikolojia, kiroho, kizazi.” Alieleza kuwa ni mgawanyiko ambao unaleta jamii za Kiafrika kwenye historia za watu wao. Na hivyo katika COP30 na, katika vyumba vya mazungumzo, amekuwa akipeleka ukweli huo kwa wale wote ambao wanauelewa mdogo.

Kushughulikia usawa         

“COP inaitwa kupokea COP” Antonio alibainisha. "Lakini wale ambao walisababisha tatizo yaani wa Kaskazini mwa Dunia   wanasitasita hata kutoa fedha zinazohitajika kwa jamii kubadilika." Kuna usawa mkubwa unaoshughulikiwa katika COP, ambapo fedha za Tabianchi zinaendelea kuweka kipaumbele katika kukabiliana na hali hiyo, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa muda mrefu, wakati wale ambao tayari wanateseka wanapiga kelele kwa msaada wa haraka ili tu kustahimili dhoruba ijayo au ukame unaofuata. Antonio alielezea mvutano ambao amepitia kwenye vyumba vya mazungumzo. Nchi za Kaskazini mwa Ulimwengu  zinalinda nafasi zao huku nchi za Kaskazini mwa Ulimwengu, huku Nchi za Kusini mwa Ulimwengu zikisubiri.

Haja ya haki ya Ikolojia fungamani

Neno linalomgusa zaidi Antonio ni haki. Alibainisha kuwa muongo mmoja umepita tangu Laudato si’ kuhimiza ulimwengu kutambua uumbaji kama "nyumba yetu ya pamoja." Hivi karibuni zaidi, ulichapishwa Waraka   Laudate Deum ukisasisha wito huo kwa uharaka wa kinabii. Nyaraka hizi ni dira za maadili," alisema. "Lakini nchi nyingi hazifanyi kazi kwa maadili." Alikumbuka ombi la Papa Francisko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR) wakati wa Ziara yake ya Kitume, ambapo alisema:” ondoeni mikono Afrika,”Ombi hili, Antonio alibainisha, si tu kwa ajili ya kulindwa kutokana na migogoro na unyonyaji, bali kutokana na dhuluma za kimazingira ambazo sasa zinatishia mustakabali wa bara. "Ni wakati wa Ulimwenhu wa Kaskazini kusikiliza," alisema, "ili nchi zinazokabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi ziweze kujenga ustahimilivu." Katika hilo, Antonio alikuwa na  ujumbe wazi kwa COP kwa ujumla kwamba utunzaji wa uumbaji  kuwa hauwezi kutenganishwa na utunzaji kwa maskini kwani alidai kwamba “ sio sera tu, bali uongofu  bali ni uongofu wa kiikolojia,"

25 Novemba 2025, 11:29