Tafuta

Meli za hospitali zikiendelea na urithi wa Papa Francisko huko Amazonia

Pembeni mwa COP30 huko Belém,Brazili,boti za hospitali zimetiwa nanga kando ya mto,zikitoa msaada wa kimatibabu kwa wale wanaohitaji zaidi.Boti hizo,zikiongozwa na Papa Francisko,husafiri kando ya Mto Amazon yote ili kushughulikia mahitaji ya jamii za Wenyeji na wale wanaoishi kando ya mto,mbali na miji.Huu ni ushuhuda wa Felipe, daktari wa kujitolea.

Na Francesca Merlo - Belém, Brazil 

Kwenye kingo za Mto Guajará, watu hupanga foleni kupanda Hospitali ya Boti ya Mtakatifu Yohane XXIII. Hii si boti ya kawaida inayobeba abiria kwenda visiwa vya karibu. Badala yake, Boti ya Hospitali ya Mtakatifu Yohane XXIII husafiri kando kando  ya Mto Amazona hadi kwenye pembe za ndani kabisa za msitu mkubwa wa mvua duniani yaani maeneo yanayofikiwa tu kwa maji, na kupeleka huduma ya matibabu ambapo ni haba. "Hakuna barabara zinazoelekea kwenye baadhi ya maeneo tunayotembelea," alisema Felipe, mtaalamu wa macho mwenye umri wa miaka 28 kutoka Minas Gerais, Brazil. "Wakati mwingine boti husafiri kwa siku mbili au tatu kabla ya kumfikia mtu yeyote."

Felipe ni mmoja wa madaktari wengi wa kujitolea ndani ya Mtakatifu Yohane XXIII, moja ya hospitali tatu zinazoelea zinazopeleka huduma ya matibabu ya bure kwa jamii za mbali za mto na Wenyeji wa Amazonia. Imetia nanga kando yake huko Belém, Pará, na nyingine, Boti ya Papa Francisko.  Zote  mbili pamoja na boti yao ya tatu dada, ya Mtakatifu Yohane Paulo II, vilitolewa na Papa Francisko ambaye alielezea nia yake, wakati wa Siku ya Vijana Duniani huko Brazili mwaka wa 2013, kwamba watu wa Amazonia wasipuuzwe na jumuiya za kitawa.

Alimuuliza Ndugu Francisco Belotti, "Uko Amazonia?" na Ndugu Francisco alipojibu "hapana", Papa Francisko alimwambia: "Unapaswa kwenda." Wito wake ulikuwa wa kufikia pembezoni, na mwaka wa 2019, ulijibiwa. Kwa pamoja, tangu wakati huo, boti hizi zimeunda kundi dogo la madaktari, wauguzi, na watu wa kujitolea ambao husaidia wale ambao vinginevyo wangeachwa bila kuonekana. Watu milioni moja wamefaidika hadi sasa.

Brother Francisco

Ndugu Francisco

"Kwa kawaida, watu huenda hospitalini," Felipe ananiambia. "Hapa, tunaenda kwa watu." Mtakatifu Yohane XXIII kwa sasa inahudumia jamii zilizo karibu na Belém, zilizosimama kwenye mto katika siku za mwanzo za COP30 karibu na  ile ya Papa Francisko inapojiandaa kwa misheni yake inayofuata ndani zaidi ya msitu. Siku hizi, ni watu wa Belém wanaonufaika na huduma zinazotolewa na boti.

Jikoni, wapishi wako bize kupika milo kwa ajili ya watu wanaosubiri. Pamoja na jikoni, ndani ya boti, kuna vyumba vya ushauri, kumbi za upasuaji, maabara na mtaalamu wa kemia - vyote vimewekwa ndani ya kile kinachoonekana kutoka nje kama boti ya kawaida ya mto. "Tuna kila kitu hapa," Felipe alielezea. "Tunafanya ushauri, upasuaji, uchunguzi - kila kitu kuanzia upasuaji wa mtoto wa jicho hadi taratibu ndogo za jumla." Matatizo ya kawaida, alisema, ni yale ambayo yangeweza kutibiwa kwa urahisi katika maeneo ya mijini lakini yameachwa kuwa mabaya zaidi kutokana na ukosefu wa ufikiaji: maambukizi, hernia, mtoto wa jicho. "Baadhi ya watu husubiri kwa miaka mingi kwa ushauri wao wa kwanza," alisema. "Wengine husafiri saa nyingi kwa mtumbwi ili kutufikia."

Mahali hapa ni safi. Hutunzwa na watu wa kujitolea na wafanyakazi kana kwamba ni nyumbani kwao. Felipe anawapenda watu anaowahudumia. "Watu hapa ni baadhi ya watu wema zaidi ambao nimewahi kukutana nao," alisema. "Wanatuamini kabisa, na hutoa mengi - hata wanapokuwa na kidogo sana. Jana, mgonjwa alinipa tunda ambalo sijawahi kuona hapo awali. Mwingine aliniletea mfuko wa jambu - jani ambalo lina athari ya ganzi mdomoni mwako - kwa sababu tu alinisikia nikisema kwamba sijawahi kuwa nalo hapo awali. Ni aina hii ya upendo inayokufanya utake kurudi tena." Watu wawili wanasimamisha kuniuliza: "Je, wewe ni daktari?" wanamuuliza, kabla ya kuniomba niwapige picha. Felipe, ambaye hufanya upasuaji wa macho hadi kumi na kuwaona wagonjwa kadhaa kila siku, anasema uzoefu huo haubadilishi tu wale wanaopokea huduma bali pia wale wanaoitoa. "Sio tu kuhusu hisani," anasema. "Ni kuhusu mabadiliko - kwao na kwetu."

Ndoto ya Papa Francisko

Anaashiria kuelekea Boti jirani ya Papa Francisko. "Ilikuwa ndoto yake," Felipe anasema. "Ndoto ya kuwafikia wale walio mbali, si kijiografia tu bali pia kijamii. Na nadhani angejivunia sana kinachotokea hapa." Huku COP30 ikiendelea huko Belém, boti kando ya Mto Amazona zinawakumbusha wale wanaohudhuria kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya kuwatunza watu na kuwatunza nyumba yetu ya pamoja. "COP inahusu mabadiliko," Felipe alisema. "Ni kuhusu kutambua kwamba sote ni tofauti, lakini kwamba kuna kitu kinachotuunganisha - wema, kujaliana, na kwa uumbaji. Boti hii ni uthibitisho wa uhusiano huo." Safari yake ya siku kumi itaisha hivi karibuni, lakini Felipe hawezi kujizuia kufikiria ni lini safari inayofuata itakuwa. "Mara tu nitakapofika nyumbani," anasema, akitabasamu, "Nitaanza kutafuta misheni inayofuata. Sitaki hii iishe."

Ni urithi mzuri sana: Papa Francis bado yuko hapa, katikati ya Amazoni.

The little port where the hospital boats are docked

Bandari ndogo ambapo boti za hospitali huwekwa

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

14 Novemba 2025, 10:14