Tafuta

Hali ya wakimbizi katika Kambi ya El Fasher ni mbaya nchini Sudan Kusini. Hali ya wakimbizi katika Kambi ya El Fasher ni mbaya nchini Sudan Kusini.  (AFP or licensors)

Sudan:Ukatili huko El Fasher unaonyesha 'kutojali kabisa maisha ya binadamu'

Masimulizi ya kutisha ya ukatili ulioripotiwa kufanywa na wanamgambo wa RSF ndani na karibu na jiji la El Fasher,Sudan yanaakisi vita vinavyoendelea vilivyosababisha makumielfu ya vifo na dharura kubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Miaka miwili na nusu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kuanza, vilivyosababishwa na mzozo wa madaraka kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka vya kijeshi, inakadiriwa kuwa watu 150,000 wameuawa na zaidi ya milioni 12 wameyakimbia makazi yao. Juma lililopita, wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) katika eneo la Darfur wanaripotiwa kufanya ukatili dhidi ya raia.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaojaribu kutoa misaada muhimu ya dharura kwa raia wa Sudan wanaokimbilia usalama wao, wenye njaa na wanaokimbia vurugu, walioogopa baada ya kupokea maelezo ya kutisha ya ukatili huo. Denise Brown, mkuu wa shughuli za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Sudan, alisema kwamba wanamgambo wa RSF ndani na karibu na jiji la El Fasher ambalo wametoka kuliteka, wanaonesha kupuuza kabisa ulinzi na haki za raia.

Wanawake na watoto katika makambi nchini Sudan wanapata shida kubwa sana
Wanawake na watoto katika makambi nchini Sudan wanapata shida kubwa sana   (AFP or licensors)

"Mapigano yalipozidi, tulianza kupokea ripoti za kuaminika za mauaji ya raia wasio na silaha, hasa wanaume waliolala chini wakipigwa risasi. Pia tumepokea ripoti za kuaminika za mauaji ya raia wanapojaribu kukimbia mapigano. Pia tumepokea ripoti, ambazo hatujaweza kuthibitisha, za mauaji ya halaiki. Tunaamini kwamba RSF imethibiti na kuzunguka jiji hilo, na watu hawaruhusiwi kuondoka. Kwa hivyo, hali ni mbaya sana," alisisitiza.

Kwa mujibu wa Mwakilishi huyo wa UN, alisema kwamba, inakadiria idadi ya vifo vya raia wakati wa shambulio la RSF kwenye jiji hilo na njia zake za kutokea, na siku zilizofuatia, inaweza kufikia mamia, huku mashahidi wakiripoti mauaji ya wagonjwa na waliojeruhiwa ndani ya Hospitali ya kujifungulia akina mama ya Al-Saudi na katika vituo ambavyo vilikuwa vinatumika kwa muda kama vituo vya matibabu.

Maisha ya Wakimbizi huko El Fasher ni magumu sana
Maisha ya Wakimbizi huko El Fasher ni magumu sana   (AFP or licensors)

Ripoti za kutisha za wasichana na wanawake kubakwa, na  bunduki zimeenea, wakati wakipigwa risasi na vitisho dhidi ya wazee. Wakati huo huo, mawasiliano ya simu yamekatizwa, na hali ya machafuko yakizidi, na kufanya iwe vigumu kupata taarifa za moja kwa moja kutoka ndani ya jiji. Kinachoweza kuepukika ni mateso yanayoendelea kwa watu wa Sudan huku kukiwa na ukimya mkubwa wa Jumuiya ya Kimataifa.

El Fasher, Sudan

 

04 Novemba 2025, 17:14