Umoja wa Mataifa:Wanawake 50,000 wameuawa kwa mwaka
Na Beatrice Guarrera- Vatican.
"Wanawake wakizungumza nasi kutoka El Fasher, kitovu cha janga la hivi karibuni nchini Sudan, wanasimulia kuhusu njaa, kuhamishwa, ubakaji na mashambulizi ya mabomu." Kwa maneno haya, Ginevra Anna Mutavati, Mkurugenzi wa Kanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika katika UN Women, hivi karibuni aliwaelezea waandishi wa habari hali katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini.nBaada ya zaidi ya siku 500 za kuzingirwa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF), unyanyasaji ulioenea - ikiwa ni pamoja na mauaji ya haraka na unyanyasaji wa kijinsia - umerekodiwa. Alisema wanawake, anaendelea kubeba mzigo mzito zaidi. Hata wakiwa wamekimbia, wanaendelea kuwa katika hatari kubwa.
Idadi ya kimataifa inaonesha unyanyasaji ulioenea
Hata hivyo, tishio hilo haliishii tu katika mazingira ya vita. Duniani kote, Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba wanawake milioni 840 - karibu mmoja kati ya watatu - wamepitia unyanyasaji wa kimwili au kingono na mwenzi, unyanyasaji wa kijinsia na mtu ambaye si mwenzi, au vyote viwili, angalau mara moja katika maisha yao. Takwimu hizo zinasisitiza umuhimu wa maadhimisho ya tarehe 25 Novemba 2025 katika Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Unyanyasaji dhidi ya Wanawake.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaakisi moja ya hali halisi ya kusikitisha zaidi: kila baada ya dakika kumi, mwanamke mmoja huuawa mahali fulani duniani. Katika mwaka uliopita, takriban wanawake 50,000 walikuwa waathiriwa wa mauaji ya wanawake, asilimia 60 kati yao waliuawa na wenzi au jamaa. Kwa kulinganisha, ni asilimia 11 tu ya waathiriwa wa mauaji ya wanaume waliuawa na wanafamilia. Ukosefu wa usawa wa kijinsia na chuki dhidi ya wanawake bado ni vichocheo vikuu.
Kwa wastani, wanawake 137 huuawa kila siku. Ingawa ni chini kidogo kuliko mwaka 2023, idadi hii inaathiriwa na ripoti zisizo sawa katika nchi mbalimbali. Hakuna eneo ambalo limeachwa, na Afrika ilirekodi tena idadi kubwa zaidi, ikiwa na waathiriwa wapatao 22,000 mwaka 2024.
Unyanyasaji mtandaoni unaendelea kupanuka
Umoja wa Mataifa unabainisha kuwa maendeleo ya kiteknolojia pia yamechangia aina mpya za vurugu. Hizi ni pamoja na kushiriki picha na taarifa bila ridhaa, kudanganya, na video za kina bandia zilizoundwa kwa kutumia akili unde(AI). Unyanyasaji otomatiki na kampeni za chuki zilizoratibiwa zinawalenga wanawake wa rika zote. Zaidi ya asilimia 38 ya wanawake wanakadiriwa kuwa wamepitia vurugu mtandaoni, huku asilimia 85 wakishuhudia unyanyasaji ukielekezwa kwa wanawake wengine kwenye majukwaa ya kidijitali.
Ahadi ya Talitha Kum
"Ni muhimu sana kwetu kuongeza uelewa, hasa katika Siku hii," alisema Sister Abby Avelino, mratibu wa kimataifa wa Talitha Kum, mtandao wa kimataifa unaoongozwa na Watwa dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Vurugu za kidijitali, alielezea, zinazidi kuenea, na ulimwengu wa mtandaoni sasa ni tovuti kuu ya unyonyaji. Sister Abby alibainisha kuwa wanachama wa mtandao huo wamekusanyika mtandaoni leo kutafakari athari za vita na migogoro kwenye vurugu zinazotokana na kijinsia. "Tulizingatia kwa njia fulani wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu popote walipo - nchini Ukraine, Kusini mwa Dunia, katika mataifa ya Afrika, na pia Asia," alisema. Aliongeza kuwa Ulaya inaendelea kupokea wanawake wengi waliosafirishwa kiharamu, hasa wale wanaolazimishwa kuhama kutokana na mitandao ya usafirishaji haramu.
Kuwafikia waathiriwa na manusura 47,000
Miongoni mwa historia za hivi karibuni, Sr Abby alikumbuka kisa cha mwanamke kijana kutoka Sudan Kusini ambaye aliomba msaada. "Hatukujua alikuwa wapi, lakini mtandao wetu uliweza kumpata," alielezea. Mwanamke huyo alikuwa amepelekwa Chad; Kupitia ushirikiano na washirika nchini Italia, aliweza kuungana tena na mama yake, yeye mwenyewe akiwa manusura wa biashara haramu ya binadamu na wakaungana tena. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Talitha Kum, mtandao huo uliwasindikiza waathiriwa na manusura 47,000 mwaka 2024. "Mawazo yangu leo," Dada Abby alihitimisha, "yanawahusu wanawake na wasichana walioathiriwa na biashara haramu ya binadamu
Kama Talitha Kum, tunaimarisha dhamira yetu ya kubaki karibu na wale wanaoteseka, tukiwapa usikilizaji, ulinzi na huruma, ili kila msichana aweze kugundua tena matumaini, usalama na nguvu ya kuanza tena. Pamoja: 'Talitha Kum' - 'Msichana mdogo, inuka.