Taa ya Chigubhu:Wanafunzi Wanabadilisha Taka kuwa mwanga unaoweza kupyaishwa
Sr. Christine Masivo, CPS- Vatican.
Kiini cha mageuzi haya ya taa ya Chigubhu, kifaa cha kumulika ambacho jina lake linamaanisha "chupa" katika lugha ya Kishona, inayozungumzwa zaidi Zimbabwe. Taa hiyo ilibuniwa na Aluwaine Tanaka Manyonga, kijana kutoka Harare, ambaye aliona changamoto mbili za nchi hiyo ya umaskini wa nishati na kuongezeka kwa taka, yani sio tu shida bali ni nafasi ya ubunifu. Usambazaji wa umeme umekuwa ni changa moto kubwa Zimbabwe. Ni asilimia 44% tu ya watu milioni 15 nchini wana umeme, asili mia zaidi ya 60% wanaoishi vijijini hawana umeme na takwimu hiyo inashuka hadi 20% tu. Kuna kukatika kwa umeme kila siku kwa zaidi ya saa 12, kutokana na viwango vya chini vya maji katika Ziwa Kariba, chanzo kikuu cha umeme wa maji nchini, na miundombinu kuzeeka katika kituo cha umeme cha Hwange.
Kusanikisha mfumo mdogo wa jua
Kutokana na hali hii, Manyonga alianza kufanya kazi miaka minne katika Shule ya Msingi ya Manyoshwa huko Seke. Lengo lake lilikuwa kusakinisha mfumo mdogo wa jua ili kuweka sola kwenye madarasa na kufanya namna ya kuweka chaji simu na kompiuta ya mikononi. Mradi huu ulionyesha hitaji la kina. Wanafunzi walikuwa na hamu ya kusoma, lakini jua lilipotua, giza lilisimamisha masomo yao. Mnamo 2022, ukweli huo ulianza kubadilika. Wanafunzi 30 walipokea taa za Chigubhu vifaa rahisi vya kuwasha vya duara vilivyokusanywa kutoka kwa vijenzi vya kielektroniki vya LED vilivyorejeshwa na kuwekwa kwenye chupa za plastiki na mikebe iliyotumika. Ghugubhu hizi zikipata chaji wakati wa mchana shuleni kwa kutumia nishati mbadala, taa hizi hutoa takriban saa nne za mwanga wa kubebeka, kuruhusu watoto kusoma na kukamilisha kazi za nyumbani jioni.
Taa 1500 kusambazwa Zimbawe
Kufikia 2023, mradi ulikuwa umeendelea zaidi. Badala ya kusambaza taa zilizotengenezwa tayari, wanafunzi walifundishwa jinsi ya kuzijenga wenyewe na jinsi ya kutambua na kurekebisha matatizo ya kimsingi ya kiufundi. Mradi huu ulianza kujisimamaia badala ya kusubiria misaada kwa uwezesha wanfunzi na kuwapa ujuzi, ubunifu, na umiliki moja kwa wanafunzi. Mpango wa taa ya Chigubhu umeenea nje ya Seke. Kupitia kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Ubalozi wa Australia mjini Harare, na makampuni ya ndani kama vile Securico, takriban taa 1,500 zimesambazwa Zimbabwe yote. Athari za mazingira ni muhimu na yanafaa kuzingatiwa. Kulingana na Shirika la Jimbo la Usimamizi wa Mazingira, Zimbabwe hukusanya kila mwaka takriban tani milioni 1.9. Plastiki pekee inachangia takriban tani 342,000 karibu 18% kwa jumla.
Mabadiliko ya taka kuwa rasilimali
Kwa kutumia tena chupa za plastiki na taka za elektroniki ambazo zingechangia uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, taa ya Chigubhu inageuza takataka kuwa rasilimali. Kinachofanya mradi kuwa wa kuvutia sana ni urahisi wake. Haitegemei miundombinu changamano au uagizaji wa bei ghali, lakini nyenzo zinazopatikana nchini na vipaji vya ndani. Katika nchi ambayo vijana mara nyingi wanakabiliwa na fursa ndogo, taa inasimama kama ishara ya uwezekano: uthibitisho kwamba suluhu zinaweza kutokea ndani ya jamii zenyewe. Jua linapotua juu ya Seke, watoto huwasha taa zao zilizotengenezwa kwa mikono, nyuso zao zikiwa na mwanga mwepesi na thabiti. Katika mwanga huo upo zaidi ya uwezo wa kusoma unabeba tumaini, uthabiti, na maono ya siku zijazo inayoendeshwa na uvumbuzi, uendelevu, na utu wa binadamu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku, bofya hapa tu:Just click here