Tafuta

Wakati wa swala ya Kiislamu Wakati wa swala ya Kiislamu  (ANSA)

Ramadhani 2026 na“mshikamano na Waislamu kuelekea ubinadamu uliovunjika"

Imam Nader Akkad anasimulia kuhusu mwezi Mtukufu wa Kiislamu wa kufunga na kusali,ambapo mwaka huu ni sanjari na Kwaresima ya Kikristo "mwezi uliobarikiwa unaowaunganisha watoto wa Ibrahimu."Matashi mema ya Kardinali Zuppi:Si kwa bahati mbaya katika kalenda ni"ishara ya mkutano mkubwa" ambao "unatusukuma kutafuta njia za pamoja za amani na ushirikiano."

Na Francesca Sabatinelli – Vatican.

Kufunga na kusali pamoja ni wakati wa utakaso kwa Waislamu, na kuwaleta karibu zaidi na Mungu na kaka na dada zao. Kuhisi njaa na kiu wakati wa Ramadhani kunamaanisha kuwa nyeti zaidi kwa kinachoendelea duniani, "ambapo kuna watu bila maji ya kunywa, bila chakula cha kutosha. Kuna mshikamano huu uliopo wa Waislamu wenye ubinadamu uliovunjika." Imam Nader Akkad, wa tume ya kisayansi ya uchunguzi wa mwezi katika Msikiti Mkuu wa Roma, alielezea maana kubwa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo unaadhimisha wakati Mtume Muhammad alipopokea mafunuo ya Qur'ani. Mwezi ambao kwa baadhi ya Jumuiya ulianza tarehe 18 Februari, na ambao, hadi Machi 18 au 19, utahitimisha kufunga kuanzia alfajiri hadi jioni, sala, na tafakari kwa karibu Waislamu bilioni 2 duniani kote, na ambao utamalizika kwa siku kuu ya  Eid al-Fitr.

Ramadhani na Kwaresima

"Waislamu," aliongeza Akkad, "wanakuwa na maombi haya ya pamoja yenye nguvu, ukaribu huu na Mungu wakati wa saa ya maombi, wakati wa usiku unaofuata siku nzima ya kufunga." Mwaka huu, Ramadhani ni sanjari na  Kwaresima ya Kikatoliki, ambayo inafikia kilele chake na Pasaka tarehe 5 Aprili, kwa hivyo itakuwa wakati wa kufunga, kutafakari, na kujitafakari kwa Jumuiya  hizo mbili. Mwezi uliobarikiwa, imamu aliuita, "ambao unaweza pia kuwaunganisha watoto wa Ibrahimu katika kushika nguzo muhimu ya dini zao. Kwa sababu kufunga ni kujinyima chakula, lakini pia ni njia ya kuwakaribia na kuwakumbuka kaka na dada zetu, kumkaribia Mungu, ambaye anatuomba tugeuze mawazo yetu kwa ubinadamu wetu. Kwa hivyo, kufunga kwenyewe kunakuwa chombo muhimu si tu kwa kumwabudu Mungu, bali pia kwa kuwa karibu na kaka na dada zetu." Ukaribu huu pia unaoneshwa kupitia upendo,  kuwasaidia wale wasiobahatika na kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Milango iliyofunguliwa na Mlo wa Kidugu

Mwezi wa Ramadhani "una sifa ya milango iliyofunguliwa," alihitimisha Nader Akkad, huku kila mtu akialikwa kushiriki mlo wa kufunga, iftar, "mlo wa kindugu" ambao kupitia huo "tunaweza kujenga uhusiano huu, mshikamano huu miongoni mwa waumini, ili kuanzisha tena uhusiano wenye nguvu zaidi kama watoto wa Ibrahimu."

Kardinali Zuppi: Mkutano wa Mioyo na Maisha

Maneno mengi ya usaidizi na matashi mema yamefikia Jumuiya za Kiislamu nchini Italia. Ujumbe kwa Jumuiya ya Bologna ulitoka kwa Askofu Mkuu wa jiji hilo, Kardinali Matteo Zuppi, ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) alisisitiza jinsi ambavyo Wakristo na Waislamu walivyokea "wakati mmoja wa toba, sala, na mshikamano na maskini zaidi, wanaolazimishwa kufunga mwaka mzima." Kardinali Zuppi alikumbuka jinsi "bahati hii nzuri katika kalenda" ilivyo "ishara ya mkutano mkubwa kati ya mioyo yetu na maisha yetu, ambayo inatusukuma kutafuta njia za pamoja za amani na ushirikiano." Kwa hivyo matumaini kwamba licha ya "ushindi wa vita, kuongezeka kwa ubaguzi, kutoaminiana kwa pande zote tayari kunaingia kwenye dawati la shule," "kuenea huku kwa habari mbaya za kutisha hakutazuia kusikia sauti maridadi ya idadi kubwa ya ishara halisi za mshikamano na wema zinazoashiria maisha ya kila siku, nyumbani, kazini, shuleni, na katika wakati wetu wa mapumziko."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

19 Februari 2026, 09:39