Iran yaonya Marekani kuhusu 'mabomu ardhini'
Nathan Morley na Sr. Christine Masivo, CPS, - Vatican.
Spika wa bunge la Iran alionya kwamba vikosi vya Iran "vinawasubiri wanajeshi wa Marekani kuingia ardhini ili waweze kuwafyatulia risasi," huku mvutano kote Mashariki ya Kati ukiendelea kuongezeka. Maoni ya Mohammad Bagher Ghalibaf yalikuja baada ya Marekani kusema takriban wanajeshi 3,500 wamewasili katika eneo hilo ndani ya meli ya USS Tripoli.
Pentagon inajiandaa kwa wiki kadhaa za operesheni za ardhini nchini Iran, ingawa haijulikani wazi kama Rais Donald Trump atawaidhinisha, Washington Post iliripoti. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Ijumaa kwamba Washington inaweza kufikia malengo yake nchini Iran "bila wanajeshi wa ardhini."
Mashambulizi yaliendelea kote katika eneo hilo. Israeli ilisema ililenga vituo vya amri vya muda huko Tehran. Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Binadamu, au Hrana, liliripoti angalau mashambulizi 701 kote Iran kufikia saa kumi na moja jioni masaa ya huko mnamo tarehe 28 Machi 2026, moja ya jumla ya juu zaidi ya siku moja tangu vita kuanza mwezi mmoja uliopita.
Miundombinu katika nchi za Ghuba pia imeshambuliwa. 'Emirates Global Aluminium'ilisema kiwanda chake kikuu huko Abu Dhabi "kiliharibiwa sana." Waasi wa Houthi wa Yemen walizindua mashambulizi ya makombora kuelekea Israeli Jumamosi tarehe 28 Machi 2026 na kusema mashambulizi zaidi yatafuata.