Tafuta

Tuutazame uliwengu na matukio yake. Tuutazame uliwengu na matukio yake.  (©bogdanserban - stock.adobe.com)

Matukio ya Ulimwengu kuanzia vita hadi mikutano ya amani

Kuanzia Marekani,Iran, Pakistan,Ufaransa,Praga,Roma,Ufalme wa Monaco na Lebanon ambapo Watu 254 wamekufa na 1,165 wamejeruhiwa.Hii ni idadi ya muda iliyochapishwa na Ulinzi wa Raia wa Lebanon kufuatia mashambulizi mengi ya anga ya wakati mmoja katika maeneo kadhaa ya Lebanon yaliyofanywa na Jeshi la Anga la Israeli Aprili 8.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

 "Vikosi vya Marekani vimepelekwa karibu na Iran hadi makubaliano ya kweli." Lango la Hormuz lafungwa baada ya mashambulizi ya Israeli huko Beirut. Vikosi vyote vya Marekani vitabaki "vimepelekwa" karibu na Iran "hadi makubaliano ya kweli yatakapofikiwa," Trump aliandika haya kiukweli. "Ikiwa hilo halitatokea, mapigano ya moto yataanza, makubwa na makali zaidi kuliko tulivyowahi kuona hapo awali," aliongeza, huku akiondoa chaguo la nyuklia.

Kwa kuwa Lango la Hormuz limefungwa, ni Meli nne tu zilizobeba mizigo mizito zimeweza kupita humo, kufuatia mashambulizi ya Israeli huko Lebanon, ambayo Umoja wa Mataifa umetangaza tishio kubwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. Wakati huo Tehran inasema kusitisha mapigano lazima pia kufanyike nchini Lebanon. Hezbollah ilirusha roketi kwenye kibbutz baada ya Israeli kukiuka.

 Pakistan

Balozi wa Tehran nchini Pakistan, Reza Amiri Moghadam, alisema kwamba ujumbe wa Iran utawasili katika mji mkuu wa Pakistan,  Islamabad jioni ya Alhamisi Aprili 9  kwa mazungumzo na Marekani yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Juma.

New York:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya mkutano Aprili 9 kujadili ripoti ya kila mwaka kuhusu shughuli za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Kosovo(UNMIK). Hii imeripotiwa kwenye tovuti ya Umoja wa Mataifa. Mkuu mpya wa ujumbe huo, Peter Due, ambaye alichukua madaraka Januari 2026 na ambaye atawasilisha ripoti ya shughuli hiyo kwa mara ya kwanza. Mjadala wa mwisho wa ripoti ya kila mwaka ya UNMIK ulikuwa tarehe 21 Oktoba 2025, wakati Serbia ilipowakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marko Djuric.

Ufaransa:Toleo la VIII la Jukwaa la Amani Duniani huko Normandy 9-10 Aprili

Katika muktadha wa misukosuko mikubwa ya kijiografia barani Ulaya na kote ulimwenguni, Mkoa wa Normandy unathibitisha tena kujitolea kwake kukuza uelewa wa masuala ya kijiografia ya kimataifa na kukuza utamaduni wa amani. Ni katika tukio la Jukwaa la Amani duniani kwa siku 2 9 na 10 Aprili 2026. "Katika miaka michache tu, Jukwaa la Amani Duniani la Normandy limekuwa haliwezi kutenganishwa na utambulisho wa Mkoa wetu," alisema hayo Hervé Morin, Mkuu wa  Mkoa wa Normandy, ambaye aliongeza: "Kuanzia sasa, Jukwaa litafanyika kila mwaka mwanzoni mwa majira ya kuchipua badala ya vuli." Jukwaa la Amani Duniani litahamasisha ushiriki mpya na wanafunzi wa shule za Sekondari pia.

Kwa upande wa François-Xavier Priollaud, Makamu Mkuu wa Mkoa wa Normandy anayehusika na masuala ya Ulaya na kimataifa na uhamasishaji wa Mkoa, "Jukwaa la Amani Duniani la Normandy limekuwa tukio linalotambulika kimataifa. Kwa kuakisi vijana, linatoa miundo bunifu ili kusaidia kufafanua mabadiliko ya kimataifa yanayojitokeza mbele ya macho yetu,” alisisitiza. Toleo la 8 la Jukwaa linaakisi mikutano, mijadala, na mikutano na watu mashuhuri kutoka  ulimwenguni kote, pamoja na shughuli ndani ya Kijiji cha Amani - nafasi ya mazungumzo na mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali washirika.

Kwa njia hiyo siku mbili za  9 na 10 Aprili,  pia zinaruhusu maandalizi ya kina zaidi ya kielimu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari wakati wa mwaka wa masomo wa 2025-2026, kwa ushirikiano wa karibu na walimu wao. Wanafunzi wengi, waliojiandikisha katika utaalamu wa Historia-Jiografia, Jiografia na Sayansi ya Siasa (HGGSP), watapata fursa ya kushirikiana zaidi na wataalamu wa nyanja hizo, wanadiplomasia, na watafiti, ambao watawasaidia kuchunguza changamoto za kimataifa za leo hii  na kesho.

Programu ya Jukwaa hili 

Programu ya kudumu ya “Normandy kwa ajili ya amani” pia inaendelea kukuza nguzo kuu nne za utekelezaji: Chuo cha Amani cha Normandy, Normandy kwa ajili ya Mazungumzo, Normandy kwa ajili ya amani,  Utamaduni na Sayansi, na hatimaye Normandy kwa ajili ya amani ya rasiliamali

Roma: Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni akihutubia Baraza la Manaibu

Bi Giorgia Meloni Waziri Mkuu wa Italia  Alhmaisi tarehe 9 Aprili 2026 akihutubia Baraza la Manaibu alisema kuwa,  "Tunaendelea kuzungumzia mabadiliko ya uchumi, awamu ya pili, mabadiliko ya ikulu, miaka ya mwanga wa dunia mbali nasi. Hakuna nia ya kufanya mabadiliko, kwa sababu licha ya mapungufu yetu yote, hii inabaki kuwa serikali ambayo, licha ya kulazimika kusimamia hali mbaya zaidi ya kiuchumi katika miongo kadhaa, imerejesha utulivu wa kisiasa, uaminifu wa kimataifa, umakini katika usimamizi wa rasilimali, na misingi bora ya kiuchumi kwa Italia kuliko ile iliyokuwa nayo katika miaka iliyopita."

Ufalme wa Monaco.Kwa mara ya kwanza Ufalme utashikilia Unyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa UE(15 Mei-10 Novemba)

Ufalme wa Monaco unajiandaa kwa wakati wa kihistoria wenye umuhimu wa kimataifa: kuanzia Mei 15 hadi Novemba 10, 2026, utashikilia Uenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Baraza la Umoja wa Ulaya kwa mara ya kwanza, moja ya majukumu muhimu zaidi ya kisiasa ndani ya Shirika, ambalo linaunganisha nchi wanachama 46. Uenyekiti utachukuliwa rasmi mwishoni mwa kikao cha mawaziri kilichopangwa kufanyika Chisinau mnamo Mei 14 na 15, 2026, ikifuatiwa na sherehe ya makabidhiano huko Strasbourg mnamo Mei 20. Wakati wa muhula huu wa miezi sita, Isabelle Berro-Amadeï, Mshauri wa Serikali na Waziri wa Mahusiano ya Kigeni na Ushirikiano, ataongoza Kamati ya Mawaziri, huku Balozi Gabriel Revel akiratibu mikutano ya kila Juma ya wawakilishi wa kudumu huko Strasbourg.

Praga,Czech:Ziara ya Rais wa Italia Sergio Mattarella

Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella anatua katika Uwanja wa Ndege wa Praga kwa ziara yake rasmi katika Jamhuri ya Czech kuanzia (Aprili 9 na 10, 2026). Mkuu wa Nchi anasindikizana pamoja na wengine Mwanae Laura, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Edmondo Cirielli. Rais Mattarella atakutana na wafanyakazi wa Ubalozi na wawakilishi wa jumuiya ya Italia katika Taasisi ya Utamaduni ya Italia. Alasiri, atakaribishwa katika Ngome ya Praga na Rais wa Jamhuri ya Czech, Petr Pavel, na mkewe, Eva Pavlová. Baada ya sherehe ya kukaribisha na kuwasilisha ujumbe rasmi, wakuu hao wawili wa nchi watafanya mkutano, ukifuatiwa na mkutano na waandishi wa habari. Jioni, chakula cha mchana kitaandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Czech kwa heshima ya Rais Mattarella.

Siku ya Ijumaa, Aprili 10, Mattarella atakutana na Rais wa Baraza la Manaibu, Tomio Okamura, huko Palazzo Thun, na baadaye atakula chakula cha mchana na Rais wa Seneti, Miloš Vystrčil. Baadaye, atarudi Roma. Ziara zilizotanguliwa , ilikuwa mnamo tarehe 28 Novemba 2023, Rais Mattarella alimpokea Rais wa Jamhuri ya Czech, Petr Pavel, katika ziara rasmi nchini Italia, katika Jumba la Ikulu.

UNICEF na Benki ya Dunia warejesha matumaini ya elimu kwa watoto Sudan kupitia programu mbadala za kujifunza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao.

Katika jimbo la River Nile nchini Sudan inaoneshwa kwenye video ya UNICEF na Benki ya Dunia inaanza kwa kumuonesha mwanafunzi Hayat akiwa ndani ya darasa lililo kuukuu yeye na wanafunzi wenzake. Mwalimu anaendelea kufundisha na wote wanafurahi kuendelea na masomo yao. Wao ni miongoni mwa wanafunzi 9,500 wanaonufaika na Programu hizo za Elimu Mbadala kwani wamepata fursa ya kurejea katika masomo na kujenga upya ndoto zao.

Lebanon:Zaidi ya watu 250 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Lebanon

Watu 254 wamekufa na 1,165 wamejeruhiwa: hii ni idadi ya muda iliyochapishwa na Ulinzi wa Raia wa Lebanon kufuatia mashambulizi mengi ya anga ya wakati mmoja katika maeneo kadhaa ya Lebanon yaliyofanywa na Jeshi la Anga la Israeli jana, Aprili 8. Kulingana na Ulinzi wa Raia, majeruhi ni kama ifuatavyo: huko Beirut, 92 wamekufa, 742 wamejeruhiwa; vitongoji vya kusini mwa Beirut, 61 wamekufa, 200 wamejeruhiwa; Baalbek/Hermel (mashariki mwa Lebanon), 27 wamekufa, 34 wamejeruhiwa; Nabatieh, 28 wamekufa, 59 wamejeruhiwa; Sidon, 12 wamekufa, 56 wamejeruhiwa; Tyre, 17 wamekufa, 68 wamejeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Lebanon, Nawaf Salam ametangaza leo, Aprili 9, siku ya maombolezo ya kitaifa "kwa waathiriwa wa mashambulizi ya Israeli, huku utawala na taasisi za umma zikifungwa, pamoja na manispaa, bendera zikiwa nusu mlingoti, na programu za vyombo vya habari zikibadilishwa kulingana na janga hili la kitaifa." Mashambulizi hayo, ambayo mengi yaligusa moyo wa Beirut, yalisababisha hofu katika mji mkuu wa Lebanon wakati wa msongamano wa magari, hasa kwa vile hayakutanguliwa na onyo kwa raia kutafuta makazi, kama ilivyotokea katika matukio mengine.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

 

09 Aprili 2026, 11:27