Messori,mchunguzi mwenye shauku wa sababu za imani
Andrea Tornielli.
Moyo wake umezima usiku, nyumbani kwake Desenzano ya Garda, saa 3:45 usiku, katika siku ya Ijumaa Kuu, baada ya kumbukumbu ya Mateso ambayo alikuwa amechunguza kwa uaminifu mkubwa wa kiakili katika kitabu: "Wanasema Amefufuka." Amefariki, Vittorio Messori, mwandishi wa vitabu vilivyouzwa sana mamilioni ya nakala kuhusu iman na kuleta matokeo katika mazingira ya kiutamaduni ya Italia na Kimataifa, na alikuwa atimize miaka 85 katika siku chache zijazo. Miaka minne iliyopita, alipoteza mke wake mpendwa, Rosanna.
Alizaliwa huko Sassuolo, Emilia, katika familia isiyopenda dini, ikahamia katika eneo la Brescia na kisha ikahamia Torino mara tu baada ya vita. Katika chuo kikuu, Vittorio alisoma na Firpo na Bobbio na akahitimu kwa shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa kuhusu Galante Garrone, akiwa na tasnifu kuhusu 'Risorgimento', YAANI kipindi cha kufufuka.
Mwaka 1964, maisha yake, ambayo hadi wakati huo yalikuwa mbali na imani, yalibadilika sana, yakisaidiwa na usomaji wa Injili. Maandiko hayo muhimu, yaliyoandikwa karibu miaka elfu mbili iliyopita, yalimgusa moyo, yakimbadilisha, kuanzia wakati huo na kuendelea, kuwa mchunguzi asiyechoka wa sababu za imani. Alijiandikisha katika Taasisi ya (Christology) yaaani kuhusu Mafunzo ya Kristo katika “Pro Civitate Christiana” huko Assisi, ambapo alitumia mwaka mmoja akisoma na kukutana na mwanamke ambaye baadaye angekuwa mke wake. Baada ya kurudi Torino, alianza kufanya kazi katika Nyumba ya Kijamii ya Kimataifa ya Kuchapisha vitabu na kuchangia katika magazeti na majarida kadhaa. Mnamo 1970, alijiunga na Shirika la Habari za jioni 'Stampa Sera' na baadaye akawa mhariri wa nyongeza wa ‘Tuttolibri della Stampa.’
Mnamo 1976, insha yake ya kwanza muhimu ya “Nadharia kuhusu Yesu” ilichapishwa, matunda ya miaka kumi na miwili ya utafiti. Kitabu hiki kinachunguza historia ya Mnazareti, na kufanya maudhui yote yapatikane kwa kawaida kwa kundi finyu la wataalamu. Alikuwa, bila kukusudia au kupanga, mwanzilishi wa maombi mapya na ya kisasa ya uombaji msamaha, yaliyofanywa kwa ukali sana. Mwaka 1978, alihamia Milano ili kuzundua “ Jesus”, jarida jipya la kila mwezi kwenye duka la Paulines ambaye alifanya kazi katika uhariri wake kwa miaka michache na kisha akaendelea kushirikiana lakini kama mshirika wa nje. Mnamo 1982, alichapisha "Scommesse sulla morte," yaani (ahadi ya kushinda au kupoteza kuhusu kifo) akishutumu mgogoro wa Umaksi. Lakini ilikuwa historia ya Injili iliyomvutia zaidi: Kitabu hicho cha kwanza muhimu kuhusu Yesu kilifuatiwa na vingine vilivyopanga utafiti ambao angeendelea kujitolea kwa shauku katika maisha yake yote:"Inchiesta sul cristianesimo" -(yaani uchunguzi kuhusu Ukristo) (1987), safari ya mazungumzo na Wakristo, waamini wa dini zingine, wasioamini Mungu, na wakana Mungu; "Aliteseka Chini ya Pontio Pilato" (1992), "Wanasema Amefufuka" (2000), na " Nadharia kuhusu Maria" (2005).
Lakini kinakumbukwa hasa kwa namna ya pekee ya mwitikio wa ajabu hada baada ya kutolewa kwa kitabu kingine cha 'Ripoti kuhusu Imani," kilichoandikwa na Messori mwaka 1984 baada ya mazungumzo ya siku kadhaa na Kardinali Joseph Ratzinger wakati wa likizo yake katika Seminari ya Bressanone. Kitabu hiki kinawakilishwa kwa umma kwa ujumla mawazo ya Kardinali ambaye Papa Yohane Paulo II alikuwa amemteua kuongoza Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, miaka michache iliyokuwa imepita na kinaonya dhidi ya kuhama kutoka itikadi kwa mtazamo fulani wa maendeleo.
Akiwa mwandishi anayeheshimika sana na Mapapa na Mapapa wajao, mwaka 1994 aliombwa kumhoji Yohane Paulo II. Hii ilisababisha kuandika kitabu:"Kuvuka Kizingiti cha Matumaini," ambapo Papa alijibu maswali 35 yaliyoulizwa na Messori. Akawa mchangiaji wa Gazeti la ‘Corriere della Sera’ na akachaguliwa kutangaza, kupitia tahariri, uamuzi uliofanywa na Karol Wojtyla mwanzoni mwa miaka ya 2000: licha ya kuendelea kwa ugonjwa wake, hangekataa kuendelea na upapa.
Katika maisha yake yote, kutangaza imani na sababu za kuamini, hoja za uhalisia wa Injili, zilikuwa kitovu cha maslahi yake. Kwa sababu ya maisha yake kabla ya kuongoka kwake na kuweka kipaumbele kwake kerygma, hakuwahi kupendezwa sana na masuala ya maadili. “Bila msumari wa imani,” alipenda kurudia, “kifuniko cha maadili hakiwezi kusimama.” Kwa hivyo alikusudia kusisitiza kwamba katika muktadha wa leo wa kidunia, ilikuwa muhimu kwanza kutangaza kifo na ufufuko wa Kristo kwa kutoa ushuhuda wa kiini cha imani.
Msomi mkubwa wa maono na miujiza ya Lourdes, katika miaka ya hivi karibuni ibada yake ya Maria iliongezeka zaidi na alikuwa amejitolea juhudi kubwa, akiwekeza rasilimali zake binafsi katika uundaji wa Kanisa la Mama Yetu wa Mti wa Mizeituni katika bustani zinazozunguka Abasia ya Wabenediktini ya Maguzzano, karibu na Ziwa Garda, ambalo kwa sasa linakaliwa na Shirika la Watumishi Masikini wa Mungu Mpaji. Inashangaza kwamba mwandishi aliyetoa nguvu zake zote kujenga upya umbo la Yesu amehitimisha maisha yake siku ambayo waamini wa ulimwenguni kote wanakumbuka kifo cha Mnazareti pale Kalvari.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.