Tafuta

Kuongezea kwa vifo kutokana na mlipukoa wa Ebola huko Congo DR. Kuongezea kwa vifo kutokana na mlipukoa wa Ebola huko Congo DR. 

Congo,DR:Ebola imeshika kasi,wakati mamia elfu wakikimbia makazi yao kwa vurugu

Jitihada zinaendelea kuimarisha mwitikio wa huduma ya afya dhidi ya janga la Ebola huku kuzuka vurugu pia kukiwa sababu ya wasiwasi:mahema yanayotumika kuwatenga wagonjwa katika Hospitali ya Rwampara nje kidogo ya Bunia,yamechomwa moto.Vifo saba vimethibitishwa hadi sasa,lakini kuna visa 750 vilivyothibitishwa na vifo 177 vinavyoshukiwa.Dharura pia imetolewa nchini Uganda.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kukusanyika katika mikesha ya mazishi na mikusanyiko ya watu zaidi ya 50 bado imepigwa marufuku katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR kutokana na mlipuko wa Ebola ambapo kila kitu kinafanywa ili kujaribu kupunguza janga la Ebola linaloenea kwa kasi katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika, ambapo wafanyakazi wa afya wanapambana. Kwa ukosefu wa rasilimali na hali ya hewa inayozidi kuwa joto, pamoja na ripoti za mapigano na vurugu, katika nchi ambayo haijuhi amani kwa zaidi ya miaka thelathini na ambapo karibu watu milioni moja wameyakimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea wa silaha kuhusu rasilimali za madini za eneo hilo.

Wauguzi kujiandaa kupokea wagonjwa
Wauguzi kujiandaa kupokea wagonjwa   (AFP or licensors)

Shirika la Afya Duniani limetangaza dharura ya Ebola

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa mlipuko wa virusi vya Ebola vya Bundibugyo sasa unaleta hatari "kubwa sana" kwa nchi  ambayo kuna ongezeko kutoka kwa uainishaji wa awali wa "juu" - ingawa hatari ya ugonjwa kuenea duniani kote bado ni ndogo. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Bwana  Tedros Adhanom Ghebreyesus alitangaza kwamba visa 82 na vifo 7 vimethibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini mlipuko huo unaaminika kuwa "mkubwa zaidi." Kwa sasa hakuna chanjo inayopatikana kwa virusi vya Bundibugyo, ambavyo vilienea kwa majuma kadhaa katika jimbo la Ituri kabla ya kifo cha kwanza kuthibitishwa. Kwa sasa kuna visa 750 vinavyoshukiwa na vifo 177 vinavyoshukiwa. "Tunajaribu kuwafikia," alitangaza Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Thérèse Kayikwamba Wagner, huku Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu likitangaza kwamba angalau watatu kati ya watu wake wa kujitolea wamefariki kutokana na janga hilo huko Mongbwalu, huko Ituri.

Vituo vya upimaji wa Ebola
Vituo vya upimaji wa Ebola   (AFP or licensors)

Ghasia za mitaani

Kuzuka kwa ghasia za mitaani sasa pia ni sababu ya wasiwasi. Mnamo Mei 22, waandamanaji walichoma moto mahema yaliyotumika kuwatenga wagonjwa katika Hospitali ya Rwampara, nje kidogo ya mji mkuu Bunia, baada ya wanafamilia na marafiki wa kijana mmoja aliyefariki baada ya kugunduliwa na virusi hivyo kuzuiwa kuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi. Polisi waliingilia kati kwa kufyatua risasi za onyo katika jaribio la kurejesha udhibiti wa hali hiyo, huku mtangazaji wa eneo hilo akiripoti kwamba, kufuatia matukio ya vurugu, wagonjwa kadhaa waliokuwa na visa vinavyoshukiwa na kuthibitishwa vya Ebola walikimbia, na mfanyakazi wa afya alijeruhiwa katika machafuko hayo.

Kuchomwa kwa kituo cha wagonjwa wa Ebola
Kuchomwa kwa kituo cha wagonjwa wa Ebola

Maeneo yanayodhibitiwa na M23

Ugonjwa huo pia umeripotiwa katika majimbo mengine mawili, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo waasi wa M23, wanaoshutumiwa kuungwa mkono na Rwanda, wanadhibiti maeneo makubwa ya eneo, ikiwa ni pamoja na miji mikuu ya Goma na Bukavu. Wanamgambo wa M23 wenyewe wameripoti visa viwili, wakitangaza kuundwa kwa kikosi kazi cha kupambana na janga hili. Hata hivyo, mamlaka za kitaifa zimetoa tahadhari kwa sababu, kama Waziri Kayikwamba Wagner alivyoeleza, "M23 haijajiandaa kabisa" kukabiliana na janga la homa ya damu inayosababishwa na virusi. Katika dharura, mwitikio wa serikali pia unakabiliwa na upinzani kutoka kwa jamii za wenyeji, kutokana na taarifa potofu au taratibu za kimatibabu zinazoonekana kupingana na desturi za wenyeji. Shughuli za mazishi kwa wanaodaiwa kuwa waathiriwa zinasimamiwa, inapowezekana, na mamlaka, kwani miili hiyo inaweza kuambukiza sana.

Mlipuko nchini Uganda

Siku ya Ijumaa Mei 22, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa umetenga dola milioni 60 ili kuharakisha mwitikio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na eneo jirani. Marekani imeahidi dola milioni 23 kwa ufadhili wa shughuli za afya si tu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bali pia nchini Uganda, ambapo idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa imeongezeka hadi tano tangu wakati huo.

 

23 Mei 2026, 13:53