Tafuta

Yalilipuka mabomu huko Damasco wakati wa ziara ya Rais Macron. Yalilipuka mabomu huko Damasco wakati wa ziara ya Rais Macron.  (AFP or licensors)

Watu 18 wamejeruhiwa baada ya mabomu kulipuka katikati mwa Damasco

Jumanne tarehe 7 Julai 2026,baada ya mabomu mawili kulipuka katikati mwa Damasco karibu na hoteli mahali ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa akiishi,kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali,watu 18 walijeruhiwa.

Na Nathan Morley – Vatican.

Watu 18 walijeruhiwa Jumanne tarehe 7 Julai 2026, baada ya mabomu mawili kulipuka katikati mwa Damasco karibu na hoteli ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa akiishi, kwa mujibu wa  vyombo vya habari vya serikali. Vikosi vya usalama viligundua vifaa hivyo na vilijaribu kuwa  kutuliza mara tu yalipolipuka, maafisa walisema. Vilipuzi hivyo, kimoja  kilikuwa kimefichwa ndani ya gari lililoegeshwa na kingine kwenye pipa la takataka. Rais Macron, akiwa katika mji mkuu wa Siria kwa mazungumzo na Rais Ahmed al-Sharaa, hakujeruhiwa na wala  hakusikia milipuko hiyo, Ofisi ilisema.

Kusini mwa Lebanon, shambulio la ndege zisizo na rubani za Israeli kwenye gari liliwaua watu wanne, akiwemo Mwalimu Mkuu wa shule, kulingana na vyombo vya habari vya serikali vya Lebanon. Jeshi la Israeli lilisema gari hilo limeingia katika eneo la usalama lililozuiliwa na lilichukuliwa kuwa tishio. Lilikuwa shambulio baya zaidi la Israeli tangu tangazo la kusitisha mapigano mwezi uliopita. Wizara ya afya ya Lebanon ilisema takriban  watu 4,319 wameuawa katika mashambulizi ya Israeli tangu uadui uanze.

Unicef:Gaza

Wakati huo huo, UNICEF ilionya kwamba hali huko Gaza bado ni janga baada ya zaidi ya siku 1,000 za vita. Watoto huko "wameuawa, kulemazwa, kuhamishwa, na kunyimwa vitu muhimu wanavyohitaji ili kuweza kuishi, kukua, na kupona," Msemaji Louise Wateredge wa UNICEF alisema, akiongeza kuwa “zaidi ya watoto 60,000 wameuawa au kujeruhiwa.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

07 Julai 2026, 15:05