Tafuta

Watu nchini Venezuela wanaendelea kuteseka kwa sababu ya Tetemeko. Watu nchini Venezuela wanaendelea kuteseka kwa sababu ya Tetemeko.  (AFP or licensors)

Idadi ya vifo yaongezeka nchini Venezuela na mgogoro wa kibinadamu

Hali ngumu ya kiuchumu baada ya tetemeko kubwa ya ardhi nchini Venezuela yanasababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Na James Blears

Katikati ya majengo yaliyoanguka, familia bado zinasubiri habari za wapendwa wao, na jamii nzima zinazojaribu kujenga upya, wakati watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mara mbili lililoikumba Venezuela Jumatano, Juni 24. Nchi 28 ulimwenguni kote wametoa msaada wao wa michango, timu za wataalamu wa utafutaji na uokoaji, vifaa, na usimamizi wa maji na usafi wa mazingira, lakini hali ni mbaya sana.

Janga la Tetemeko nchini Venezuela

Tayari Venezuela ilikuwa imedhoofishwa sana na miaka ya vikwazo vikali vya kiuchumi vilivyoongozwa na Marekani janga la mitetemeko miwili ya ardhi mfululizo, lilizidisha hali mbaya ya maelfu ya watu, likizidi kubomoa miundombinu pamoja na maisha ya kila siku. Serikali ya Kaskazini mwa Guaira limeathiriwa sana. Uhaba mkubwa wa maji safi ya kunywa, chakula, vitu muhimu vya kila siku na dawa yamesababisha ongezeko la njaa, ugonjwa wa kuharisha na vipele vya ngozi.

UN yazindua wito wa kibindamu 

Matibabu ya moyo, shinikizo la damu na magonjwa ya kisukari yako katika shida kubwa. Umoja wa Mataifa (UN) umezindua wito wa kibinadamu ya mamilioni ya dola. Hata hivyo, itachukua mailioni ya pesa taslimu na miaka, kama si miongo kadhaa, kwa Venezuela kujikomboa kutoka katika miji ya mahema na kufanya makazi ya zamu kuwahifadhi watu wenye njaa.

TETEMEKO VENEZUELA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Julai 2026, 11:42