Tafuta

Huko Bosnia mauajia ya kimabari yalitokea 1995. Huko Bosnia mauajia ya kimabari yalitokea 1995.  (AFP or licensors)

Maelfu wafanya kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya halaiki ya Srebrenica

Maelfu ya watu walikusanyika karibu na Srebrenica tarehe 11 Julai 2026,kufanya kumbukizi ya miaka 31 ya ukatili mbaya zaidi barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Na Stefan J. Bos – Vatican

Zaidi ya wanaume na wavulana 8,000 Waislamu wa Bosnia waliuawa kimfumo kwa siku kadhaa mnamo Julai 1995 baada ya vikosi vya Waserbia wa Bosnia kuteka mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia wakati wa miezi ya mwisho ya vita vya Bosnia. Maafisaa wa uchunguzu walitumia miongo kadhaa kutafuta makaburi ya halaiki mahali hapo. Miili mingi baadaye ilifukuliwa na kuzikwa tena katika makaburi mengine katika jaribio la kuficha ushahidi wa uhalifu huo. Mabaki ya waathiriwa wa Srebrenica yalipatikana na kutambuliwa kupitia uchambuzi wa Vinasaba(DNA.) Waathiriwa wapya wanaliotambuliwa walizikwa

ambapo kila mwaka mnamo Julai 11, ukumbumbwa tarehe ambayo mauaji hayo yalianza mwaka 1995. Hata hivyo mwaka huu, mabaki ya waathiriwa 10 zaidi yalizikwa katika Kituo cha Ukumbusho cha Srebrenica katika kijiji cha karibu cha Potočari. Kabla hafla ya mazishi, jamaa na maelfu ya washiriki wengine walikamilisha Maandamano ya Amani ambayo hufanyika kila mwaka ya kwenda Potočari.

Maandamano ya amani

Maandamano hayo hufuata sehemu ya njia iliyotumiwa na wanaume na wavulana wa Bosnia ambao walijaribu kutoroka kupitia misitu baada ya Srebrenica kuanguka. Inaashiria njia ya uhuru kwa wale walionusurika na njia ya kifo kwa wale waliokamatwa na kuuawa. "Ni vigumu, na  vigumu sana," alisema Arnes Alić, ambaye baba yake alikuwa miongoni mwa waliouawa."Nimewaambia tu wenzangu kwamba ilinichukua muda kufanya uamuzi huu, kwa sababu hii ni mara ya kwanza na ya mwisho kukutana naye tangu alipokufa nilipokuwa na umri wa mwaka mmoja tu," aliongeza. Almir Baraković, muombolezaji mwingine, alisema maadhimisho hayo pia yalikuwa ya uchungu sana kwake. Alikuwa na umri wa miaka saba tu alipompoteza ndugu yake katika mauaji hayo. Watu zaidi ya 100,000 walikufa wakati wa Vita vya Bosnia vya miaka ya 1990 na kuwalazimisha mamilioni ya watu kuondoka makwao.

Licha ya maamuzi ya mahakama mbili za Umoja wa Mataifa, viongozi wa kisiasa katika eneo la Serbia nchini Bosnia na jirani Serbia wanaendelea kukataa kutajwa kwa mauaji ya halaika ya Srebrenica kama mauaji Kimbari. Maafisa wengi wa kisiasa na kijeshi wa Serbia nchini Bosnia wamehukumiwa na kwa mauaji ya kimbari uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

KUMBUKUMBU YA SREBRENICA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

11 Julai 2026, 11:04