Tafuta

Nelson Mandela, aliyekuwa Baba wa Taifa la Afrika Kusini. Nelson Mandela, aliyekuwa Baba wa Taifa la Afrika Kusini.  

Siku ya Mandela Kimataifa 2026:kujitolea na ujasiri wake katika kutetea uhuru na haki za binadamu!

"Siku ya Mandela ni hafla ya kila mwaka kimataifa,inayotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa,ya Julai 18 ili kuheshimu maisha na urithi wa Nelson Mandela.Siku hiyo ni wito wa kuchukua hatua kwa watu binafsi,jamii na mashirika kutafakari maadili na kanuni za Mandela na kuchukua hatua zenye maana ili kuleta matokeo chanya katika jamii zao.Katika fursa ya siku hii,Mfuko wa Nelson Mandela ulizindua Jukwaa huko New York,Marekani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya Mandela ni sherehe ya kila mwaka ya kimataifa, iliyotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa, ambapo maadhimisho hayo yalianzishwa mwaka  2009 kwa Azimio la Mkutano Mkuu A/RES/64/13, kwa kutambua mchango wa Mandela katika mapambano ya demokrasia na kukuza utamaduni wa amani duniani kote. Kwa njia hiyo hafla hiyo hufanyika kila ifikapo tarehe 18 Julai ili kuheshimu maisha na urithi wa Nelson Mandela. Pamoja na hayo tarehe hii ni Siku ya kuzaliwa kwake ambapo alizaliwa huko Mvezo katika kijiji kidogo kwenye Wilaya ya Mashariki,  katika mkoa wa Transkei nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai 1918. 

Siku hiyo ya mandela ni wito wa kuchukua hatua kwa watu binafsi, jamii na mashirika kutafakari maadili na kanuni za Mandela, na kuchukua hatua zenye maana ili kuleta matokeo chanya katika jamii zao.Kwa hakika Nelson Mandela, ni mtu ambaye maisha na maadili yake yamekuwa na yanaendelea kuwa chanzo cha msukumo kwa ulimwengu. Katika siku hii, jumuiya ya kimataifa inamkumbuka Rais wa zamani wa Afrika Kusini kwa kujitolea na ujasiri wake katika kutetea uhuru na haki za binadamu.

Ulimwengu uliojaa migawanyiko

Katika ulimwengu unaozidi kuwa na mgawanyiko ambapo ukosefu wa usawa unaendelea kukua na ambapo aina mpya za mgawanyiko, ushawishi na unyang'anyi zinaibuka. Mabadiliko ya tabia nchi, vita na migogoro vinasababisha kuhamishwa na umaskini wa jamii nyingi na hata jamii nzima. Haja ni kubwa kuliko hapo awali ya mipango inayokuza mshikamano, inayovuka tofauti na kukumbatia dhana ya ubinadamu wa pamoja. Bado iko mikononi mwako kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa. Wito wa kuchukua hatua ni mpana na unaojumuisha iwezekanavyo - tambua wale wanaohitaji karibu nawe na ufanye unachoweza kufanya ili kuleta mabadiliko nao na kwa ajili yao.

Uongozi unaotokana na ujasiri, mazungumzo na uwajibikaji

Ni katika muktadha huo ambapo wakati kuna  wanachama wa mfuko wa Mandela ambao umekuwa muhimu kwa urithi wa Nelson Mandela,   na sio uongozi kama nafasi ya mamlaka tu, lakini uongozi unaotokana na ujasiri, mazungumzo, uwajibikaji na huduma. Kwa njia hiyo Mwezi huu wa Mandela, Mfuko wa Nelson Mandela umezindua Jukwaa la Uongozi la Kimataifa la Nelson Mandela jijini New York, Marekani na kuunda jukwaa jipya la kimataifa la mazungumzo kuhusu changamoto za uongozi zinazounda ulimwengu wetu wa leo.

Kipindi cha ukosefu wa usawa na migogoro ya kivita

Katika kipindi cha ukosefu wa usawa unaoongezeka, migogoro, kupungua kwa imani katika taasisi za umma na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa, Jukwaa limewaleta pamoja viongozi, wafikiri na waleta mabadiliko ili kutafakari jinsi uongozi unaoongozwa na maadili unavyoonekana katika vitendo. Jukwaa la uzinduzi limemshirikisha Meya wa Jiji la New York, Zohran Kwame Mamdani kama Spika , akiendeleza utamaduni wa muda mrefu wa Mfuko wa kukusanya sauti zenye ushawishi ili kushiriki na baadhi ya maswali muhimu ya wakati wetu. Likiongozwa na imani ya Madiba katika nguvu ya mazungumzo, Jukwaa limelenga kuhimiza mazungumzo ya kweli, mawazo mapya na hatua za pamoja katika kutafuta ulimwengu wa haki na usawa zaidi. "Nimepigana dhidi ya utawala wa weupe na dhidi ya utawala wa weusi. Nimethamini wazo la jamii huru na ya kidemokrasia ambapo wote wanaweza kuishi pamoja kwa amani na fursa sawa. Ni wazo ambalo natumaini kuishi nalo na kulifikia. Lakini ikihitajika, ni wazo ambalo niko tayari kulifia." (Nelson Mandela.)

Kumbukumbu isiyofutika

Nelson Rolihlahla Mandela, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 1993, alikuwa mtu mweusi wa kwanza kushika wadhifa wa rais wa Afrika Kusini. Mnamo tarehe 10 Mei  1994, alijiwasilisha kwa ulimwengu kwa hotuba inayotaka ufufuko wa kisiasa na kijamii. Mandela alifanikiwa kukomesha utawala wa ubaguzi wa rangi baada ya mapambano ya upinzani kabla na wakati wa kifungo chake cha miaka 26. Na kunako mwaka 2015, "Kanuni za Nelson Mandela," ambazo hufafanua viwango vya kuwatendea wafungwa, zilipitishwa. Pia alihimiza kuanzishwa kwa mchakato wa upatanisho wa kitaifa unaotegemea utambuzi wa pande zote kati ya vipengele tofauti vya jamii ya Afrika Kusini. "Madiba" (jina alilopewa na kabila lake la Xhosa) alifariki mwaka 2013 jijini Johannesburg. Urithi wa Nelson Mandela unabaki kuwa marejeo muhimu kwa watu wake na ulimwengu mzima.

SIKU YA MANDELA KIMATAIFA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

18 Julai 2026, 12:59