Marekani itatoa Nishani ya Uhuru kwa Papa Leo XIV
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mnamo tarehe 3 Julai 2026, usiku wa kuamkia miaka 250 wa uhuru wa Marekani, watamtunuku Nishani ya Uhuru ya kila mwaka kwa Baba Mtakatifu, Papa Leo XIV ikiwa ni toleo la 38 kwa ajili ya kazi yake ya maisha yote katika kuhamasisha uhuru wa kidini na uhuru wa dhamiri na kujieleza ulimwenguni kote kama ilivyoainishwa na waanzilishi wa Marekani katika Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani. Haya yameelezwa na waandaaji wa hafla hiyo nchini Marekani.
Nishani ya Uhuru ya kila mwaka ya Kituo cha Katiba ya Kitaifa inawaheshimu wanaume na wanawake waliojipambanua kwa ujasiri na imani na wanaojitahidi kupata baraka za uhuru kwa watu ulimwenguni kote. Kutokana na taarifa kuhusu Joto kali la Jiji la Philadelphia kuanza Jumatano, na utabiri ulibainisha uwezekano mkubwa wa hali zisizo salama kwa programu za nje mnamo Julai 3, sherehe ya kutoa Nishani ya Uhuru itahamishiwa ndani ya Kituo cha Katiba ya Kitaifa.
https://constitutioncenter.org/about/liberty-medal
Huku taifa likisherehekea miaka 250, sherehe hiyo itawakutanisha viongozi wa kiraia na wa kidini, pamoja na wageni kutoka Philadelphia, kote nchini, na ulimwenguni kote, kutafakari jinsi ahadi ya kwamba watu binafsi wanaweza kuabudu kwa uhuru, kuzungumza waziwazi, na kuishi kulingana na imani zao wenyewe ambayo imeimarisha maisha ya kiraia nchini Marekani na kuhamasisha harakati za utu na uhuru wa binadamu ulimwenguni kote. Papa Leo XIV anatarajia kutoa hotuba za moja kwa moja kupitia vyombo vya Vatican, ambazo zitarushwa mbashara kwa wale wote watakaokuwa wamekusanyika kwenye ukumbi Mkuu na hadhira duniani kote. Zaidi ya hayo, sherehe itaanza saa 4:45 asubuhi, badala ya saa 11 asubuhi zaa za Marekani.
Ifuatayo ni orodha ya washiriki waliothibitishwa katika hafla hiyo
Baba Mtakatifu Leo XIV jwa njia ya Mtandao kupitia chanel za Vatican; Gavana Josh Shapiro, Commonwealth of Pennsylvania;
Meya Cherelle L. Parker, wa mji wa Philadelphia
Dave Sunday, Pennsylvania Mwanasheria Mkuu( Attorney General)
Vince Stango, Rais wa Muda na Mkurugenzi Mtendaji, Kituo cha Katiba cha Taifa
Askofu Mkuu Nelson J. Pérez, wa Jimbo Kuu la Philadelphia
Jill L. Maderer, Mkuu wa Kiyahudi, shirika la Rodeph Shalom
Imam Quaiser D. Abdullah, Ph.D., Ofisi ya Meya ya Ushiriki wa Waislamu
Carolyn C. Cavaness, Mama Bethel Kanisa la AME
Maonesho ya muziki kutoka Kwaya ya Kanisa Kuu la Basilika na Kwaya ya Jimbo Kuu la Philadelphia.
Roho ya Siku kuu ya Uhuru
Kuanzia Juni 4-6, 2026, Mfuko wa Kumbukumbu za Kitaifa umeandaa Tamasha la Roho ya Uhuru, tamasha la kuvutia la siku nyingi kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 250 ya Azimio la Uhuru. Likiwa limeandaliwa chini ya hema lenye ukubwa wa vitalu viwili vya jiji mbele ya Kumbukumbu za Kitaifa, tamasha hilo litajumuisha matukio ya mchana bila malipo kwa familia na matukio matatu ya jioni ya manufaa ili kuunga mkono Mfuko na juhudi zake za kuwashirikisha umma wa Marekani na historia ya taifa letu.
Vita ya Uhuru wa Marekani
Vita ya Uhuru wa Marekani ilipigwa kati ya Uingereza na walowezi wa makoloni yake 13 kwenye pwani ya Amerika ya Kaskazini katika miaka 1775 hadi 1783. Makaoloni haya yalikuwa: (Connecticut, Delaware, Georgia, Maryland, Massachusetts, New Hampshire, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, Rhode Island, South Carolina, Virginia) yaliyokaliwa na wahamiaji kutoka Uingereza wenyewe na nchi nyingine. Jeshi la walowezi lililoongozwa na George Washington na wengineo lilishinda jeshi la Dola la Uingereza kwa msaada wa Ufaransa. Hivyo hatimaye makoloni hayo yakapata uhuru kama "Muungano wa Madola ya Amerika" au Marekani.
Tarehe 4 Julai 1776 wawakilishi kutoka makoloni yote walitangaza uhuru wa Muungano wa Madola ya Amerika. Bado Waingereza walisonga mbele wakatwaa pia mji wa New York. Lakini tangu mwaka 1777 Ufaransa ulianza kwa siri kutuma silaha kwa Wamarekani; mwaka 1778 Ufaransa, Hispania na Uholanzi ziliungana na kutangaza vita dhidi ya Uingereza. Manowari za Ufaransa zilishambulia meli za Waingereza zilizopeleka silaha na askari kwenda Marekani. Mwaka 1781 sehemu kubwa ya jeshi la Uingereza ilishindwa kwenye mji wa Yorktown ikalazimika kujisalimisha. Tangu siku hiyo mapigano yalipungua na mwaka 1783 Uingereza ukakubali uhuru wa makoloni yake ya awali. Wakazi wengi wa makoloni walioendelea kusimama upande wa Uingereza walihamia Canada iliyobaki kuwa koloni.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.