Tafuta

Hali mbaya Gaza Hali mbaya Gaza  (DAWOUD ABU ALKAS)

UNICEF:Gaza yapambana na matatizo mengi ya kibinadamu

Mashirika ya kibinadamu yajaribu kuzuia kuenea kwa magonjwa huko Gaza huku kukiwa na msongamano mkubwa na kuzorota kwa hali ya afya ya umma.

Na Nathan Morley

Kusitishwa kwa mapigano huko Gaza kumekuwa "udanganyifu wa kikatili na hatari," msemaji wa UNICEF James Elder alisema hayo,  kwani takwimu za hivi karibuni zinaonesha zaidi ya watoto 250 wa Kipalestina wameuawa tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yalipotangazwa mnamo Oktoba 2025. Katika maoni yake ya hivi karibuni, Elder alisema kuwa mtoto mmoja uhuawa kila siku, huku wengine zaidi ya 400 wakijeruhiwa, wengi wakipata majeraha yanayaowaacha na makavu mabaya na kubadilisha maisha yao. Alisema watoto wanakufa katika maeneo ambayo wanapaswa kuwa salama, manyumbanu kwao, shuleni na katika makazi ya muda,  na alionya kwamba kuathiriwa mara kwa mara na vurugu kumewaacha wengi na kiwewe kikubwa cha kisaikolojia.

Hali ya kibinadamu huko Gaza ni mbaya

Wakati huo huo, hali ya kibinadamu kote Gaza, bado ni mbaya. Mashirika ya misaada yaliripoti uhaba mkubwa wa mafuta ya injini, magurudumu ya gari na vipuri, ambayo sasa inatishia shughuli za kuokoa maisha. Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilisema uzalishaji wa maji umepungua hadi takriban 40% ya viwango vya kabla ya Oktoba 2023 kutokana na ukosefu wa kemikali na vipuri. Zaidi ya 70% ya idadi ya watu wa Gaza sasa wanategemea maji ya kunywa yaliyosafirishwa na UNRWA na mashirika washirika. Kulingana na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), watoto milioni 1.1 wanakabiliwa na upatikanaji wa maji usio na uhakika kila siku.

Shirika la Mpango na wa Chakula Duniani limetoa wito wa dharura

Kwingineko, Umoja wa Mataifa uliwasaidia wakulima wanaojitahidi kujenga upya mashamba yao madogo katika maeneo yaliyoharibiwa na vita vya Hamas na Israeli. Umoja wa Mataifa ulionya kwamba wakulima "wanabanwa katika nafasi inayopungua kwa kasi" huku shughuli za kijeshi za Israeli zikiendelea. Katikati ya haya yote, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, limetoa wito wa dharura wa ufikiaji rahisi wa Gaza ili kuwafikia Wapalestina wengi zaidi kwa msaada muhimu. Kuna sehemu moja tu ya kuvuka iliyo wazi kuelekea eneo la Israeli huko Kerem Shalom, ambalo liko kusini kabisa mwa Ukanda.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

20 Julai 2026, 12:54