Askofu Mkuu wa Baltimore atoa wito wa kupyaishwa sera za kisiasa za Marekani
Na Jenny Kraska – Baltimore
Katika kuelekea maadhimisho ya makubwa ya kihistoria ya miaka 250 ya Azimi la Uhuru nchini Marekani, itakayoadhimishwa tarehe 4 Julai 2026, inahitaji mang’amuzi. Shukrani kwa baraka za taifa lazima zifanyike pamoja na utambuzi wa kweli wa migawanyiko inayounda maisha ya kiraia sio tu Amerika, bali katika demokrasia ulimwenguni kote. Haya yanaonekana katika barua ya kichungaj yenye kichwa: Upendo na Ukweli: Kuelekea mfumo mpyaisho wa utamaduni wa sera za kisiasa, iliyoandikwa na Askofu Mkuu Williamo Lori, wa Jimbo Kuu la Baltimore nchini Marekani, akiandika kwamba mgogoro wa kisiasa wa leo hii si wa kitaasisi tu ni wa kimaadili na kiroho. Ingawa sheria na miundo ni muhimu, haviwezi kuchukua nafasi ya wema. Unaanza na kurudi kwa Yesu Kristo. Askofu Mkuu alisisitiza kwamba maisha halisi ya kisiasa yanategemea kurejesha maono wazi ya mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu, aliyepewa hadhi isiyoweza kuvunjika, na kuitwa kuwajibika kwa wengine.
Sinodi zaidi ya miundo ya Kanisa
Mada ya barua ya kichungaji ya Askofu Mkuu ni Sinodi. Kwa njia hiyo ingawa mara nyingi hujadiliwa kwa maneno ya kikanisa, Askofu Mkuu anapendekeza roho yake ina mafunzo kwa ajili ya maisha ya umma pia. Kiini chake, Sinodi ni kuhusu kusikiliza kwa unyenyekevu, kuzungumza kwa uaminifu, kutambua kwa uvumilivu, na kutembea pamoja badala ya kujitenga katika vikundi, jambo amalo halikubaliki. Na kikinachokataliwa ni kugawanyika. Maisha ya ndani ya Kanisa hayawezi kuunganishwa tu na sera za kisiasa za kidunia. Hata hivyo tabia ambazo sinodi huendeleza ni usikivu, uvumilivu, uzito wa maadili, heshima kwa utu ni muhimu kwa jamii yoyote inayotarajia kuvumilia wingi bila kujitenga.
Kurejesha mawazo ya maadili
Katika Kiini cha barua hiyo kwa ajili ya wito wa kurejesha kile kinachoweza kuitwa mawazo ya maadili katika maisha ya kisiasa, Askofu Mkuu anabainisha kuwa hii si ujinga. Wala si kujitenga na imani. Mawazo ya kimaadili ni uwezo unaoundwa na wema, wa kufikiria maisha ya umma ambapo ujasiri hauwi uchokozi, haki haihitaji udhalilishaji, na ukweli hautenganishwi na upendo.
Upyaishaji kutoka miongoni mwetu
Utamaduni wa kisiasa huundwa na tabia za maadili za watu wa kawaida. Taasisi ni muhimu, lakini haziwezi kufidia upungufu wa wema. Mabadiliko yanayohitajika hayawezi kulazimishwa; lazima yapandishwe kupitia dhamiri, mshikamano, na kujitolea upya kwa kutembea pamoja licha ya kutokubaliana. Katika enzi inayojaribiwa na kujiondoa upande mmoja na utawala upande mwingine, kwa Upendo na Ukweli: Kuelekea mfumo mpya isho wa utamaduni wa sera za kisiasa,inapendekeza njia nyingine: siasa inayoongozwa na wema, inayoendelezwa na mawazo ya kimaadili, na iliyojengwa katika imani kwamba upendo na ukweli ni pamoja. Katika uwanja wa umma uliochoka, hilo linaweza kuwa pendekezo kubwa zaidi kuliko yote.
Kwa kifupi Azimio la Uhuru la Marekani ni hati ya kihistoria iliyoidhinishwa na Kongamano la pili la Bara la Amerika mnamo tarehe 4 Julai 1776, ambalo lilitangaza uamuzi wa makoloni kumi na tatu ya Marekani kujitenga na Uingereza. Ilikuwa ni hatua ya kutangaza rasmi kutengana kwa makoloni na utawala wa Uingereza na kuweka msingi wa kuanzishwa kwa Nchi za Umoja wa Marekani. Kwa nia hiyo tangazo hili linasherehekewa kama alama ya uhuru, demokrasia, na haki za binadamu, na misingi yake imeathiri harakati za uhuru na haki za raia Ulimwenguni kote.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here