Miaka 70 ya kuzaliwa kwa Papa:Asante wazazi na walionikumbuka katika sala
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 14 Septemba 14, Baba Mtakatifu alisema kuwa: Wapendwa kaka na dada, kesho (15 Septemba 2025) ni kumbu kumbu ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu, wazo la kinabii la Mtakatifu Paulo VI, ili Maaskofu waweze kufanya ushirika mkubwa na bora zaidi na Mrithi wa Petro.” Papa aliongeza: “Ninatumaini kwamba maadhimisho haya yatahamasisha kujitolea upya kwa umoja, sinodi, na utume wa Kanisa.”
Papa alitoa salamu zake za upendo kwa wote, waamini wa Roma na mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali, hasa wale wa Villa Alemana na Valparaíso, Chile, kutoka Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania, na Humpolec, Jamhuri ya Czech; Waperu wa Jumuiya ya Kidini ya Yesu wa Nazareti Cautivo. Kisha waamini wa Chiaiamari, Anitrella, Uboldo, Faeto, Lesmo, Trani, Faenza, Pistoia, Mtakatifu Martino huko Sergnano, Guardia ya Acireale, Mtakatifu Martino wa Ngazi huko Palermo, na Alghero.
![]()
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana (@VATICAN MEDIA)
Pia bendi za muziki za Borno na Sonico huko Val Camonica, Chama cha "La Nuova Famiglia" cha Monza, Kamati ya Pro Loco ya Mkoa wa Lazio, Umoja wa Utume wa Kikatoliki, vijana wa Don Bosco, na Jumuiya ya Chama cha Ukombozi cha Roma; pamoja na Chama cha Sanaa na Ufundi cha Mtakatifu Agata wa Militello, waendesha pikipiki kutoka Ravenna, na waendesha baiskeli kutoka Rovigo.
![]()
"Happy Birthday!" Kumtakia heri Papa Prevost kwa lugha ya kiingereza. (@VATICAN MEDIA)
Papa ameshukuru kupewa heri za kuzaliwa kwake
Wapendwa, inaonekana mnajua kuwa leo ninatimiza miaka sabini. Ninamshukuru Bwana na wazazi wangu; na ninawashukuru wale ambao wamenikumbuka katika maombi yao. Asanteni nyote sana! Asante! Dominika Njema. Ikumbukwe Papa Leo XIV alizaliwa huko Chicago, Illinois, tarehe 14 Septemba 1955. Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kila watu walionesha Mabango mengi yenye matakwa mema katika kila lugha na kutoka ulimwenguni kote.
![]()
Matashi mema kwa lugha ya kihispania (@VATICAN MEDIA)
