Tafuta

2025.10.24 Papa alikutana na Wakuu wa Shirika la Yesu mjini Vatican katika fursa ya Mkutano wao. 2025.10.24 Papa alikutana na Wakuu wa Shirika la Yesu mjini Vatican katika fursa ya Mkutano wao.  (@Vatican Media)

Leo XIV kwa Wajesuit:Jumuiya isoma ishara za nyakati&utambuzi katika utume

Papa alikutana na wakuu wa Jumuiya ya Yesu na kuwatia moyo,kwa roho ya Mtakatifu Ignatius,kutambua na kuvumbua katika ulimwengu uliogawanyika kuwa lazima wawe wataalamu wa upatanisho.Wafikie mipaka yote ya mbali na kiroho.Ni muhimu kuzungumza lugha ya vijana,kuwalinda maskini kutokana na ukiukwaji mwingi wa hadhi yao na kuhamasisha maadili katika akili unde,huku wakipinga miungu ya uwongo wa matumizi hovyo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV  alitoa Hotuba yake alasiri, tarehe 24 Oktoba 2025 kwa wakuu wa Shirika la Kijesuit, zaidi ya mia moja aliokutana nao katika Ukumbi wa Sinodi, wakiongozwa na Mkuu wa Shirika hilo, Padre Arturo Sosa. Hotuba hiyo ndefu ilikuwa mada mbali mbali ambapo Papa alianza kumshukuru  Mkuu wa Shirika hilo  na kuhimiza Jumuiya kutambua njia mpya za kuishi kulingana na utume wako katika ulimwengu wa leo. Mkutano wa Wakuu wa Shirika hilo ulianza  tangu 2005 ambao unawaleta pamoja takriban Wajesuiti 100 kutoka ulimwenguni, wakiwemo Wakuu kanda , na marais wa Baraza . Mkutano huo wa siku kumi, ulioanza tarehe 17 Oktoba 2025, unajumuisha nyakati za kutafakari, utambuzi wa pamoja, na hija ya Jubilei kupitia Mlango Mtakatifu.

Mkuu wa Shirika la Yesu wa Sasa akiwa na Papa mbele ya wanashirika
Mkuu wa Shirika la Yesu wa Sasa akiwa na Papa mbele ya wanashirika   (@Vatican Media)

Katika hotuba yake pana, Papa Leo XIV alielezea wakati uliopo kama mabadiliko ya enzi yaliyooneshwa na mabadiliko ya haraka katika utamaduni, teknolojia, na siasa. “Akili Unde(AI) na uvumbuzi mwingine unabadilisha uelewa wetu wa kazi na mahusiano, na hata kuibua maswali kuhusu utambulisho wa binadamu," alisema, akibainisha pia vitisho vya uharibifu wa ikolojia, ukosefu wa usawa, na mgawanyiko. “Lakini katika ulimwengu huu, Kristo bado anawatuma wanafunzi wake," alifafanua huku, akikumbuka jinsi Mtakatifu Ignatius wa Loyola na wenzake  ambao hawakuogopa kutokuwa na uhakika au ugumu; walikwenda pembezoni, ambapo imani na sababu ziliingiliana na tamaduni mpya na changamoto kubwa.

Hotuba ya Papa kwa Shirika la Yesu
Hotuba ya Papa kwa Shirika la Yesu   (@Vatican Media)

Akinukuu hotuba ya Mtakatifu Paulo VI ya mnamo 1974 kwa Wajesuit, Papa alirudia: kusema kuwa "Popote Kanisani, hata katika nyanja ngumu na kali zaidi ... Kumekuwa  na...  na kuna, Wajesuiti." Na kwa hiyo Papa aliendelea kusema kuwa “Narudia: Kanisa linawahitaji kwenye mipaka, iwe ni ya kijiografia, kiutamaduni, kiakili au kiroho. Hizi ni sehemu za hatari, ambapo ramani zinazojulikana na hazitoshi tena." Papa aliwaalika Wajesuit kutambua kwa ujasiri na kutekeleza kanuni ya Mtakatifu Ignatius ya kujali utakatifu kama utayari wa kuachana na miundo au majukumu yanayothaminiwa nje, wakati Roho inapoongoza mwili wa kitume mahali pengine kwa manufaa zaidi."

Wanashirika wa Yesu wakikutana na Papa Leo
Wanashirika wa Yesu wakikutana na Papa Leo   (@Vatican Media)

Miongoni mwa mipaka mikubwa inayolikabili Kanisa leo hii, Papa Leo XIV aliakisi njia ya sinodi, akiiita safari inayohitaji kumsikiliza Roho Mtakatifu kwa undani zaidi na kwa kila mmoja. Aliishukuru Jumuiya kwa michango yake katika mchakato wa sinodi na kwa kusaidia jumuiya za Kanisa kutembea pamoja kwa matumaini. Akigeukia mada ya upatanisho, alisema dunia inaendelea kuteseka kutokana na migogoro, ukosefu wa usawa na unyanyasaji, na kwamba majeraha mengi yanaendelea kutopona katika vizazi na watu. Lazima tupinge utandawazi wa ukosefu wa nguvu kwa utamaduni wa upatanisho, na  kukutana katika ukweli, msamaha na uponyaji Papa alisisitiza akiwahimiza Wajesuit kuwa wataalamu wa upatanisho, wakiwa na uhakika kwamba mema yana nguvu kuliko uovu.

Papa Leo XIV alijikita na sehemu ya hotuba yake katika changamoto za kimaadili zinazotokana na teknolojia mpya, hasa akili  Unde (AI). Aliita hii ni vizingiti  muhimu, akibainisha kwamba kuwa ingawa ina uwezo mkubwa, pia ina hatari za kutengwa, kupoteza kazi na aina mpya za udanganyifu. Kwa hiyo "Kanisa lazima lisaidie kuongoza maendeleo haya kimaadili, kutetea hadhi ya  binadamu na kukuza manufaa ya wote. Tunahitaji kutambua jinsi ya kutumia majukwaa ya kidijitali kuinjilisha, kuunda jumuiya na kutoa changamoto kwa miungu ya uongo, nguvu na kujitosheleza."

Papa alikutana na wakuu wa Shirika la Yesu
Papa alikutana na wakuu wa Shirika la Yesu   (@Vatican Media)

Ukitaka kusoma hotuba nzima ya Papa bonyeza hapa:READ POPE LEO'S FULL DISCOURSE HERE

Mapandeleo 4 ya Utume wa Kijesuit Ulimwenguni

Baba Mtakatfu Leo XIV akijikita kuzungumzia Mapendeleo manne ya Kitume  Ulimwenguni ya Shirika la Yesu(Jesuit), yaliyothibitishwa mnamo mwaka  2019 na Mtangulizi wake, Papa Francisko,  aliyaelezea kama “mipaka inayohitaji utambuzi na ujasiri." Akikumbuka Upendeleo wa kwanza, aliwahimiza Wajesuit kuwaongoza watu kwa Mungu kupitia Mafungo  ya Kiroho na utambuzi, huku  akibainisha kwamba wengi leo hii wanatafuta maana, mara nyingi bila kutambua. Akimtaja Mtakatifu Agostino, asemaye: "Umetuumba kwa ajili yako mwenyewe, Ee Bwana, na mioyo yetu haina utulivu hadi itulie ndani yako”, aliwataka Wajesuiti wakutane  na watu katika hali hiyo ya kutotulia ... katika nyumba za mapumziko, vyuo vikuu, mitandao ya kijamii, parokia na maeneo yasiyo rasmi ambapo watafutaji hukusanyika, na kubaki"watafakari katika vitendo, wenye mizizi katika urafiki wa kila siku na Kristo."

Pendekezo la Pili  kutembea na maskini na waliotengwa

Papa Leo XIV akizungumzia Upendeleo wa pili wa  kutembea na maskini na waliotengwa - alilaani "mfumo wa kiuchumi unaoendeshwa na faida zaidi ya hadhi ya mtu," akinukuu Wosia wake wa hivi Karibuni wa Dilexi Te, ambapo alionya dhidi ya udikteta wa uchumi unaoua. “Ukosefu huu wa usawa wa kimataifa unawasukuma watu wengi kuhama wakitafuta kuishi. Ufuasi wa kweli unahitaji kukemea dhuluma na pendekezo la mifumo mipya inayotokana na mshikamano na manufaa ya wote,” alisema. Kwa njia hiyo  Papa Leo XIV alihimiza “taasisi za ya KiJesuit,  ikiwa ni pamoja na Vyuo vikuu, vituo vya kijamii, machapisho, na Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit, kuhamasisha na kukuza mabadiliko ya kimfumo na kupinga uchovu wa huruma au imani ya hatima, badala yake wakiamini nguvu ya mabadiliko ya upendo wa Mungu.”

Pendeleo la 3 la kusinidikiza vijana

Akigeukia Upendeleo wa tatu, kuhusu kusindikiza vijana, Papa Leo XIV alisema kwamba “vijana wanashiriki kiu ya uhalisi na mabadiliko na kwamba Kanisa lazima lipate na kuzungumza lugha yao. Ni muhimu kuunda nafasi ambapo wanaweza kukutana na Kristo, kugundua wito wao, na kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme, alisema, akibainisha kuwa Siku ya Vijana Duniani ijayo nchini Korea(WYD2027) itakuwa wakati muhimu kwa utume huo.”

Papa akitoa hotuba yake
Papa akitoa hotuba yake   (@Vatican Media)

Upendeleo wa 4: Utunzaji wa Nyumba yetu ya pamoja

Kuhusu Upendeleo wa nne wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, Papa Leo XIV  alielezea ubadilishaji wa ikolojia kama wa kiroho sana, huku  ukitaka kupyaishwa  uhusiano wetu na Mungu, sisi kwa sisi na kazi ya uumbaji. Jamii zenu ziwe mifano ya uendelevu wa ikolojia, unyenyekevu na shukrani kwa zawadi za Mungu,” alisisitiza Baba Mtakatifu huku  akirudia kutazama Waraka wa Laudato Si' wa Papa Francisko  na wito wake wa ikolojia fungamani.

Sala, Sakramenti, na maisha ya kijumuiya

Kwa kuhitimisha hotuba yake, Papa Leo XIV aliwaalika Wajesuit kubaki karibu na Yesu kupitia sala, Sakramenti, na maisha ya kijumuiya. “Kutokana na mizizi hii, mtakuwa na ujasiri wa kutembea popote: kusema ukweli, kupatanisha, kuponya, kufanya kazi kwa ajili ya haki, kuwaweka huru mateka. Hakuna mpaka utakaokuwa nje ya uwezo wenu ikiwa mtatembea na Kristo,"aliwashauri. Papa alielezea matumaini yake kwamba “Jumuiya ya Yesu inaweza kuendelea kusoma ishara za nyakati kwa kina cha kiroho,"kukumbatia kile kinachohamasisha heshima ya mwanadamu na kubaki wenye bidii, wabunifu, wenye utambuzi na daima katika utume. Bwana na awaongoze kwenye mipaka ya leo hii  na zaidi, na kupyaisha Kanisa na kujenga Ufalme wa haki, upendo na ukweli.”

Papa na Wajesuit
24 Oktoba 2025, 17:30