Papa Leo XIV:Miaka 2 ya uchungu tangu Oktoba 7.Kupunguza chuki,kurudi kwenye mazungumzo
Na Daniele Piccini – Castel Gandolfo.
Hii imekuwa miaka miwili yenye uchungu sana. Miaka miwili iliyopita, watu 1,200 walikufa katika shambulio hili la kigaidi. Ni lazima tufikirie ni kwa kiasi gani chuki iko duniani na kuanza kujiuliza nini tunaweza kufanya. Katika miaka miwili, takriban Wapalestina 67,000 wameuawa. Lazima tupunguze chuki; lazima turudi kwenye uwezo wa mazungumzo, kutafuta suluhisho za amani.” Yamesema ba Baba Mtakatifu Leo XIV alasiri tarehe 7 Oktoba 2025 kwa waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri kwenye lango la Villa Barberini huko Castel Gandolfo, akimaanisha kumbukumbu ya shambulio la kigaidi la Hamas ambalo, hasa miaka miwili iliyopita, lilisababisha vifo vya zaidi ya Waisraeli elfu moja, utekaji nyara wa watu wasiopungua 250, na, baadaye, majibu makubwa ya Jeshi la Ulinzi la Gaza.
Hapana kwa ugaidi na chuki dhidi ya Wayahudi
Papa alilaani ugaidi na matukio ya hivi karibuni ya chuki dhidi ya Wayahudi, akithibitisha tena ujumbe wa Injili wa amani. "Ni hakika,” Papa alisema dakika chache kabla ya kurejea Vatican, ambako aliratibiwa kukutana na waamini wa Croatia saa 11:30 jioni masaa ya Ulaya “kwamba hatuwezi kukubali makundi yanayosababisha ugaidi; ni lazima kila mara tukatae aina hii ya chuki duniani. Wakati huo huo, kuwepo kwa chuki dhidi ya Wayahudi, iwe juu au la, ni wasiwasi. Daima tunapaswa kutangaza amani na heshima kwa utu wa watu wote. Huu ni ujumbe wa Kanisa."
Mahojiano ya Kardinali Parolin
Baadaye Papa Leo XIV alijibu swali kuhusu Ubalozi wa Israel katika majibu ya Vatican ambapo Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akihojiana na vyombo vya habari vya Vatican, ambaye, kwa mujibu wa taarifa, inadhoofisha juhudi za amani. "Kadinali alielezea maoni ya Vatican vizuri sana katika suala hili," Papa alisisitiza.
Nguvu ya Maombi yasiyokoma
Kisha Papa aliwaalika waamini wote kuendelea kuombea kukomesha mgogoro huu wa umwagaji damu na akahakikishia dhamira ya Kanisa katika kuendeleza mazungumzo na upatanisho. "Kanisa," Askofu wa Roma aliendelea, "limeomba kila mtu kuombea amani, hasa katika mwezi huu. Pia tutatafuta, kwa njia zilizopo kwa Kanisa, kuendeleza mazungumzo daima
Ziara ya Uturuki
Katika siku ya kutangazwa rasmi kwa ziara yake ya kwanza ya kitume, ambayo itamwona akisafiri hadi Uturuki na Lebanon kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 2, Papa Leo XIV, aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu sababu za safari hiyo katika eneo nyeti na lenye hali ya kisiasa la kijiografia, alieleza: "Safari ya Uturuki imechochewa na kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea. Kwa Wakristo wote, itakuwa ni wakati wa umoja wa kweli katika imani.
Ujumbe wa Amani kwa Lebanon
Pamoja na ziara yake ya Lebanon, Papa anakusudia zaidi ya yote kupeleka faraja kwa watu ambao mateso yao yameongezeka tangu mlipuko katika bandari ya Beirut mnamo Agosti 4, 2020. "Nchini Lebanon," alisema, "nitapata fursa ya kutangaza tena ujumbe wa amani katika Mashariki ya Kati, katika nchi ambayo imeteseka sana. Papa Francisko pia alitaka kuwapa watu wa Lebanoni hilo, baada ya yote wameteseka tutajaribu kupeleka ujumbe huu wa amani na matumaini."
Asante sana kusoma makala hii. Ikiwa unataka kubaki umesasishwa tunakualika kubonyeza cliccando qui.
