Katekesi Papa Leo XIV:Kutumaini ni kuwa na msimamo:Dorothy Day
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV katika mwendelezo wa Katekesi za Jubilei, Jumamamisi tarehe 22 Novemba 2025 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ambapo kabla ya kuanza tafakakari alizungukia uwanja na kuwasalimu huku akiwakumbatia na kuwabariki watoto wadogo. Papa aliongozwa na mada ya “Kutumiani ni kuwa na msimamo.” Dorothy Day.” Hii ni sura nyingine ya mwanaharakati wa Marekani aliyebadilisha maisha yake baada ya kukutana na Ukatoliki, huku akijitolea kikamilifu kwa waliotengwa mwanzoni mwa karne ya ishirini na kuwa bingwa wa upatanisho. "Dorothy Day aliandika kama mwandishi wa habari; alifikiri na kuwafanya wengine wafikiri. Uandishi ni muhimu. Na ndivyo ilivyo kwa leo hii kusoma, zaidi ya hapo awali. Kisha Dorothy Day alihudumia milo, alitoa nguo, akavaa na kula kama wale aliowahudumia: aliunganisha akili, moyo na mikono." Kwa njia hiyo ilisomwa Injili kwa lugha mbali mbali:
"Kwa kila mtu aliyepewa vingi, vingi vitahitajika; na kwa yule aliyekabidhiwa vingi, zaidi vitahitajika. Nimekuja kuleta moto duniani, na laiti ungekuwa tayari umewashwa! Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina huzuni sana hadi ukamilike!(Lc 12,48-50.)
Papa Leo alianza kuwasalimia na kusema kuwa “Kwa wengi wenu, kuwa Roma leo ni utimilifu wa hamu kubwa. Kwa wale walio kwenye hija na kufikia mwisho wao, ni muhimu kukumbuka wakati wa kufanya uamuzi. Kuna kitu, mwanzoni, kilihamia ndani yenu, labda kutokana na neno au mwaliko wa mtu mwingine. Hivyo, Bwana mwenyewe alitushika mkono: shauku na kisha uamuzi. Bila hili, usingekuwa hapa. Ni muhimu kukumbuka hili.
Papa alisema kwamba "Na kile tulichosikia muda mfupi uliopita kutoka kwa Injili pia ni muhimu: "Yeyote aliyepewa mengi, mengi yatahitajika; ambaye amekabidhiwa mengi, mengi zaidi yataombwa." Yesu anasema hivi kwa wanafunzi wake wa karibu, kwa wale waliokuwa karibu naye. Na sisi pia tumepokea mengi kutokana na safari tuliyofanya hadi sasa; tumekuwa pamoja na Yesu na Kanisa, na ingawa Kanisa ni jumuiya yenye mapungufu ya kibinadamu, tumepokea mengi. Kwa hivyo, Yesu anatarajia mengi kutoka kwetu. Ni ishara ya uaminifu, ishara ya urafiki. Anatarajia mengi kwa sababu anatujua na anajua tunaweza kuyafanya!
Papa alikazia kusema kuwa "Yesu alikuja kuleta moto: moto wa upendo wa Mungu duniani na moto wa hamu ya mioyoni mwetu. Kwa namna fulani, Yesu anaondoa amani yetu ikiwa tunaiona amani kama utulivu usio na kitu. Hata hivyo, hii si amani ya kweli. Wakati mwingine tunatamani "tungeachwa peke yetu": kwamba hakuna mtu anayetusumbua, kwamba wengine hawapo tena. Sio amani ya Mungu. Amani ambayo Yesu analeta ni kama moto na inatutaka mengi. Zaidi ya yote, inatuomba tuwe na msimamo. Katika hali ya ukosefu wa haki, ukosefu wa usawa, ambapo heshima ya binadamu inakanyagwa, ambapo walio dhaifu wananyimwa uwezo wa kusema: kuwa na msimamo. Kutumaini ni kuwa msimamo. Kutumaini ni kuelewa moyoni na kuonesha kwa vitendo kwamba mambo hayapaswi kuendelea kama hapo awali. Huu pia ni moto mzuri wa Injili."
Sura ya Dorothy Day
Papa Leo kwa njia hiyo alisema kwamba alitaka kumkumbuka mwanamke mdogo, mkubwa wa Marekani, Dorothy Day, aliyeishi katika karne iliyopita. Alikuwa na moto ndani. Dorothy Day alichukua msimamo. Aliona kwamba mfumo wa maendeleo wa nchi yake haukuunda fursa sawa kwa kila mtu. Alielewa kwamba kwa wengi sana, ndoto hiyo ilikuwa ndoto mbaya. Kama Mkristo, ilibidi ashirikiane na wafanyakazi, wahamiaji, na wale waliokataliwa na uchumi unaoua. Aliandika na kutumikia: ni muhimu kuunganisha akili, moyo, na mikono.
Hii ni kuwa na msimamo. Aliandika kama mwandishi wa habari; yaani, alifikiri na kuwafanya wengine wafikiri. Uandishi ni muhimu. Na ndivyo ilivyo kwa leo hii kusoma, zaidi ya hapo awali. Na kisha Dorothy alihudumia milo, alitoa nguo, akavaa na kula kama wale aliowahudumia: aliunganisha akili, moyo, na mikono. Kwa njia hiyo, kutumaini ni kuwa na msimamo. Dorothy Day alihusisha maelfu ya watu.
Papa alisisitiza juu ya sura hii ya mwanaharakati wa upendo kuwa "Alifungua nyumba katika miji mingi, katika vitongoji vingi: sio vituo vikubwa vya huduma, lakini vituo vya upendo na haki ambapo wangeweza kuitana kwa majina, kufahamiana mmoja baada ya mwingine, na kubadilisha hasira kuwa ushirika na vitendo." Hivi ndivyo wapatanishi walivyo yaani wanakuwa na msimamo na kubeba matokeo, lakini wanaendelea mbele. Kutumaini kunamaanisha kuwa na msimamo, kama Yesu, pamoja na Yesu. Moto wake ni moto wetu. kwa kuhitimisha Papa alisema "Jubilei na iwashe tena ndani yetu na katika Kanisa lote!"
