Tafuta

Papa amemteua katibu Msaidizi wa Baraz ala Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu Papa amemteua katibu Msaidizi wa Baraz ala Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu 

Papa amteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu

Jumatatu tarehe 24 Novemba 2025,Papa Leo XIV amemteua Katibu Msaizidi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu,Monsi Jozef Barlaš, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican.

Vatican News

Jumatatu tarehe 24 Novemba 2025, Baba Mtakatifu amemteua Katibu Msaizidi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamanai ya Binadamu, Monsi Jozef Barlaš, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican.

Wasifu wake

Mons. Barlaš alizaliwa tarehe 7 Mei 1985 huko  Snina (Slovakia). Alipewa daraja la upadre kwa ajili ya  Jimbo Kuu la Košice mnamo tarehe 19 Juni 2010. Alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran mnamo 2022.

Tangu tarehe 1 Oktoba 2020, amekuwa Afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican. Aliteuliwa kuwa Padre wa Kikanisa cha Baba Mtakatifu mnamo mwaka huu 2025. Mbali na Kislovakia, anazungumza Kiitaliano, Kiingereza, na Kihispania.

Katibu Msaidizi Maendeleo
24 Novemba 2025, 12:40