Papa atembelea wamonaki wa kiagostinian:"ni mtu mwenye utulivu"
Na Tiziana Campisi – Vatican.
Baada ya kukutana na Maaskofu wa Italia huko Assisi, Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 20Novemba 2025 alitembelea Jumuiya ya watawa wa Monasteri ya Kiagostinian, ya Mtakatifu Clara huko Montefalco kwa ziara ya kibinafsi. Monasteri hiyo inajulikana kwa kuhifadhi kumbukumbu ya Mtakatifu Clara, inayojulikana kama Conventi ya Msalaba. Papa alitumia muda wake kukaa na watawa, kisha akaadhimisha ibada ya Misa na hatimaye akala chakula cha mchana nao. Hata hivyo Papa aliwahi kwenda huko kama Padre, kisha katika matukio mengine akiwa Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino, na kwa njia hiyo amerudia akiwa kama Baba Mtakatifu wa 267 wa Kanisa la Ulimwengu.
Kwa hiyo ziara hii ilikuwa ni wakati wa ushirika na watawa wa familia ya Kiagostinian waliovalia sare, ambao Papa Leo XIV alichagua kama kituo cha pili katika ziara yake fupi ya Umbria, baada ya kwenda Assisi kukutana na Baraza la Maaskofu Italia(CEI), ambao walihitimisha Mkutano wao Mkuu wa 81.
Kwa upande wa Mkuu wa Monasteri Sr Maria Cristina Daguati alitoa maoni kwa vyombo vya habari vya Vatican kuwa, "Wakati wa kufahamiana zaidi na mtu tunayemjua kwa miaka mingi. Papa Leo XIV ameleta mazingira mazuri ya maombi. Kwa hivyo sio kwamba alitusumbua sana, ilikuwa vizuri sana. Nzuri... "Ni urafiki mzuri, kwa sababu ni wazi tumemjua kwa miaka mingi, na kwa hivyo ningesema kila kitu kilijitokeza katika roho ya kufahamiana sana," aliongeza Sr Daguati "siku rahisi sana" na "mtu mwenye "utulivu."
Makabirisho huko Montefalco
Papa Leo XIV hata hivyo aliondoka huko Assisi yapata saa 4:00 asubuhi masaa ya Ulaya. Alikuwa amefika kwa helikopta yapata saa 2:30 asubuhi kutoka mjini Vatican katika Uwanja wa Migaghelli, kisha aakaenda katika Basilika ya Mtakatifu Francis na akakaa kimya kwa maombi mbele ya kaburi la Mtakatifu Francis. Baada ya hapo alihamia katika Basilika ya Mtakatifu Maria wa Malaika (Maria degli Angeli,) ambapo alizungumza na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), kabla ya kwenda na helikopta huko Montefalco.
Katika mji huu mdogo katika jimbo la Perugia, kulikuwa na msisimko mkubwa kuhusu kuwasili kwa Papa Leo XIV, Papa wa kwanza kutembelea maeneo hayo. Meya wa mji Alfredo Gentili na Naibu Meya Daniele Morici walimkaribisha kwenye uwanja wa michezo.
Watu wengi walikusanyika kando ya mitaa ya kale kati kumlaki. Watoto kadhaa walimsubiri kwa furaha karibu na monasteri, na Papa aliwapungia mkono kutoka kwenye gari lake kabla ya kuingia katika monasteri ya kale ya Mtakatifu Clara ambayo asili yake inaanzia katika karne ya 13.
![]()
Baada ya kufika Papa huko Montefalco (@Vatican Media)
Jumuiya ya Wamonaki na watawa wa Mtakatifu Clara wa Montefalco
Katika jumuiya ya watawa ambayo inafuata Kanuni ya Mtakatifu Agostino tangu tarehe 20 Juni 1290, na ambayo leo hii ina watawa 13, ushuhuda wa Clara wa Montefalco unaendelea. Huyu ni Mtawa wa Kiitaliano aliyezaliwa mwaka 1268 na kufariki mwaka 1308. Sura yake inahusishwa na Montefalco ambapo pia ni kijiji cha Umbria kinachojulikana kwa mandhari yake, harufu, na ladha, na pia kwa uzalishaji wake wa divai, kama vile 'Sagrantino di Montefalco.' Alikuwa mtawa aliyetangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1881 na Papa Leo XIII.
Katika maisha yake alikuwa na umri wa miaka sita alipoonesha hamu ya kujitoa kwa Mungu na kufanya toba, kama dada yake Giovanna akiwa na umri wa miaka sita. Akiwa aliyachiliwa akiwa na umri wa miaka ishirini na mitatu tu, alitoa msukumo mpya kwa Jumuiya ya Kitawa, akipanga maisha ya pamoja vizuri zaidi, akiwataka masista wote kufanya kazi za mikono, lakini akiwapa uhuru wa kutosha wale waliopenda zaidi kusali. Alijitambulisha kama mwanamke mwenye uthabiti ulioelimika. Watu wengi maskini na wenye uhitaji walimkaribia, na Clara alikuwa tayari kila wakati kuwapa chakula au neno la faraja.
Mtakatifu Clara wa Montefalco
Kwa wanaume waliosoma, makuhani, na mapadre wa juu, alikuwa mshauri mwenye busara, mwenye uwezo wa kusoma mioyo ya wengine na kuona matukio. Yote haya licha ya jaribio kali la ukame wa kiroho ulimsumbua kwa miaka 11. "Nina Yesu wangu moyoni mwangu," alirudia baada ya Kristo kumtokea katika bustani ya monasteri kama msafiri anayeteseka, akimwambia: "Natafuta mahali pazuri ambapo naweza kupanda Msalaba, na hapa ndipo ninapopata mahali pazuri." Simumuli inasema kwamba Yesu, kama msafiri, alimpatia fimbo yake, na kwamba ilipopandwa, ilizaa mti, ambao bado unastawi hadi leo hii .
Ni Melia Azedarach, asili ya Himalaya, au "mti wa Mtakatifu Clara," ambao mbegu zake za miti zimetumika kwa karne nyingi kutengeneza rozari. Clara alifariki mnamo tarehe 17 Agosti 1308, na watawa wenzake waliamua kuhifadhi mwili wake. Kwa sababu hiyo, viungo vyake viliondolewa, na ishara za Mateso ya Kristo ziligunduliwa moyoni mwake: "katika umbo la mishipa migumu ya nyama, upande mmoja msalaba, misumari mitatu, sifongo, na mwanzi; na upande mwingine nguzo, mjeledi... na taji...
Katika mfuko wa nyongo... kulipatikana mawe matatu ya mviringo, yote yanafanana... ambayo yanawezekana yaliwakilisha Utatu." Sifa ya Clara ya utakatifu ilienea haraka, na miujiza kadhaa kupitia maombezi yake iliandikwa. Alitangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Leo XIII mnamo tarehe 8 Desemba 1881.
Misa ya Papa katika Kanisa la Mtakatifu Clara
Papa alitumia muda kuzungumza na watawa hawa, kisha akaadhimisha Misa katika Kanisa zuri la karne ya 17 lililobuniwa na mbunifu wa Peru, Valentino Martelli. Katika sehemu ya kulia, nyuma ya reli, kuna chombo cha fedha chenye mabaki ya Mtakatifu Clara. Madhabahu iliyowekwa wakfu kwake ina sehemu kubwa ya mbele ya stucco, iliyopambwa kwa nguzo, mahindi, fremu za mapambo, na sanamu mbili katika sehemu mbili za pembeni, zinazowakilisha Watakatifu Agostino na Jerome.
Sehemu zingine mbili zilizofunikwa na reli zina mabaki zaidi ya Clara, ikiwa ni pamoja na moyo wake, Siri za Mateso ya Kristo zilizogunduliwa hapo msalabani, na mawe matatu yaliyopatikana kwenye kibofu chake cha nyongo. Lakini mahali pa kusisimua zaidi pa Clara ni Kanisa la Msalaba Mtakatifu, lililopambwa kwa michoro mizuri ya karne ya 14. Hapo awali, Kanisa dogo alilokuwa amejenga na mahali palipochaguliwa kwa siku zake za mwisho za maisha yake, inasemekana kwamba miujiza mingi iliyosimuliwa katika michakato ya kutangazwa watakatifu ilitokea hapo.
![]()
Paa Leo XIV amekula chakula na watawa wa ndani wa kiagostino(@Vatican Media)
Chakula cha Mchana na Watawa
Watawa walimpatia Papa chakula cha mchana cha kawaida cha Umbria. Mkuu wa Monasteri Cristina Daguati, na watawa wenzake waliwasilisha kalenda ya 2026, "Kuelekea Amani Isiyo na Silaha," pamoja na maandishi kutoka katika hotuba na mahubiri yake na ya Mtakatifu Agostino, na michoro ya Sr Maria Rosa Guerrini, Mkuu mpya aliyechaguliwa hivi karibuni wa Shirikisho la Watawa wa Kiagostino nchini Italia, Picha ya Bikira Maria Mama wa Ushauri Jema " shirikisho alilokutana nalo hivi karibuni tarehe Novemba 12.
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu hapa: cliccando qui
