Papa atoa mabaki 62 ya sanaa kutoka Makumbusho ya Vatican kwa maaskofu wa Canada
Vatican News
Tarehe 15 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Jumba la Kitume na Askofu Pierre Goudreault, wa Jimbo la Mtakatifu Anna wa Pocatière na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada, akisindikizana na Askofu Mkuu Richard Smith, wa Jimbo Kuu la Vancouver, Padre Jean Vézina, Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu hilo.
Katika taarifa iliyotolewa pamoja na Vatican na Baraza la Maaskofu Canada, inabainisha kuwa “Wakati wa Mkutano huo Papa ametoa zawadi ya mabaki 62 ya kisanaa kutoka kwenye makusanyo ya kiutamaduni ya Makumbusho ya Vatican, kwa Baraza la Maaskofu wa Canada. Akihitimisha ile safari iliyoanzishwa na Papa Francisko, kupitia Ziara yake ya Kitume mnamo 2022 kwenda Canada, mikutano mbalimbali na Jumuiya za watu wa Asilia na kuchapishwa kwa Azimio la 2023 kuhusu Mafundisho ya Ugunduzi, ambapo Baba Mtakatifu Leo XIV alitaka zawadi hiyo iwakilishe ishara halisi ya mazungumzo, heshima, na udugu. Hili ni tendo la kushiriki Kanisa, ambalo Mrithi wa Petro alikabidhi mabaki haya kwa Kanisa nchini Canada, ambayo yanashuhudia historia ya kukutana kati ya imani na tamaduni za watu wa asilia.
Mabaki sitini na mbili, yanayotoka katika jumuiya mbalimbali, ambayo ni sehemu ya urithi uliopokelewa wakati wa Maonesho ya Kimisionari ya Vatican ya 1925, yaliyotangazwa na Papa Pio XI wakati wa Mwaka Mtakatifu, ili kutoa ushuhuda wa imani na utajiri wa kiutamaduni wa watu. yaliyotumwa Roma na wamisionari Wakatoliki kati ya 1923 na 1925, mabaki haya baadaye yalitiririka hadi Jumba la Makumbusho ya Kimisionari ya Lateran, ambalo baadaye likawa Jumba la Makumbusho la Kimisionari la "Anima Mundi" la Makumbusho ya Vatican.
Zawadi ya Baba Mtakatifu ni sehemu ya Jubilei ya 2025, ambayo inaadhimisha “Matumaini”, na “miaka mia moja ya Maonesho ya Kimisionari ya Vatican.” Mabaki haya ya sanaa, yakiambatana na taarifa zilizomo katika Makumbusho ya Vatican, ambayo yanathibitisha asili yake na hali ya kuhamishiwa kwao Roma kwa ajili ya Maonesho ya 1925, yaliwasilishwa katika Mkutano wa Maaskofu wa Canada, ambao, kwa roho ya ushirikiano mwaminifu na mazungumzo na Kurugenzi ya Urithi wa Utamaduni na Jiji la Vatican, wameazimia kuhakikisha kwamba yanalindwa, yanatangazwa na kuhifadhiwa vya kutosha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
