Tafuta

Papa Leo XIV:Wazee ni hekima ya watu,hazina kwa wajukuu,familia na jamii!

Papa akikutana na wazee huko Istanbul aliwambia wao ni hekima ya watu na hazina kwa familia na jamii.Ni katika siku yake ya pili Novemba 28 huko Türkiye,ambapo Papa alitembelea nyumba ya wazee inayohudumiwa na watawa wa Shirika wa Dada Wadogo wa Maskini nje kidogo mwa Istanbul.Neno,wazee,leo lina hatari ya kupoteza maana yake halisi.Katika miktadha ya kijamii,yenye ufanisi na ubinafsi vikitawala,hisia ya heshima kwa wazee imepotea.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV , Ijumaa tarehe 28 Novemba 2025 ikiwa ni siku ya Pili ya Ziara yake ya Kwanza ya Kitume nchini Türkiye- (Uturuki,) baada ya kukutana na Maaskofu, Mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume na wahudumu wa kichungaji, katika Kanisa Kuu la Rogo Mtakatifu, alikwenda kutembelea Nyumba ya Wazee iliyopo nje kidogo mwa mji wa Istanbul inayohudumiwa na watawa wa Dada Wadogo wa maskini.

Watawa Dada Wadogo wanaotunza wazee huko Istanbul
Watawa Dada Wadogo wanaotunza wazee huko Istanbul   (@Vatican Media)

Akianza hotuba yake Baba Mtakatifu Le XIV aliawasalimia  na kushukuru maneno ya Sista kwa kumkaribisha na kuwakaribisha wazee, kwa ukarimu wanaooneshwa na wote. "Ukarimu ni zawadi ya nyumba hii!“ Papa aliongeza, "Kiukweli ni zawadi inayotoka kwa Mungu na inatekelezwa na masista Wadogo wa Maskini, wafanyakazi, wafadhili, na pia na wakazi wote, katika maisha yenu ya kila siku pamoja. Asante kwa kila mtu!” Baba Mtakatifu alipenda kushirikishana nao  tafakari mbili fupi. "

Papa alikutana na wazee
Papa alikutana na wazee   (@Vatican Media)

Papa alisema "Ya kwanza limeongozwa na jina la watawa wenyewe wapendwa, kwa maana wao ni "Dada Wadogo wa Maskini." Hili ni jina zuri, na linalotufanya tufikiri! Ndiyo, Bwana amewaita si tu kuwasaidia au kuwasaidia maskini, bali pia amewaita kuwa "dada" zao”. Kwa namna hiyo  Papa aliongeza: “Mnapaswa kuwa kama Yesu, ambaye Baba alimtuma kwetu si tu kutusaidia na kututumikia, bali pia kuwa ndugu yetu. Siri ya upendo wa Kikristo ni kwamba kabla ya kuwa kwa ajili ya wengine, lazima kwanza tuwe na wengine katika ushirika unaotegemea udugu," Papa alishauri.

Wazee wanatunza na dada Wadogo wa Maskini
Wazee wanatunza na dada Wadogo wa Maskini   (@Vatican Media)

Tafakari ya pili Papa alisema imetokana wazee hao " wakazi wapendwa wa nyumba hii." Papa aliongeza "Ninyi ni wazee. Neno hili, "wazee," leo lina hatari ya kupoteza maana yake halisi. Katika miktadha mingi ya kijamii, ambapo ufanisi na ubinafsi vinatawala, hisia ya heshima kwa wazee imepotea. Kwa upande mwingine, Maandiko Matakatifu na tamaduni njema zinatufundisha kwamba, kama Papa Francisko alivyopenda kurudia  kusema kwamba: “wazee ni hekima ya watu, hazina kwa wajukuu zao, familia na jamii kwa ujumla.

Papa :"Wazee ni hekima ya familia na jamii"
Papa :"Wazee ni hekima ya familia na jamii"   (@Vatican Media)

Kwa hivyo, shukrani mara mbili kwa nyumba hii, ambayo inawakaribisha watu kwa jina la udugu, na hufanya hivyo hasa kwa wazee. Tunajua kwamba hii si rahisi kwani inahitaji uvumilivu mwingi na maombi. Kwa hivyo sasa, hebu tumwombe Bwana awasindikize na kuwategemeza. Kwa nyote, ninawaombea baraka za Mungu.”

Papa akiuhutubia wazee na watawa dada wadogo wa Maskini
Papa akiuhutubia wazee na watawa dada wadogo wa Maskini   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui

 

28 Novemba 2025, 12:09