Tafuta

Uchaguzi Mkuu Tanzania uliasababisha vifo na majeruhi kadhaa ambapo bado kujua idadi kamili. Uchaguzi Mkuu Tanzania uliasababisha vifo na majeruhi kadhaa ambapo bado kujua idadi kamili.  (AFP or licensors)

Papa Leo XIV:Tuwe wajenzi wa udugu katika dunia inayoteseka!

Kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa Leo XIV alikumbuka "sherehe kubwa" ambayo familia ya wanadamu imekusudiwa,tofauti na mikasa inayotesa dunia kutokana na dhuluma za siku hizi.Alitoa salamu zake kwa ujumbe wa Kanisa la Uingereza,waliofika Roma kwa ajili ya kutangazwa kwa Mtakatifu John Henry Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa na kwa washiriki wa "Mbio za Watakatifu."

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Chini ya anga lililikowa safi la blu, lenye mawingi meupe asubuhi Jumamosi tarehe 1 Novemba 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa wito wake kabla ya sala ya Malakia wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambapo pamoja na mwengine ya mtazamo wa furaha zaidi ya wakati ujao  lakini pia  yale ya dharura zaidi ya wakati huu unaomkubwa mwanadamu. Papa alisema “ Siku kuu ya Watakatifu Wote ni kumbukumbu hai, pumzi ya kina ya sherehe kubwa ambayo ubinadamu umekusudiwa. Kinachoizuia, wakati huo huo, ni migogoro na dhuluma za wakati huu, ambazo familia ya wanadamu inaitwa kukabiliana nazo kwa kujenga udugu.”

Misa ya kutangazwa Kardinali Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa
Misa ya kutangazwa Kardinali Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa   (@Vatican Media)

Utukufu wa leo unaelekeza macho yetu kuelekea "ukweli wa wakati ujao" wa mbinguni, furaha iliyoshirikishwa na Mungu, "iliyopo katika mambo yote katika yote," inayoweza kufichua "uzuri wa nyuso nyingi, zote tofauti na zote zinafanana na Uso wa Kristo." Hili linasimama katika tofauti kubwa na "yenye uchungu" na mikasa ya sasa, ambayo azimio lake limekabidhiwa kwa maombezi ya Bikira Maria na Watakatifu wote.

Kuwasalimia wajumbe wa Kanisa la Uingereza

Katika wito wake wa awali kabla ya sala ya Malaika, Papa aliwakaribisha na kuwasalimia wajumbe wa Kanisa la Uingereza wakiongozwa na Askofu Mkuu Stephen Cottrell wa York. Uwepo unaofufua "furaha" ulishirikishwa siku chache zilizopita katika "mkutano wa maombi ya kihistoria" na Mfalme Charles III wa Uingereza katika Kikanisa cha Kipapa cha Sistine. Matumaini ni kwamba Mwalimu mpya wa Kanisa, Mtakatifu John Henry Newman, "atawasindikiza Wakristo katika safari yao kuelekea umoja kamili."

Mshikamano wa "Mbio za Watakatifu"

Papa Leo XIV kadhalika alitoa salamu zake kwa washiriki vijana  katika Mbio za Watakatifu, tukio "linalochanganya michezo na mshikamano na watoto walio katika mazingira magumu zaidi." Sasa katika toleo la mwaka wa kumi na saba na kutangazwa na Utume wa  Don Bosco, mbio hizo zinapita katikati ya kituo cha kihistoria cha Roma na njia maalum ya Jubilei, inayounganisha basilika nne za Papa za mji mkuu.

Asante kwa kusoma makala hii.Ikiwa unataka kusasishwa,tunakualika kujiandikisha makala zetu kwa kubonyeza hapa: cliccando qui

01 Novemba 2025, 14:26