Papa Leo XIV:Vita vya Kwanza vya Dunia,ni mauaji yasiyo na maana
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV, akiwasalimu waamini wa Poland waliohudhuria Katekesi yake, tarehe 12 Novemba 2025 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alisisitiza thamani ya amani, akikumbuka kumbukumbu ya mwisho ya "mauaji yasiyo na maana" ya Vita vya Kwanza vya Dunia, kama Papa Benedikto XV alivyoiita, iliyoadhimishwa tarehe 11 Novemba 2025.
Papa Leo alisema "Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya amani," ambayo, kama Mtakatifu Agostino alivyosema, "hakuna kilicho bora zaidi. Tuihifadhi kwa mioyo iliyojikita katika Injili, katika roho ya udugu na upendo kwa nchi yetu." Baba Mtakatifu Leo XIV pia alikumbusha kwamba mwisho wa mgogoro huo, kwa watu wengi, wakiwemo Wapoland, uliambatana na "mapambazuko ya uhuru."
Akiwasalimu mahujaji wa Italia, Papa Leo XIV alikumbuka mfano wa Mama Eliswa Vakayil, mwanzilishi wa Shirika la tatu la Watawa wa Karmeli wa Mtakatifu Theresa aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri Jumamosi, tarehe 8 Novemba 2025 huko Kochi, katika jimbo la Kerala, India.
Papa Leo hasa alikumbuka kazi ya mtawa huyo kwa ajili ya wanawake walio pembezoni mwa jamii; kwa hivyo alionesha matumaini kwamba "kujitolea kwake kwa ujasiri kwa ajili ya ukombozi wa wasichana maskini zaidi" kutakuwa "chanzo cha msukumo kwa wote wanaofanya kazi, katika Kanisa na katika jamii, kwa ajili ya heshima ya wanawake."
Baba Mtakatifu pia aliwakumbusha waamini wa Kroatia, hasa wale wa Jimbo la Gospić-Senj, ambalo inaadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwake,wakisindikizwa na Askofu Marko Medo, kwamba "zawadi kubwa zaidi tunayoweza kutoa ni imani hai inayooneshwa kwa kuwajali wengine."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here
