Simulizi kwa picha za Siku ya II ya Papa Leo huko Türkiye

Baba Mtakatifu Leo XIV alikuwa na siku yenye msisimko mkubwa huko Istanbul, akianza na mkutano wa maombi na Maaskofu, Mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, na wahudumu wa kichungaji katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.

Katika tafakari yake Papa aliwakumbusha kwamba "nguvu ya kweli ya Kanisa" iko katika "mantiki ya udogo," si katika makubaliano ya idadi au nguvu, bali katika “kuamini ahadi ya Bwana.”

Kukutana na Wazee

Papa alikuwa mchangamfu na mwenye upendo wakati wa ziara yake kwenye makazi ya Masista Shirika la Dada Wadogo wa Maskini, ambao wamejitolea kwa zaidi ya miaka mia moja kwa ajili ya huduma ya upendo  kwa wengine.


Kilele cha maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso

Katika siku ya Papa Leo haikuishia hapo bali, kilele cha siku hiyo kilikuwa cha kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza wa  Nicaea katika sala ya pamoja kati ya Papa, Patriaki wa Kiekumeni wa Constantinople Bartholomew I, na viongozi na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo Ulimwenguni wakiwa juu ya magofu ya Basilika ya kale ya Mtakatifu Neophytos.

Baba Mtakatifu katika maombi hayo alitoa wito wa "kupinga vikali" matumizi ya dini kuhalalisha vita na vurugu, msimamo mkali, na ushabiki. Haya ndiyo yalikuwa matukio muhimu sana katika siku yake ya Pili kati ya siku sita atakazokuwa huko kwenye Ziara yake ya Kwanza ya Kitume kuanzia 27 Novemba hadi tarehe 2 Desemba 2025 kwa Türkiye- Uturuki na Lebanon.

 

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui

28 Novemba 2025, 20:11