PapaLeo XIV:"Vijana ni wahusika wakuu wa mstakabali wao wenyewe"
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 30 Machi 2026, alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia, mjini Vatican, Mfuko ambao unajihusisha na kuwasaidia vijana, ambapo katika hotuba yake aliwakaribisha akisema: “mwanzo wa Juma Takatifu, kipindi cha majaliwa ya Mungu kwa ajili ya kumfuata Bwana Yesu, aliyesulubiwa, akafa na kufufuka kwa ajili yetu.” Papa Leo XIV aliwashukuru “kwa kujitolea kwao kwa ukarimu kuwasaidia vijana katika njia zao za elimu na kazi.”
Kuwekeza si katika vitu, bali kwa watu
Papa Leo XIV alisisitiza kwamba: “Kuwekeza si katika vitu, bali kwa watu, katika ujuzi na uwezo wao, ni nguvu ya kazi yao.” Kwa hiyo vijana wenyewe “wanakuwa wahusika wakuu wa mustakabali wao wenyewe, badala ya kuchukuliwa kama zana tu katika kupanga kampuni au katika mafanikio yake ya kibiashara.”
Mzunguko mzuri wa maarifa na ushirikiano
Baba Mtakatifu kadhalika, aliwahimiza mwanachama hao wa Mfuko wa Ausilia, “kuendelea katika mipango wanayohamasisha: hasa katika hali ya sasa ya kutokuwa na uhakika, mzunguko mzuri wa maarifa na ushirikiano wanaohamasisha, kwa hakika utatoa matunda.” Kama ishara ya heshima yake. Papa alifurahi kuwapatia Baraka yake ya Kitume wote waliokuwapo hapo na wapendwa wao.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
