Tafuta

Katika nyayo za Kiagostino,Papa Leone XIV kwa kimya na sala katika mabaki ya Hippo

Eneo la akiolojia na la Askofu wa kale,Baba wa Kanisa ni kituo cha kwanza katika siku ya Pili ya Ziara ya Papa nchini Algeria.Kutokana na hali mbaya ya hewa na mvua kubwa,ziara ya kutembelea mitaa ya jiji la bandari lililokuwa likistawi ilifupishwa.Papa alipanda mzeituni na kuweka shada la waridi jeupe na njano.

Tiziana Campisi–Mwakilishi Annaba na Angella Rwezaula–Vatican.

Mvua kubwa ilinyesha Annaba; ikawa siku ya kijivu. Lakini miongoni mwa magofu ya Hippo ya kale, yaliyopita na ya sasa yalionekana kuungana. Enzi mbili tofauti, zilizotenganishwa zaidi ya karne kumi na sita, lakini ambazo ujumbe huo huo unafikia ulimwengu, kutoka kwa Mtakatifu Agostino na Papa Leo XIV: tunaweza kuishi kama ndugu tukijenga amani pamoja. Ni siku ya pili ya Ziara yake ya kitume ya Papa kuwa barani Afrika, moja ya siku zinazotarajiwa sana.

Papa alitembelea maeneo ya akiolojia huko Annaba
Papa alitembelea maeneo ya akiolojia huko Annaba   (@Vatican Media)

Papa wa kiagostino, kupitia mvua iliyoonyesha, alitembea sehemu fupi ya eneo la akiolojia, sehemu ya barabara inayopitiwa mara nyingi na Askofu Aurelius Augustinus, mzaliwa wa Thagaste, sasa Souk Ahras, na Askofu wa jiji la bandari linalostawi. Kwa kupanua mtazamo wa macho, mtu anakumbatia kilima cha Annaba na Kanisa kuu au Basilika  ya  Baba wa Kanisa. Kwa hiyo jana na leo, na Papa wa kwanza katika ardhi ya Algeria anayemheshimu Baba yake wa kiroho, na kukusanya urithi wake na kutoa sauti tena kwa mwaliko wake wa kuishi kwa amani, ili kuwe na amani miongoni mwa watu. Kwa sababu, kama laivyo sisitiza "amani ndiyo mwisho wa mema yetu," aliandika Agostino katika "Mji wa Mungu," katika sura ya XIX (11), ambapo anarudia neno "amani" zaidi ya mara mia moja.

Papa alipanda mti wa Mzeituni
Papa alipanda mti wa Mzeituni   (@Vatican Media)

Miongoni mwa magofu ya jiji ambalo Agostino aliishi

Akisalimiwa kwenye mlango wa uchimbaji na Afisa wa eneo hilo, Papa Leo XIV alibanisha akiguswa sana, magofu ya Hippo Regius, yaliyokaliwa hadi karne ya 5 na wavuvi, mabaharia, Askari, wafanyabiashara, mafundi, maafisa, na wakulima, pamoja na familia tajiri, wamiliki wa meli.

Wakati wa kupanda na kumwagilia mti wa mzeituni
Wakati wa kupanda na kumwagilia mti wa mzeituni   (@Vatican Media)

Hali mbaya ya hewa ililazimisha sherehe iwe fupi, ambapo Papa Leo XIV, chini ya Tenti, kwa msaada wa Skauti wawili wachanga, aliweka shada la waridi nyeupe na njano na kisha akapanda mzeituni, ishara ya amani na inayokumbusha mti wa mzeituni wa karne nyingi katika mji wake wa nyumbani, ambao mila na tamaduni  inashikilia tangu wakati wake.

Watu wa Annaba
Watu wa Annaba   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV alibaki amezama katika maombi kwa muda mfupi, mikono yake ikiwa imeshikamana. Wakati huo huo, njiwa weupe waliachiliwa kwenye anga lenye , lililojaa mvua, huku kwaya ya Taasisi ya Muziki ya Annaba ikiimba nyimbo kwa Kilatini, Berber, na Algeria, huku maandishi ya Askofu wa Hippo kuhusu amani na udugu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

14 Aprili 2026, 15:02