Tafuta

 Bwana Isaac Herzog,Rais wa Serikali ya Israeli alipokutana na Papa Leo XIV kunako mwaka 2025. Bwana Isaac Herzog,Rais wa Serikali ya Israeli alipokutana na Papa Leo XIV kunako mwaka 2025.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV na Rais Herzog:kufungua tena njia za kidiplomasia

Katika hafla ya kipini cha Pasaka,simu ilifanyika asubuhi ya Ijumaa Kuu,Aprili 3,kati ya Papa na Mkuu wa Nchi ya Israeli.Haja ya kufungua tena mazungumzo ya kidiplomasia ilirudiwa"kwa lengo la amani ya haki na ya kudumu katika Mashariki ya Kati."Umuhimu wa kuwalinda raia na kukuza heshima kwa sheria za kimataifa na za kibinadamu ulisisitizwa.

Vatican News

Katika siku ya jumaa Kuu Takatifu asubuhi tarehe 3 Aprili 2026 , Baba Mtakatifu Leo XIV alizungumza kwa simu na Mheshimiwa Isaac Herzog, Rais wa Nchi ya Israeli, katika fursa ya siku kuu ya Pasaka. Haya ni maelezo kutoka taarifa za Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu. “Wakati wa mazungumzo hayo, taarifa inasomeka, “ hitaji la kufungua tena njia zote zinazowezekana za mazungumzo ya kidiplomasia lilirudiwa, ili kukomesha mzozo mkubwa unaoendelea, kwa lengo la kufikia amani ya haki na ya kudumu Mashariki ya Kati yote.”

Taarifa hiyo aidha imebainisha kuwa, “Mazungumzo hayo pia yalilenga umuhimu wa kuwalinda raia na kuhamasisha heshima kwa sheria za kimataifa na za kibinadamu.

SIMU PAPA NA RAIS WA ISRAELI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

03 Aprili 2026, 16:12