Tafuta

2026.05.15 Misa kwa ajili ya Mazishi ya Kardinali Paul Emil Tscherring katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. 2026.05.15 Misa kwa ajili ya Mazishi ya Kardinali Paul Emil Tscherring katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Kard Tscherrig alijitolea kama mwanadiplomasia na zaidi kama mchungaji wa Kanisa

Papa Leo XIV aliongoza ibada ya Misa ya Mazishi ya Kard.Tscherrig,ambapo katika mahubiri alikumbuka utume wa Kardinali katika nchi mbalimbali kwa uvumilivu na kujitoa,kuwakusanya watu pamoja kwa maelewano huku akikabiliwa na vikwazo na changamoto ambazo mwakilishi wa Papa anaitwa kukumbatia kwa ajili ya mema ya wote.Kardinali wa Uswiss,mwanadiplomasia wa muda mrefu na Balozi wa Kitume nchini Italia na San Marino,alifariki Mei 12.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa alasiri tarehe 15 Mei 2026, aliongoza misa ya mazishi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Kardinali Paul Emil Tscherrig, wa Uswisi ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 79 mnamo tarehe 12 Mei 2026. Katika mahubiri yake Papa alimfafanua kama Kardinali, “kaka, mwanadiplomasia, mchungaji, ambaye alihudumia Kanisa la ulimwengu kwa kazi ambayo mara nyingi haikuwa ya kuvutia, lakini hata hivyo ilikuwa ya bidii na yenye kuhitaji juhudi.” Papa alifamfafanua Kardinali mpendwa ambaye, miongoni mwa majukumu yake mbalimbali, aliongoza Ubalozi wa Vatican nchini Italia na San Marino kuanzia 2017 hadi 2024, wa kwanza asiye Mwtaliano kushika wadhifa huo. Aliundwa kuwa Kardinali na Papa Francisko katika Baraza Kuu la Makardinali la tarehe 30 Septemba 2023, mwaka huo huo pamoja na Robert Francis Prevost aliyepokea ukardinali.

Misa ya Mazishi ya Kardinali Tscherrig
Misa ya Mazishi ya Kardinali Tscherrig   (@Vatican Media)

Kumtumikia Bwana wa ukarimu

Na kwa hiyo Papa Leo XIV ali msindikiza kwamba: "Kaka huyu katika mkutano mkuu na mzito na Bwana ambaye alimtumikia kwa ukarimu, pamoja na Rafiki ambaye alitembea kando yake kwa uaminifu katika maisha yake yote, zaidi ya nusu yake alitumika katika huduma ya Kiti cha Ubalozi wa Vatican kwa Uwakilishi mbalimbali wa Kipapa na katika Sekretarieti ya Vatican." Papa Leo  katika mahubiri hayo alimweleza alivyokuwa mvumilivu na kijikana kuwa: "Kujitolea kwake kama mwanadiplomasia, na zaidi kama mchungaji wa Kanisa," kumemwona ndugu yetu huyu akifanya kazi kwa miaka mingi, kwa uvumilivu na kutokuwa na ubinafsi, kukusanya watu waliokabidhiwa utunzaji wake kwa utii, hata kukabiliana na vikwazo na changamoto ambazo mwakilishi wa papa anaitwa kukumbatia kwa manufaa ya wote."

Makardinali
Makardinali   (@Vatican Media)

Uzoefu wa kidiplomasia katika nchi mbali mbali

Papa Leo XIV  alikumbuka tena  uzoefu mkubwa wa kikanisa na kimataifa wa Kardinali Tscherrig huko Burundi, Trinidad na Tobago, na mataifa kadhaa ya Caribbean, Korea Kusini, Mongolia, na baadaye Sweden, Denmark, Finland, Iceland, Norway, na Argentina, hatimaye akawasilisha Italia na San Marino. "Uzoefu mkubwa wa kikanisa na kimataifa, unaoshuhudia upatikanaji wake na uwezo wake wa kubadilika, katika upendo wake  kama Mchungaji, katika mazingira tofauti sana: maeneo na watu aliotumwa, kwa niaba ya Baba Mtakatifu, kuunganisha uhusiano wa ushirika kati ya Makanisa mahalia na Kiti Kitakatifu, pamoja na kuimarisha vifungo vya urafiki." Baba Mtakatifu aliendelea kuwa: “Sasa Kardinali Paul Emil anakutana na Bwana wake na tunamsindikiza katika kifo hiki cha ajabu” huku akitumaini kwamba, “wakati huu unaweza kuwa fursa ya kutafakari na kutia moyo, kuthamini wema alioutoa, kwa neema ya Mungu, kwa imani na kujitolea. Dunia Yetu inahitaji wahudumu wa Bwana wa kuitikia wito wake.

Mazishi ya Kardinali Paul Emil
Mazishi ya Kardinali Paul Emil   (@Vatican Media)

Kufanya matumaini yasitawi na matarajio mema ya watu

Katika mahubiri yake  Papa Leo XIV alinukuu hotuba ambayo Papa Francisko alikutana na Tscherrig huko Buenos Aires na ambaye aliwahimiza wanadiplomasia "kufanya matumaini yastawi karibu nao, kama jibu la hamu na matarajio mema ya watu. "Ni mwaliko, ambao sisi pia tunaweza kuukubali leo hii kuutekeleza popote tunapoitwa kuwatumikia na kuwapenda kaka  na dada zetu. Dunia yetu inahitaji sana wajumbe ambao wanaweza kuisaidia kupata tena uaminifu, na ushuhuda mzuri wa wale ambao Mungu amewachagua kama wahudumu wake unaweza kutusaidia katika kuitikia wito huu."

Mazishi ya Kardinali Tscherrig

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

15 Mei 2026, 17:20