Tafuta

Papa Leo XIV na Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella. Papa Leo XIV na Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella.  (@Vatican Media)

Papa kwa Mattarella:Asante kwa umakini wa maisha ya kikanisa nchini Italia

Papa Leo XIV alituma telegramu kwa Rais wa Jamhuri ya Italia wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 85,akimhakikishia maombi yake kwa ajili ya"kazi kubwa"inayofanywa kwa ajili ya kuwahudumia watu na kumkabidhi kwa maombezi ya Watakatifu walinzi wa nchi,Francis wa Assisi na Catherine wa Siena.

Vatican News

Shukrani kwa "umakini wa kila mara" ambao "maisha ya kikanisa na kijamii" ya Italia yanasindikizwa na kwa kuwategemea watakatifu wake walinzi, Francis wa Assisi na Catherine wa Siena. Hivi ndivyo Papa Leo XIV alivyozungumza na Rais wa Jamhuri ya Italia, Sergio Mattarella, katika telegramu iliyotumwa tarehe 23 Julai 2026, wakati wa siku yake ya kuzaliwa  miaka 85 iliyopita. Salamu hii, maandishi yanaendelea, "inaambatana na baraka ya kitume iliyotolewa kwa familia yake, washirika, na "Italia pendwa" yenyewe."

Ziara ya Papa Leo XIV Ikulu ya Italia

Askofu wa Roma alitembelea Ikulu ya Italia mnamo tarehe 14 Oktoba 2025, akitoa hotuba iliyolenga ushirikiano wa pande nyingi na usaidizi kwa familia barani Ulaya ambapo kiwango cha kuzaliwa kinapungua sana ambapo  Papa Leo XIV alibainisha, "kinapungua sana." Baba Mtakatifu pia aliakisi vita vinavyoendelea ulimwenguni kote, akialika kutazama nyuso za wengi "waliozidiwa na ukatili usio na maana wa wale wanaopanga kifo na uharibifu bila huruma" katika vita vingi "vinavyoharibu sayari yetu," na kusikiliza kilio chao.

Rais Mattarella, kwa upande wake, alisisitiza kujitolea kwa Papa Leo XIV kwa "umoja wa utu wa mwanadamu" na mazungumzo. Ahadi hii ilirudiwa mara kwa mara na kusifiwa na Rais katika jumbe zingine zilizotumwa kwa Papa, kama vile ile ya mwaka mmoja baada ya kuanza huduma yake kama Kharifa wa Mtume Petro na wakati wa Pasaka.

PAPA KWA MATTARELLA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

23 Julai 2026, 19:10