Subiaco,Papa Leo XIV atembelea Monasteri za Mtakatifu Benedikto na Mtakatifu Scholastica!
Vatican News
Asubuhi ya Jumatano tarehe 22 Julai 2026, Papa Leo XIV aliondoka kwenye Madhabahu ya Utatu Mtakatifu, mojawapo ya sehemu za ibada zinazoheshimiwa zaidi katika Vilima vya Kati vya Mkoa wa Lazio na yapata saa sita mchana kwa gari walifika kwenye Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco,ikiwa ni kilomita thelathini kutoka hapo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican ilitangaza kwenye akaunti yake ya Telegram kwamba, "wakati wa ziara yake kwenye Monasteri hiyo alisimama kimya kimya akitafakari mbele ya sanamu ya karne ya 13 ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Na katika Pango Takatifu, alibusu goti la sanamu ya Mtakatifu Benedikto, kama ilivyo desturi, na akasali Sala ya Bwana pamoja na wale waliokuwepo."
Hatimaye, alipanda hadi Monasteri ya Mtakatifu Scolastica, ambapo alisimama kwa chakula cha mchana na jumuiya ya Wabenediktini na kutembelea mazingira ya watawa. Baada ya saa 10:00 jioni, Papa Leo XIV na wenzake waliondoka kurudi Castel Gandolfo.
![]()
Wakati wa Kutembelea Monasteri ya Wabenediktini wa Subiaco (@Vatican Media)
Furaha na Shukrani za Jumuiya ya Wabenediktini
"Jumuiya ya Wabenediktini ya Subiaco inakaribisha kwa furaha na shukrani ziara ya Mtakatifu Leo XIV katika Monasteri Takatifu, mahali ambapo Mtakatifu Benedikto alianza safari yake ya kiroho." Hivi ndivyo Abate wa Kawaida wa Subiaco, Dom Mauro Meacci, alivyoliambia Shirika la habari za Kanisa la Italia(SIR.)"Uwepo wa Baba Mtakatifu," aliendelea, "unafufua uhusiano kati ya Kanisa na karama ya Wabenediktini, ukimkumbusha kila mtu umuhimu wa sala, kusikiliza Neno, na kutafuta amani."
Ujumbe ulioachwa na Papa kwa jumuiya ya watawa
Katika kitabu cha wageni cha Monasteri ya Mtakatifu Benedikto, Papa aliandika: "Ombeni na mfanye kazi... Ushuhuda wa watawa wa Benedikto ni halali na muhimu sana katika Kanisa na katika ulimwengu wa leo. Ninaishukuru jumuiya hii kwa mapokezi yao mazuri, na ninawaalika kusali pamoja na Kanisa lote kwa ajili ya amani duniani. Ni ninatoa baraka yangu katika siku kuu ya Mtakatifu Maria Magdalena."
Na katika kitabu cha wageni cha Monasteri ya Mtakatifu Scholastica, aliandika: "Ninamshukuru Bwana kwa neema ya kuweza kutembelea mahali hapa patakatifu, katika siku kuu ya kiliturujia ya Mtakatifu Magdalena, aliyekuwa wa kwanza kutangaza Ufufuko wa Bwana."
![]()
Wakati wa kutembelea Jengo la Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco(@Vatican Media)
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
